Ulusumo lunulo, lwingila kuli munhu uyo ocholaga gupandika ng’ombe mulugutu lo ng’ombe, umujigalalilaga. Umunumo jigalekaga tembe iyo adulile umunhu nulu gulibhila amagulu gakwe uyo wingila moyi.
Umunhu ng’wunuyo agayukoya ugugafunya amagulu gakwe kunguno ya gulibhila umutembe ija ng’ombe ijojalijachilulwa jugading’wa. Agang’wila ung’wiye uyo bhali nawe, “ahenaha jilihoyi ing’ombe ningi noyi kunguno itembe jiniji jiliningi mpaga nalikoya ugugafunya amagulu gane.” Ung’wiye aganshokeja aliyomba, “ugukoyaga na tembe ing’ombe jachilulaga.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo uyo gudina na solobho yose yose. Umunhu ng’winuyo agajimijaga makanza gakwe bho nduhu solobho, ukunhu alijimala sagala ninguzu jakwe. Uweyi agamalaga nguzu jakwe bho nduhu gupandika solobho yose yose.
Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga nimo uyo gudikilile nu munhu uyo agukoyelaga tembe ja ng’ombe umo jitiho ing’ombe jinijo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga umunhu ng’wunuyo giki, “ugukoyaga na tembe ing’ombe jachilulaga.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka gutumama milimo iyo idina solobho yose yose, kunguno bhagujimija makanza gabho sagala. Gashinaga lulu, igelelilwe bhaisolanye imilimo iyo idulile gubhenhela solobho ningi, umuwikaji bhobho, hunabhayitumama lulu iyiniyo.
Mathayo 13:5-7.
Wagalatia 6:7-10.
UNAHANGAIKA NA TOPE (KINYESI CHA NG’OMBE) NG’OMBE WAMEENDA MACHUNGANI.
Methali hiyo ilianzia kwa mtu aliyekuwa akitafuta kupata ng’ombe, akiwa ndani ya zizi la ng’ombe waliokuwa wameenda machungani. Kwenye zizi hilo, kulikuwepo na tope la kinyesi cha ng’ombe la kuzamisha miguu yake yule anayeingia
Mtu huyo, alianza kuhangaika kuitoa miguu yake kwenye matope hayo kwa sababu ilikuwa imezama kwenye zizi hilo la ng’ombe waliokuwa wameenda machungani. Alimwambia mwenzake, “hapa pana ng’ombe wengi sana kwa sababu ya kinyesi au tope hili kuwa jingi mpaka nahangaika kuitoa miguu yangu.” Mwenzake akamjibu akisema, “unahangaika na tope (kinyesi cha ng’ombe) ng’ombe wameenda machungani.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi isiyo na faida yoyote. Mtu huyo, hupoteza wakati wake bure, huku akizimaliza hovyo nguvu zake hizo. Yeye huzimaliza nguvu zake hizo kwa kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu na bila faida yoyote.
Mtu huyo, hufananishwa na mtu anayehangaika na kinyesi cha ng’ombe kilichoachwa zizini na ng’ombe walioenda kuchungwa. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “unahangaika na tope (kinyesi cha ng’ombe) ng’ombe wameenda machungani.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kupoteza muda wao katika kufanya kazi isiyo na faida yoyote, maishani mwao. Kumbe basi, wanatakiwa kuzifanyia utafiti kazi zao, ili waweze kuzichagua na kuzitekeleza zile zinazowaletea faida katika kuziendeleza familia zao.
Mathayo 13:5-7. “Nyingine zikaanguka sehemu yenye mawe, ambapo hapana udongo mwingi. Zikaota haraka kwa sababu udongo ulikuwa hauna kina. Lakini jua lilipozidi, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikuwa na kina. Mbegu nyingine zilianguka katikati ya miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga.”
Wagalatia 6:7-10. “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.”
ENGLISH: YOU ARE STRUGGLING TO FREE YOURSELF FROM THE COW DUNG BUT THE CATTLE HAVE GONE TO THE PASTURES
This proverb is tailored around a man who was looking for cattle, in a cowshed but the cattle were not there. They had gone to the pasture in the plains. They had left behind a mountain of fresh cow dung which made him stuck into it to the point of failing to get out of it
Seeing that the cattle he was looking for were not there and having been stuck his feet being stuck in the mud, he began struggling to get them out of the fresh cow doing. Seeing the amount of fresh dung, he told his colleague, “There must be many many cows in this shed because of the amount of cow dung I See. Look, this cowdung is so thick that I am not sure to get my feet out of it.” His companion replied, “You are so obsessed with the mere cow dung. Remember the cattle have gone to the pastures.”
This proverb is likened with a man who works in vain. Such man wastes his time as well as his energy.
Someone who wastes his energy and time for nothing is likened with a man who is struggling to get out of fresh cowdung left in the cowshed by the cattle which have gone to pasture
This proverb teaches people to stop wasting their time by doing useless work, in their lives. Therefore, they need to choose and implement only those activities that can benefit them in the development of their families.
Matthew 13: 5-7 Galatians 6: 7-10.