723. OSHELA HA NYAGA.

Oliho mayu umo uyo oshaga bhusiga, aliyo lulu oshelaga haluyaga. Ubhufu bhokwe bhomanaga bhuchalwa na luyaga. Aho omala ugusha wisanga bhoshilaga guchalwa na nyaga ubhufu bhoke. Aho obhugaiwa ubhufu agayomba, “nanoga bhure kunguno nu bhufu nagaiwa.” Abhiye bhung’wila giki, “oshela ha nyaga.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo uyo gudina na solobho yose yose. Umunhu ung’winuyo agajimijaga makanza gakwe bhure ukunhu alijimala sagala inguzu jakwe. Uweyi agamalaga nguzu jakwe bho nduhu gupandika solobho yose yose.

Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga nimo uyo gudikilile na munhu uyo alishela bhusiga bhokwe ha nyaga aho bhugamanaga bhuchalwa ubhusu ubho alibhusha. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga umunhu ng’wunuyo giki, “oshela ha nyaga.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka gutumama milimo iyo idina solobho yose yose, kunguno bhagujimija makanza gabho sagala. Gashinaga lulu, igelelilwe bhaisolanye imilimo iyo idulile gubhenhela matwajo mingi, umuwikaji bhobho, hunabhayitumama lulu iyiniyo.

Mathayo 13:5-7.

Wagalatia 6:7-10.

KISWAHILI: UMESAGIA KWENYE UPEPO.

Alikuwepo mama mmoja ambaye alikuwa anasaga mtama, lakini alikuwa anasagia kwenye upepo. Unga wake ulikuwa ukichukuliwa na upepo. Alipomaliza kusaga akajikuta hana unga, akasema, “nimechoka bure na unga nimekosa.” Wenzake wakamwambia kwamba, “umesagia kwenye upepo.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi isiyo na faida yoyote. Mtu huyo, hupoteza wakati wake bure huku akizimaliza hovyo nguvu zake hizo. Yeye huzimaliza nguvu zake hizo kwa kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu na bila faida yoyote.

Mtu huyo, hufanya kazi ambayo haiko tofauti na mtu aliyesagia mtama wake kwenye upepo ambao ulikuwa unauchukua unga wake aliokuwa akiusaga. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “umesagia kwenye upepo.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kupoteza muda wao katika kufanya kazi isiyo na faida yoyote maishani mwao. Kumbe basi, wanatakiwa kuzifanyia utafiti kazi zao, ili waweze kuzichagua na kuzitekeleza zile zinazowaletea faida katika kuziendeleza familia zao.

Mathayo 13:5-7. “Nyingine zikaanguka sehemu yenye mawe, ambapo hapana udongo mwingi. Zikaota haraka kwa sababu udongo ulikuwa hauna kina. Lakini jua lilipozidi, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikuwa na kina. Mbegu nyingine zilianguka katikati ya miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga.”

Wagalatia 6:7-10. “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.”

mayu nshi

stone-grinding.1

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.