722. KUBHIBHA MU MASWA KUSHELA HASI.

Bhaliho bhanhu bhadatu, abho bhikalaga hakaya yimo, aliyo bhuli ng’wene otumamaga nimo gokwe, uyo goli heka nugo bhiye. Uogwandya olimaga bho gujib’ib’a inbuyu mumaswa, uokabhili oshelaga bhusu hasi, uokadatu ojidimaga mitugo.

Unimi agang’wila unshi, “udashelage hasi kunguno bhugujimila mmasalu ubhufu bhoko.” Unshi nawe agashosha, “unene nadulile gubhusungula ubhusu nubhupandika nulu bhugehu, alubhebhe iki ulijibhibha mumaswa inbiyu jako, udujijimijaga sagala lulu?” Hunaubhawila undimi omitugo giki, “kubhibha mu maswa kushela hasi.”

 Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agunlangaga munhu uyo adigwaga iyo alilangwa.  Ukwene huguhaya giki, alijimija mihayo na makanza gakwe dalali. Ilinduhu solobho yose yose ukuli nangi kunguno unangwa alisawa na gulu.

Umunhu ng’wunuyo agatumamaga nimo uyo gudikilile na munhu uyo alishela bhusu bhokwe hasi, nulu uyo alib´ib´a mbiyu jakwe mu maswa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “kubhibha mu maswa kushela hasi.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka gutumama milimo iyo idina solobho yose yose, kunguno bhagujimija makanza gabho sagala. Gashinaga lulu, igelelilwe bhaisolanye imilimo iyo idulile gubhenhela matwajo mingi, umuwikaji bhobho, hunabhayitumama lulu iyiniyo.

Mathayo 13:5-7.

Wagalatia 6:7-10.

KISWAHILI: KUSIA KWENYE MAJANI KUSAGIA CHINI.

Walikuwepo watu watatu waliokuwa wakiishi kwenye familia moja, lakini kila mmoja alifanya kazi tofauti na ya mwingine. Wa kwanza alikuwa analima kwa kuzimwaga mbegu kwenye majani, wa pili alikuwa anasagia unga chini, na wa watatu alikuwa mchungaji wa mifugo.

Mkulima alimwambia msagaji, “usisagie chini kwa sababu unga wako utapotea kwenye mchanga.” Msagaji akajibu, “mimi naweza kupepeta walau nikapata unga kidogo, nawewe kwa vile unasia mbegu kwenye majani, huzipotezi hovyo mbegu zako hizo?” Ndipo yule mchungaji wa mifugo akawaambia kwamba, “kusia kwenye majani kusagia chini.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule anayemfundisha mtu asiyesikia kile anachofundishwa. Kumfundisha mtu kama huyo, ni kupoteza maneno na wakati wake bure. Hakuna faida yoyote kwa mfundishaji, wala kwa yule anayefundishwa, kwa sababu mtu yule ni sawa na kiziwi.

Mtu huyo, hufanya kazi ambayo haitofautiani na mtu anayesagia unga wake chini, au yule anayesia mbegu zake kwenye majani. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kusia kwenye majani kusagia chini.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kupoteza muda wao katika kufanya kazi isiyo na faida yoyote maishani mwao. Kumbe basi, wanatakiwa kuzifanyia utafiti kazi zao, ili waweze kuzichagua na kuzitekeleza zile zinazowaletea faida katika kuziendeleza familia zao.

Mathayo 13:5-7. “Nyingine zikaanguka sehemu yenye mawe, ambapo hapana udongo mwingi. Zikaota haraka kwa sababu udongo ulikuwa hauna kina. Lakini jua lilipozidi, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikuwa na kina. Mbegu nyingine zilianguka katikati ya miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga.”

Wagalatia 6:7-10. “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.”

GRASS

farmer-1

ENGLISH: SOWING ON GRASSES IS LIKE GRINDING CORN ON THE FLOOR.

There were three people living in the same family, but each had a different job from the rest. The first was plowing and sowing seeds, the second was grinding flour, and the third was a herdsman.

The farmer told the one who was grinding, “don’t leave it on the ground because your flour will be lost in the sand.” The one who was grinding replied, “I can sift at least a little flour, and since you leave the seeds in the leaves, don’t you see that you are wasting your seeds?” The herdsman then told them, “Sowing on grasses is like grinding on the floor.”

This proverb is likened with a person who teaches another who does not observe or take note of what he is being taught. Teaching such a person is a waste of time and effort. There is neither benefit to the instructor, nor to the one who is being taught, because that person is like the deaf who never hears anything.

That person is like a person who grinds his flour on the ground, or one who sows his seeds on grasses. That is why the saying goes, “Sowing on grasses is like grinding on the floor.”

This proverb teaches people to stop wasting their time by doing useless things in their lives. Therefore, they should be discriminating in their practices by avoiding doing things which are useless or wastage of time. Instead, they should choose doing things that are beneficial to themselves and their families.

Matthew 13: 5-7. Galatians 6: 7-10.

mbula-compound-60 from Aimee

One comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.