721. NG´WANA WA NZOKA ADIBHENGAGWA.

Olihoyi munhu uyo oli na nhungwa ja gujidarahija ijisumva ijidololo guti kana ka nzoka. Umunhu ng’wunuyo agagema kugigusija kana ka nzoka kunguno ya kugadalahija giki kadikomile ugunuma. Abhiye bhagang’wila, “lekaga ugukigusija akayoka kenako kaguguluma.” Uweyi agabhalemeja aliyomba, “kaduniluma kunguno katali kadololo noyi. Abhiye bhung’wila, “ng’wana wa nzoka adibhengagwa.’ Aho wigwa chene agogoha ukaleka, kunguno agadebha igiki gashinaga kadulile gunuma iki ung’wana o nzoka nang’hwe nzoka, gutumo bhahaila abhanhu abha kale.

Ulusumo lunulo lulolile, jisumva ijo jili na bhusungu ubho bhudibho gudalahijiwa. Inzoka idulile gubhenhela nhabhala abho ilabhalume kunguno ya bhusungu bhoyo, iki mumo igadohela ubhusungu bhoyo bhuli giti bho nzoka nhale. Gashinaga lulu uyo yunuma agupandika makoye na adulile nulu gucha ulu adingijiwe ubhusungu bhunubho.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adadabhalelaga chiza abhana bhakwe nulu bhalita mihayo ya bhubhi agabhilolelaga duhu. Umunhu ng’wunuyo agabhalekanijaga abhana bhakwe bhenabho bhakula na nhungwa ja bhubhi ijo jigikolanijiyagwa na bhusungu bho ng’wana wa nzoka.

Inhungwa jinijo, jidulile gung’wenhela nhabhala umunhu ng’wunuyo, umuwikaji bhokwe iyo ikolile na ya gulung’wa nzoka iyo ili na bhusungu. Gashinaga igelelilwe  abhana bhapandike ilange lya gudula gubhingija inhungwa ija bhubhi, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ng’wana wa nzoka adibhengagwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gufunya ilange lya wiza ukubhana bhabho, kugiki bhadule gukula bhajilekile inhungwa ija bhubhi, umuwikaji bhobho. Igelelilwe abhanhu bhaleke ugulunga bhunwani na bhanhu abho bhali na kajile kabhubhi, umuwikaji bhobho.

Marko 10:13-14.

1Wakorintho 1:19-20.

KISWAHILI: MTOTO WA NYOKA HADHARAULIWI.

Alikuwepo mtu aliyekuwa na tabia ya kudharau viumbe vidogo wakiwemo watoto wa nyoka. Mtu huyo, alijaribu kucheza na mtoto wa nyoka kwa sababu alimdharau akimfikiria kwamba hataweza kumdhuru. Wenzake wakamwambia, “acha kumchezea huyo mtoto wa nyoka atakuuma.” Yeye alikataa akisema, “hataweza kuniuma kwa sababu bado ndogo mno.” Wenzake wakamwambia, “mtoto wa nyoka hadharauliwi.” Aliposikia hivyo aliogopa na kumuacha mtoto huyo, kwa sababu alielewa kwamba kumbe mtoto wa nyoka naye ni nyoka, kama walivyosema watu wa zamani.

Methali hiyo huangalia viumbe vyenye sumu isiyo takiwa kudharauliwa. Nyoka aweza kuwaletea matatizo wale atakaowauma kwa sababu ya sumu yake ilivyo kali na ya hatari. Kumbe basi, mtu yule atakayeumwa na yule nyoka atapata matatizo yawezayo hata kupelekea kifo chake kama sumu hiyo haitawahiwa kuondolewa.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hawalei vizuri watoto wake. Yeye huacha kuwaonya hata kama wanatabia mbaya. Mtu huyo huwatelekeza watoto wake hao kwa kuwaacha wakue wakiwa na tabia zao mbaya zinazofananishwa na sumu ya mtoto wa nyoka, maishani mwao.

Tabia hizo mbaya zaweza kumletea matatizo mtu huyo katika maisha yake, yanayofanana na nyoka mwenye sumu. Kumbe basi, inafaa watu wawapatie malezi mema watoto wao wangali bado wadogo ili waweze kuyaendeleza vyema maisha yao. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtoto wa nyoka hadharauliwi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwapa malezi mema watoto wao tangu wakiwa wadogo, ili waweze kukua wakiwa na tabia njema maishani mwao. Yafaa pia watu waache kushikana urafiki na watu wenye tabia mbaya, katika maisha yao.

Marko 10:13-14. “Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse lakini wanafunzi Wake wakawakemea. Yesu alipoona yaliyokuwa yakitukia akachukizwa, akawaambia wanafunzi Wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu kama hawa.”

1Wakorintho 1:19-20. “Kwa maana imeandikwa: “Nitaiharibu hekima ya wenye hekima na kuzibatilisha akili za wenye akili.” Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa umpumbavu?”

small snake2

small snake1

ENGLISH: NEVER LOOK DOWN AT A YOUNG SNAKE.

There was a man who had a habit of despising small creatures including small snakes. Therefore, the man, tried to play with the snake’s child because he despised thinking that it could not harm him. His companions told him, “Stop playing with the baby snake, it will bite you.” He refused, saying, “It can’t hurt me because it is still too young.” His companions told him, “never look down at a young snake” When he heard this, he became afraid and left it, because he knew that small  snake was also a snake, like what the old people say that a  baby snake  should not be looked down at.

This proverb focuses on poisonous creatures that should not be despised. The snake can cause problems for those it will bite because of its dangerous venom. However, the person who is bitten by the snake will have problems that can even lead to his death if the poison is not removed.

This proverb is likened with a person who does not raise his children well. He stops warning them even if they have bad attitudes. He abandons his children by making them grow up with their own bad habits resembling the venom of a baby snake, in their lives.

Such bad habits can lead to problems in one’s life, much like the venom of a poisonous snake is. Therefore, it is important for people to give their children a good upbringing at an early age so that they can improve their lives. That is why people say “never look down at a young snake.”

This proverb teaches people to give good education to their children from an early age, so that they can grow up to be good people in their lives. It is also important for people to stop associating themselves with bad people in their lives.

Mark 10: 13-14. 1 Corinthians 1: 19-20.

research-committee-71 (1) from Aimee

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.