Ulusumo lunulo lwingilile kubhakima abho bhagagunanhwa bho gubhukijiwa nigo gobho na nyanda ndololo. Abhakima bhenabho bhagaduma gubhubha nigo gobho gunuyo kunguyo goli ntale. Kiza kayanda kadololo kubhawila, “ulu gomulemelaga ugugubhucha unigo gunuyo, nize nang’wambilije.”
Abhoyi bhagashosha, “godulemelaga nayise abhatale ubhebhe ulindololo chiniko ugugudula ugugucha?” Akayanda kenako kagashosha “nilekelaji nageme.” Aho bhakalekala, kugubhucha unigo gunuyo mpaka kugushisha ukobhaguchalaga. Hunagwene abhakima bhenabho bhagayomba giki, “ng’wana ngosha adibhengagwa.”
Ulusumo lunuyo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhadahahijaga abhanhu kunguno ya mimili yabho guyibhona giki ili midololo. Umunhu ng’wunuyo agayilamulaga imihaho yakwe bho gulola bhutale bho mili go ng’wa munhu. Uweyi adamanile igiki, umunhu adulile gutumama milimo mitale aliyo umili gokwe guli ndololo.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhakima abho bhakagadalaha akayanda ako kagabhambilija ugugubhucha unigo uyo goli gobhalemela abhoyi. Hunagwene aho kabhambilija ugugubhucha, bhagayomba giki, “ng’wana ngosha adibhengagwa.’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka gubhiza nibhengwe ukubhanhu bhanhu bhabho, kugiki bhadule gwiyambilija chiza uguitumama imilimo yao iyagupandikila matwajo ga gujibheja chiza ikaya jabho. Gashinaga igelelilwe abhanhu bhose bhabhize nikujo ukubhichabho.
1 Samweli 17:42-54.
KISWAHILI: MTOTO WA KIUME HADHARAULIWI.
Methali hiyo, ilitokea kwa wanawake waliosaidiwa kazi ya kubeba mzigo wao na mvulani mdogo. Wanawake hao, walishindwa kubeba mzigo wao huo kwa sababu uliokuwa mzito. Akaja mvulana mmoja mwenye umbo dogo akawambia, “kama huo mzigo umewashinda nije niwasaidie kuubeba.” Wao wakamjibu, “ikiwa sisi tulio wakubwa tumeshindwa kuubeba, utauweza kuubeba wewe uliye mdogo?” Yule kijana akajibu, “niachieni nijaribu.” Walipomuachia yule kijana aliubeba ule mzigo mpaka akaufikisha kule walikokuwa wakienda. Ndipo hao wanawake wakasema kwamba, “mtoto wa kiume hadharauliwi.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu mwenye tabia ya kuwadharau watu kwa sababu ya muonekano wa miili yao kuwa ni wadogo. Mtu huyo, huamua maneno yake na mipango yake, kwa kuangalia umbo la nje ambalo mtu analo. Yeye haelewi kwamba, mtu anaweza kufanya kazi kubwa hata kama anaumbile dogo la mwili wake.
Mtu huyo, hufanana na wale wanawake waliomdharau yule kijana mwenye mwili mdogo aliyeweza kuwasaidia katika kuubeka mzigo wao, mpaka akaufikisha kule walikokuwa wakielekea. Ndiyo maana wale wanawake walisema kwamba, “mtoto wa kiume hadharauliwi.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kuwadharau watu wao kwa sababu ya muonekano wao wa nje, ili waweze kusaidiana vizuri katika kuyatekeleza majukumu yao yanayoweza kuwaletea maendeleo ya kuzijenga vizuri familia zao. Kumbe, wanatakiwa kuwa na heshima kwa watu wote wanaoishi nao bila kuwabagua kutokana na maumbile yao.
Daudi na Golithi,
1Samweli 17:42-54. “Mfilisti akamwangalia Daudi kote na kumwona kuwa ni kijana tu, mwekundu na mzuri wa kupendeza, naye akamdharau. Akamwambia Daudi, ‘Je, mimi ni mbwa, hata unanijia na fimbo? ‘ Yule Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. Akamwambia, “Njoo hapa, nami nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni nyama yako.” Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki (fumo) lakini mimi ninakujia kwa jina la BWANA Mwenye Nguvu, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana. Siku hii leo BWANA atakutia mkononi mwangu, nami nitakupiga na kukukata kichwa chako. Leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya jeshi la Wafilisti, nayo dunia yote itajua kuwa yuko Mungu katika Israeli. Wale wote waliokusanyika hapa watajua kuwa BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki, kwa kuwa vita ni vya BWANA, naye atawatia wote mikononi mwetu.”
Yule Mfilisti aliposogea karibu ili kumshambulia, Daudi akaenda mbio kuelekea safu ya vita kukutana naye. Akatia mkono wake mfukoni na kuchukua jiwe, akalirusha kwakombeo nalo likampiga yule Mfilisti kwenye paji la uso. Nalo lile jiwe likaingia chini kipajini mwa uso, akaanguka kifudifudi. Basi Daudi akamshinda huyo Mfilisti kwa kombeo na jiwe, bila kuwa na upanga mikononi mwake akampiga huyo Mfilisti na kumwua. Daudi akakimbia na kusimama juu yake. Akaushika upanga wa huyo Mfilisti na kuuvuta toka kwenye ala yake. Baada ya kumwua, akakata kichwa chake kwa ule upanga. Wafilisti walipoona kuwa shujaa wao amekufa, wakageuka na kukimbia. Ndipo watu wa Israeli na Yuda wakainuka kwenda mbele wakipiga kelele na kufuatia Wafilisti mpaka kwenye ingilio la Gathi kwenye malango ya Ekroni. Maiti zao zilitawanyika kando ya barabara ya Shaaraimu hadi Gathi na Ekroni. Waisraeli waliporudi kutoka kuwafukuza Wafilisti wakateka nyara kambi yao. Daudi akachukua kichwa cha yule Mfilisti na kukileta Yerusalemu, naye akaweka silaha za huyo Mfilisti katika hema lake mwenyewe.”
ENGLISH: DO NOT DESPISE A YOUNG BOY.
This Kisukuma proverb emanates from the story of women who were helped to carry their heavy luggage by a small young boy. These women were unable to carry it because it was too heavy for them to carry. Puzzled, not knowing what to do next, a small young boy came up to them and said, “If this luggage of yours is too heavy for you to carry it, let me help you to carry it.” Looking at him and seeing how small he was, they replied, “If we who are grown up and energetic have failed to carry it, will this small young boy be able to carry it?” The small young man replied, “Let me try.” When they let him try, the young man carried the load until he reached the women’s destination. Surprised at what he had done, the women said, “do not despise a young boy.”
This proverb serves as a lesson to a person who has a tendency to look down on some people because of their physical appearances. Because of this bad habit, such person, evaluates or assigns value to a person based on the outward appearance that such a person has. He does not understand that a person can do great work even if he/she is small in stature.
Such person is like the women who despised the little boy but who was able to help them carry their load, until he got to where they were going. That is why the women said, “Do not despise a young boy.”
This proverb teaches people to stop despising other people because of their outward appearance. Instead; they should support each other in fulfilling their responsibilities for better building of their families. In fact, they should respect other people by living with them without discriminating them.
This proverb is closely related with David and Goliath’s story found in 1 Samuel 17: 42-54.