Olihoyi munhu uyo agalima ngunda ntale na ujibhibha imbiyu chiza. Imbiyu jinijo aho ja jukula agailimila ingeze ya ngunda gunuyo mpaka uyimala. Oho japya ijiliwa jinijo ijamungunda gokwe gunuyo, agazumalika umunhu ng’wunuyo. Unhekela munhu ungi uyo agajihelemba ijiliwa jinijo na gwandya gujilya. Abhanhu aho bhabhona shene, bhuyomba giki, “mibhi ungi nu ng’helembi ungi (mibhi ungi nu nimi ungi).”
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agukoyakoyelaga ginhu jose jose umuwikaji bhokwe. Aliyo lulu ulu ugajipandika isabho ijagufumila umunimo gunuyo, agakijaga ugujitumamila hamo kunguno ya gwinga kuwelelo, nulu gusamijiwa kungi uko adikomile ugujiyegela ijo ujikoyelaga. Iginhu jinijo jigatumamilagwa na bhanhu bhangi abho bhadajikoyelile.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu mibhi o mbiyu uyo agajikoyelaga ijikolo ijo adajitumilaga ulu japya, kunguno nu weyi agabhalekelaga bhanhu bhangi, bhajitumamila abho bhadajikoyelile. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “mibhi ungi nu ng’helembi ungi (mibhi ungi nu nimi ungi).”
Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gwitolea gubhatumamila bhichabho umuwikaji bhobho, kugiki bhadue gupandika matwajo mingi, ayo gadulile gujibheja chiza ikaya jabho. Igelelilwe bhajileke inhungwa jagwiiganika bhoyi duhu, umuwikaji bhobho.
Waefeso 5:32.
Yohana 3:25.
Yahana 4:37-38.
1 Wakorintho 3:6-9.
Luka 10:2.
Wagalatia 6:7-9.
MPANDAJI MWINGINE NA MVUNAJI MWINGINE (MPANDAJI MWINGINE NA MLIMAJI MWINGINE.
Alikuwepo mtu mmoja aliyelima shamba kubwa, akamwaga mbegu vizuri. Zilipoota mbegu hizo aliipalilia palizi mpaka akaimaliza. Yalipoiva mazao yake, mtu huyo alifariki dunia. Akamwachia mtu mwingine ambaye aliyavuna mazao hayo na kuanza kuyatumia. Watu walipoona vivyo, walisema kwamba, “mpandaji mwingine na mvunaji mwingine (mpandaji mwingine na mlimaji mwengine).”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huhangaika kuifanya kazi fulani ambayo matunda yake hushindwa kuyafaidi, maishani mwake. Mtu huyo, hufanya kazi kwa bidii sana mpaka akafikia hatua ya kuanza kuyatumia matunda ya kazi yake hiyo. Lakini kabla ya kuanza kuyatumia matunda hayo, mtu huyo, ama hufariki dunia au huhamishwa na kupelekwa sehemu ambayo hushindwa kuyafaidi matunda ya kazi yake hiyo aliyoihangaikia.
Mtu huyo hufanana na mpandaji wa mbegu katika shamba ambaye alilitunza shamba lake mpaka apata mavuno mengi ambayo aliwaachia wengine wakayafaidi, kwa sababu naye huyu aliwaachiwa wengine wakafaidi matunda ya kazi hiyo, aliyoihangaikia. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mpandaji mwingine na mvunaji mwingine (mpandaji mwingine na mlimaji mwingine).”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujitolea kufanya kazi kwa ajili ya wenzao maishani mwao, ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi yawezayo kuziendeleza vizuri familia zao.
Waefeso 5:32. “Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa.”
Yohana 3:25. “Mashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa.”
Yahana 4:37-38. “Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”
1 Wakorintho 3:6-9. “Mimi nilipanda mbegu, Apolo akatia maji, lakini Mungu ndiye aliyekuza. Hivyo mwenye kupanda mbegu na mwenye kutia maji si kitu, bali Mungu peke Yake ndiye akuzaye. Apandaye mbegu ni sawa na yule atiaye maji. Kila mmoja atalipwa kulingana na kazi yake. Sisi ni watenda kazi pamoja na Mungu, ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.”
Luka 10:2. “Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, awapeleke watenda kazi katika shamba lake.”
Wagalatia 6:7-9. “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.”
ENGLISH: THE PLANTER IS NOT NECESSARILY THE REAPER
There was a man who plowed a great field and sowed good seeds. When the seeds sprouted, he weeded out the weed making his crops clean. Unfortunately, when his crops ripened, the man died. He left his field to someone who harvested the crops and began to use them. When the people saw him they all said, “The planter is not necessarily the reaper.”
This proverb is likened with a man who struggles with a desire to accomplish something in his life. Such a man works very hard until he reaches the point where he begins to use the fruits of his labour. But before one begins to use the fruit, the person either dies or is transferred to a place where he is unable to enjoy the fruits of his labour.
Such a man is like a man who sowed seed in his field, but he did not reap what he had sown. That is why people say, “The planter is not necessarily the reaper.”
This proverb teaches people about volunteering to work for others in their lives, so that they can achieve more success that can make their families live better life
Ephesians 5:32. John 3:25. John 4: 37-38. 1 Corinthians 3: 6-9. Luke 10: 2. Galatians 6: 7-9.