726. OB´IB´ILA MU MHAGALE.
Ulusumo lunulo, lulolile bhub’ib’i bho mbiyu mu mhagale. Imhagale gali manumba ayo gatali ugushila uguzengwa. Olihoyi munhu uyo agab’ib’a mbiyu jakwe umu mhagale jinijo aliganika giki adulile gubisha jiliwa moyi. Aho oduma ugubhona solobho yose yose wibhuja, “nibhuli nagaiwa solobho yose yose umubhutumami bhone?” Abhiye bhung’wila giki, “ob’ib’ila mu mhagale.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agahoyelaga mihayo iyo itina solobho yose yose, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agajimijaga makanza gakwe sagala, kunguno adapandikaga ginhu ijo jidulile gung’wambilija umuwikaji bhokwe. Uweyi agabhalendejaga na bhiye bhaduma uguitumama imilimo yabho, kunguno ya guhoyela mihayo iyo idadulile ugubhambilija jose jose.
Umunhu ung’wunuyo, agikolaga nu uyo ob’ib’ila mbiyu jakwe mu mhagale, kunguno nang’hwe adapandikaga solobho yose yose, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ob’ib’ila mu mhagale.’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guhoyela mihayo ya gubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, kugiki bhadule gupandika solobho ya gubhulang’hana chiza ubhupanga bho bhanhu bhabho, umuwikaji bhobho
Mathayo 13:5-7.
KISWAHILI: ULIPANDIA KWENYE MAPAGALE.
Methali hiyo, huangalia usiaji wa mbegu kwenye mapagale. Mapagale ni majengo yale ambayo hayajaisha kujengwa. Alikuwepo mtu mmoja ambaye alisia mbegu kwenye mapagale akitumainia kupata mazao kutoka humo. Alipokosa kupata faida yoyote, alijiuliza, “kwa nini nimekosa faida yoyote kwenye utendaji wangu wa kazi?” Wenzake walimjibu kwamba, “ulipandia kwenye mapagale.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutumia muda wake katika huongelea maneno yasiyo na faida yoyote kwenye maisha yake. Mtu huyo, huupoteza hovyo muda wake kwa sababu huwa hapati kitu kinachoweza kumsaidia katika maisha yake. Yeye huwachelewesha hata wenzake kufanya kazi zao kwa sababu ya kuendelea kuwaongelesha maneno yasiyoweza kuwasaidia chochote.
Mtu huyo, hulingana na mtu aliyepanda mbegu kwenye mapagale, kwa sababu naye hakuweza kupata faida yoyote, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “ulipandia kwenye mapagale.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao katika kuongelea maneno yawezayo kuwaletea mandeleo kwenye familia zao, ili waweze kupata faida ya kuyalinda na kuyaendeleza vizuri maisha yao.
Mathayo 13:5-7. “Nyingine zikaanguka sehemu yenye mawe, ambapo hapana udongo mwingi. Zikaota haraka kwa sababu udongo ulikuwa hauna kina. Lakini jua lilipozidi, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikuwa na kina. Mbegu nyingine zilianguka katikati ya miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga.”
ENGLISH: YOU PLANTED YOUR SEED IN AN UNFINISHED HOUSE.
There was one man who sowed seeds in the fields, hoping to get some produce from it. When he did not get any benefit, he asked himself, “Why have I missed any benefit in my career?” His colleagues replied, “You planted seeds in an unfinished house.”
This proverb is likened with a man who spends his time by talking nonsense in his life. Such person wastes his time carelessly because he does not find anything that will help him in his life. He delays even his colleagues from doing their work because he continues to speak words that do not help them at all.
The man is like the one who sowed seed in an unfinished house, because he did not have the benefit of it in his life. That’s why people say to him, “you planted you see in an unfinished house.”
This proverb teaches people how to spend their time by talking about words that can bring development to their families, so that they can reap the benefits of protecting and improving their lives.
Matthew 13: 5-7.