718. NG’WANA JITALE.

“Ng’wana Jitale oliotolwa na mbehi umo umu kaya nhale yabhana bhadoo bhingi. Igigela giki, Ung’wana Jitale bhuduma ugwitogwa na nina bhukwi okwe. Unina bhukwi agancholela nzila ya gumpegeja. Bhuli ikanza ulubhalitenga ijiliwa, Ung’wana Jitale winhiwagwa wasa bho heke bho gwigasha bihi na nnengelo ya minzi. Ahikanza lya gulya, abhana bhenabho abhadoo abha ha kaya yiniyo inhale bhankoyaga noyi umamu ng’wunuyo, bhogunomba bhuli ikanza, bhaliyomba, “Ng’wana Jitale minzi, ng’wana jitale minzi.”

Giko uweyi adadulile ugupandika uwasa bho gulya mpaga jushila ijiliwa. Yubhiza giko bhuli lushiku. Ung’wana Jitale agazonga nose ukonda. Ungoshi, o ng’wana Jitale, aho obhona giki ihali yanke iligaluka, agabhiza na bhuyangi umumoyo aliyomba, “Ginehe nke one bhuli ihali yako yilimana yubhiza mbi? Ni bhuli ulikonda? Ehe, udigutaga?” Ung’wana Jitale nang’hwe agashosha, “unene nalinhola.”

Kugiki abhupandike ubhunhana bho nke umo bhuli, agapandika masala, agapundula ipundu ahandugu ya numba kugiki apandike gukengela iginhu ijo jigitiyagwa ahikanza lya gulya. Aho jatengwa ijiliwa, ungoshi, o ng’wana Jitale, agibhanda ahahanze ya ndugu, ukungila na gukengela umugati ya numba bho gubhitila ahipundu. Huna ubadija igiki unke oliotulwa bho makala aha bihi ni nengelo ya minzi, kugiki pye ilikanza amane utung’wa na gukoyiya, bho nduhu upandika ilikanza ilya gulya mpaga jashila ijiliwa.

Ungoshi aho omana chene, agapelana. Huna bhiyangula gusama aha kaya na gwizugila. Ukukaya yabho imhya, uweyi kihamo nu nke bhagayulya chiza. Ihali ya nke igagaluka, ubhelela na gugina.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 83-  84.

Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Umu jigano jise dabhona umu unkoshi o ng’wana Jitale oliantogelilwe unke. Agamonela isungu unke umu likoye lyakwe. Wiyangula gulekana na bhabyaji bhakwe kugiki bhizugile bhinikili.

Hi giko dabhona numo ung’wana Jitale oliodula gwiyumilija umugukoyiwa nu nina bhukwi okwe kunguno ya kuntogwa ungoshi. Agalema gete ugulekana nanghwe. Agabhona ili hambo hambo ugupandikwa ni koye na bhukoyiwa kukila ugubhubhinza uwitoji.

Ijigano jiniji jilidulanga bhutogwa bhushikanu umu witoji. Jilidulanga gutimo abhanhu abhabhili umu witogi bhagadula gwitogwa, idi umubhuyeji duhu, aliyo numu makoye na bhuluhi.

Hangi ijigano jiniji jilidulanga higulya ya bhulumani wise nu Yesu, “Bhuliho bhunhana ubhowibhisile umu mihayo yiniyi, nane alibhona giki yilinola Kristo ni kelesia lyakwe (Waefeso 5:32).

Mulungu B’ab’a agadulumanya ayise bhose abho dabhatijiwa mugati yakwe uYesu Kristo. Yadudakila gwikala mubhutogwa bhokwe bho nduhu ugwilekanya nanghwe nulu mulikanza lya gugeng’wa.

Umu kaya jise abhatoji na bhatolwa bhabhize bhanhu bha gwivumilia na gwitogwa no no ahi kanza ilya makoye guti ga bha Ng’wana Jitale nu ngoshi.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 84-85.

Mwanzo 2:23.

Marko 10:6-9.

Waefeso 5:25, 31-33.

Waroma 8:35-37.

KISWAHILI: BINTI JITALE.

“Binti Jitale aliolewa na bwana mmoja katika jamii kubwa yenye watoto wagodo wengi. Ikatokea Binti Jitale hawakupendana na mama mkwe wake. Mama mkwe akatafuta njia ya kumfukuza. Kila walipoandalia chakula, Binti Jitale  alipewa nafasi maalum ya kukaa karibu na mtungi wa maji. Wakati wa kula, watoto hao wadogo wa jamii hiyo kubwa walimsumbua sana mama huyu, wakimwomba kila mara, wakisema, “Binti Jitale maji, Binti Jitale maji.”

Hivyo yeye hakuweza kupata nafasi ya kula hadi mwisho wa chakula. Ikawa hivyo kila siku. Binti Jitale akawa akisononeka na hatimaye kukonda. Mumewe, Binti Jitale, alipoona hali ya mkewe inazidi kubadilika, akapatwa na wasiwasi moyoni akisema, “Vipi mke wangu, hali yako inazidi kuwa mbaya? Mbona unakonda? Je, hushibi?” Binti Jitale naye akajibu aksisema, “Mimi sijambo.”

Ili kupata ukweli wa hali halisi, akapata maarifa, akatoboa ufa ukuta wa nyumba ili apate kuchunguza mambo yaliyokuwa yakitendeka wakati wa kula. Pindi chakula kilipoandaliwa, mumewe, Binti Jitale, akawa anabana nje ukutani, akivizia na kuchungulia ndani ya nyumba kwa tundu la ufa. Ndipo alipong’amua kwamba mkewe aliwekwa makusudi karibu na mtungi wa maji, ili daima apate kutumwatumwa na kusumbuliwa, bila kupata muda wa kula hadi mwisho wa chakula.

Mumewe alipokwisha fahamu vile, akakasirika. Ndipo walipoamua kuhama nyumbani na kujitegemea. Huko katika maskani yao mapya, yeye pamoja na mkewe walianza kula vizuri. Hali ya mkewe ikabadilika, akanawiri na kunenepa.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 83 – 84.

Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Katika hadithi yetu tunaona jinsi mumewe Binti Jitale alivyompenda mkewe. Akamwonea huruma mkewe katika shida yake. Akaamua kutengana na wazazi wake ili wajitegemee wenyewe.

Kadhalika tunaona jinsi Binti Jitale alivyoweza kuvumilia katika kusumbuliwa na mama mkwe wake kwa sababu ya kumpenda mumewe. Akakataa kabisa kuachana naye. Akaona ni afadhali kupatwa na shida na usumbufu kuliko kuvunja ndoa.

Hadithi hii inatufundisha upendo kamili katika ndoa. Inatufundisha kama watu wawili katika ndoa waliweza kupendana, siyo katika furaha tu, bali katika shida na usumbufu.

Tena hadithi hii inatufundisha juu ya ushusiano wetu na Yesu, “Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake (Waefeso 5:32).”

Mungu Baba alituunganisha sisi sote tuliobatizwa ndani yake Yesu kristo. Yatupasa kukaa katika upendo wake bila kujitenga naye hata wakati wa majaribio.

Katika familia zetu mabwana na mabibi arusi wawe watu wa kuvumiliana na kupendana hasa wakati wa shida kama walivyofanya Binti Jitale na mumewe.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 84-85.

Mwanzo 2:23. “Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.’”

Marko 10:6-9. “Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke. Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’ Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.””

Waefeso 5:25, 31-33. “Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake. Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa. Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.”

Waroma 8:35-37. “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga?  Kama ilivyoandikwa: “Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.” Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda.”

stone woman

kwando family

marriage1

 

ENGLISH: JITALE’S DAUGHTER.

Once upon a time, there was a woman known by the name of Jitale’s daughter. This woman got married to a man whose family had a lot of siblings. Since by that time marriage meant taking a woman straight from her family and making her live with the husband’s family together with the husband’s siblings, Jitale’s daughter also was to join her husband’s family.

The family of her husband did not like Jitale’s daughter. They were struggling to make sure that Jitale’s daughter is chased away by her husband. To do so, everyday during eating time, Jitale’s daughter was forced to sit near the drinking water pot so that she can be serving water to her husband’s siblings. Every time, during meal, children could shout: “Jitale’s daughter water, Jitale’s daughter water.” Jitale’s daughter spent much of the time serving water without eating food as a result she emaciated to the extent of making her husband begin asking her: “How are you my wife, your condition is getting worse? What do you like to eat? Are you not satisfied? ” Jitale’s daughter replied, “I’m fine.”

The husband was not satisfied with his wife’s answer. To seek for more information, one day when they were eating, he stood outside the house unnoticedly and peeped through a wall crack to see what is happening inside the house when eating. He got the truth on why his wife is uncomfortable. The troubles his siblings were causing to his wife made him angry and decided to leave the house with his wife and build a separate home for his new family.

 At their new home, he and his wife began to eat well. His wife’s condition changed, and she became more healthier than before (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering Seeds of the Gospel,’ pages 83 – 84). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.

In our story we see how the husband loves his wife. He felt sorry for his wife in her plight. He decided to separate from his parents to build his home for the seek of his wife.

We also see how Jitale’s daughter was able to endure the suffering of her mother-in-law because of her love for her husband. She refused to give up. She found it much easier to suffer the pain and discomfort than breaking up her marriage.

This story teaches us perfect love in marriage. It teaches us that marriage is accomplished through love and happiness.

Again this story teaches us about our relationship with Jesus: “There is truth hidden in these words, and I perceive that they are in regard to Christ and His church” (Ephesians 5:32).

God the Father has united us all who have been baptized in Jesus Christ’s name. We must abide by His love without forsaking Him even during trials.

In our families, husbands and wives have to be tolerant and loving, especially in times of difficulty like what Jitale’s daughter and her husband did (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ pages 84-85).

Genesis 2:23. Mark 10: 6-9. Ephesians 5:25, 31-33. Romans 8: 35-37.

One comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.