“Olihoyi nkima umo uyo witanagwa Ngolo. Unkima ng’wunuyu oliatogilwe noyi ugubhina imbina. Oliadalekaga uguzwala inhinda umumagulu na gubhucha ng’oma umumakono bhuli kwene uko ojaga. Ukumabhega obhuchaga ifurushi lwakwe lya jiliwe. Mpaga ahikanza lya nzala uweyi agaja gujusuma ukunu alina ng’oma yakwe. Uluwibhona na bhimeji bhakwe bhanombaga bhabhine mbina, bhalimbaga: “Ngolo dubhine kihamo. Ngolo tulaga akafurushi kako! Ngolo dubhine mbina.”
Ungolo agalembwa, uzunya ugubhina mbina, ukunu otulaga akafurushi kakwe hasi. Ahikanza Ungolo unonelwa mbina abhimeji bhakwe bhagang’wibhila ijiliwa.
Aliyo kunguno ya gwibhonelwa na bhimeji bhakwe, bhanwani bhakwe bhagehu abho bhantogilwe, bhaganhugula umo ali nghala, bhaling’wila “Bhaligulebya masala. Bhagugumaja ijiliwa ja bhana. Ulu ulibhina imbina udizukatula hasi akafurushi kako aliyo ubhine nako.”
Imihayo yiniyo agayigwa. Mpaga lushigu lumo, ahikanza alifumila ugujuchola jiliwa, Ungolo agabhitila umuchalo ja bhimeji bhakwe bhumpelela, bhaling’wimbila ilyimbo lyabho:
“Ngolo dubhine kihamo. Ngolo tulaga akafurushi kako! Ngolo dubhine mbina!”
Lushigu lumo Ungolo agazunya ugubhina imbina. Agabhina noyi, aliyo oliakadimilile akafurushi kakwe mumakono. Ukunu alimba:
“Ngolo dubhine mbina, na kafurushi nako mbina, bhimeji bhapankike gubhona.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 90.
Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guzunya gulangwa kugiki bhapandike masala guti numo agazunija Ungolo uguwinja ubhuhala bhokwe kunzila ya gulangwa na bhiye, umuwikaji bhokwe.
“Giko ayise aho dudina pandika ibhatizimu dali guti bhanhu abho bhadina masala, dali dudamanile inzila ya gubhupandikila ubhupanga ubho bhudashilaga. Aliyo ulushigu lunulo ulo bhatizimu, aho datangagijiwa umhayo go ng’wa Sebha, dugazunya guleka kikalile ka kale, akabhuhala wise na gwikala jitakatifu. Kunguzu ja ng’wa Moyo Ntakatifu dugagalucha akajile kise. Duginga mugiti na gwingila muli sana lya ng’wa Sebha.
Uludushoka nyuma hangi, ubhuhala wise bhugubhiza ginehe? Ihali ise ehe, idubhiza mbi kukila aho gwandya?” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 91.
Dudizuzunya ugushoka inuma umuwikaji wise. Digemeje jigemelo ja ng’wa Ngolo uyo adashokile inuma, umukikalile kakwe.
Yona 3:10.
Mathayo 7:24.
Mathayo 12:41.
Waebrania 10:38.
KISWAHILI: NGOLO WEKA MFUKO WAKO. TUCHEZE NGOMA.
“Kulikuwepo na mwanamke mmoja akiitwa Ngolo. Mwanamke huyu alipenda sana kucheza ngoma. Alikokwenda hakuacha kuvaa njuga miguuni na ngoma mikononi. Mabegani akabeba kifurushi chake cha chakula. Hata wakati wa njaa yeye alienda kuhemea huku akiwa na ngoma yake. Alipokutana na watani wake walimwomba awachezee ngoma, wakaimba: “Ngolo tucheze pamoja. Ngolo weka kifurushi chako! Ngolo tucheze ngoma!”
Ngolo alishawishika, akakubali kucheza ngoma, huku ameweka kifurushi chake chini. Wakati Ngolo aliponogewa na ngoma watani wake wakamwibia chakula.
Lakini kutokana na kuonewa na watani zake, baadhi ya rafiki zake wampendao, wakamwonya jinsi alivyokuwa mjinga, wakamwambia, “Wanakuzidi akili. Watakumalizia chakula cha watoto. Uchezapo ngoma usiweke kifurushi chako chini bali ucheze nacho.”
Maneno hayo akayasikia. Hata siku moja, wakati akitoka kutafuta chakula, Ngolo alipita kijijini na watani wake wakamkimbilia, wakimwimbia wimbo wao:
“Ngolo tucheze pamoja, Ngolo weka kifurushi chako. Ngolo tucheze ngoma!”
Siku hiyo Ngolo akakubali kucheza ngoma. Akacheza sana, lakini akiwa amebeba kifurushi chake mgongoni. Huku akiimba:
“Ngolo nicheze ngoma, Na kifurushi nacho ngoma, Watani wapate kuona.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 90.
Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kukubali kufundishwa kusudi wapate akili kama Ngolo alivyokubali kuuondoa ujinga wake kwa kufundisha na wenzake, katika maisha yake.
“Vile vile sisi kabla ya ubatizo tulikuwa kama watu wasio na akili, tulikuwa hatujui jinsi ya kupata uzima wa milele. Lakini siku ile ya ubatizo, baada ya kutangaziwa neno la Bwana, tulikubali kuacha maisha ya zamani, yaani ujinga wetu na kuishi kitakatifu. Kwa nguvu ya Roho Mtakatifu tukageuza mwenendo wetu. Tukatoka gizani na kuingia katika nuru ya Bwana.
Tukirudi nyuma tena, ujinga wetu utakuwaje? Hali yetu je, haitakuwa mbaya zaidi kuliko hapo mwanzo?” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 91.
Tusikubali kurudi nyuma katika maisha yetu. Tuige mfano wa Ngolo ambaye hukurudi nyuma, katika maisha yake.
Yona 3:10. “Mungu alipoona walivyofanya na jinsi walivyogeuka kutoka katika njia zao mbaya, akawa na huruma wala hakuleta maangamizi juu yao kama alivyokuwa ameonya.”
Mathayo 7:24. ‘‘Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.”
Mathayo 12:41. “Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu, kwa maana wao walitubu katika kuhubiri kwa Yona na tazama hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.”
Waebrania 10:38. “Lakini mwenye haki Wangu ataishi kwa imani. Lakini kama akisita-sita sina furaha naye.””
ENGLISH: NGOLO PUT YOUR PARCEL DOWN AND LET US DANCE.
Once upon a time, there was a woman know by the name of Ngolo. This woman was a very good expert in dancing. Everywhere she goes she would not forget carrying with her a banch of ankle bells for her dance. When her village was affected by famine, Ngolo could travel for a long distance in search for food. One day when she met people with whom she has joke relationship, they asked her to dance. The song they sung went like: “Let’s dance together. Take off your luggage and put it down! ” Ngolo responded to her clients by putting down her luggage.
The clients stole Ngolo’s luggage thus making her lose the food she went to search for. Some other good people who were enjoying Ngolo’s dance advised her not to put down her luggage when dancing because people aim more at stealing Ngolo’s food; not really enjoying her dance. Ngolo listerned to this advice. Another day when she was passing with her luggage, clients asked her again to dance for them. As usual, the song went as follows:
“Let’s dance together, put your luggage down.”
Ngolo agreed to dance but, at this time she didn’t put down her luggage. She was singing:
“Let’s dance, and the luggage too dances” (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 90). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.
This proverb teaches people about accepting teaching so that they can gain sense. Ngolo allowed herself to learn in order to shake off her ignorance thus people need to learn from her so that they can have good life in future.
Before baptism we were like mindless people, we did not know how to gain eternal life. But on the day of baptism, after the preaching of the word of the Lord, we were willing to give up our old way of life, our ignorance and live holy. By the power of the Holy Spirit we changed our behaviour. We came out of darkness into the light of the Lord.
If we go back again to darkness, how ignorant will we be? Wouldn’t our situation be worse than before? (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 91).
We must not allow ourselves to go back into our lives. Let’s follow the example of Ngolo who never went back in her life.
Matthew 7:24. Matthew 12:41. Hebrews 10:38.