716. ZENGA NA NG’WANISHI UTIZUZENGA NA NOMOLOMO.

Ijinakikalile, ung’wanishi adi munhu ng’wikorosha; adatogilwe ugunhabhula munhu ose ose mpaga bhidumaga nang’hwe. Aliyo, nulu igiko haho ung’wanishi adiniyangula gunhabhula munhu, agafunyaga bhuhuguji. Ulu ubhebhe udizunilijaga nang’hwe nu ulikomeja gubhiza jidigwa, huna nang’hwe agatimijaga nhana uwiganiki bhokwe ubho gwita ya bhubhi. Adulile gugulabhula.

Aliyo umunhu unomolomo adalendaga. Uweyi ikanza lyose ahayile gugulumula mihayo yabhubhi mingi iyo iliyabhulomolomo kugiki alisanye bhanhu. Umujigemelo: Aho kale, alihoyi mbehu umo agantola ng’wana o Ntemi. Abhanhu abhabhili bhenabho, bhalibhitogilwe noyi. Mpaga ungoshi uganemeja ung’wana o Ntemi uguyela sagala ugubhazenganwa, kugiki adizilanga yabhubhi.

Aliyo iki abhanhu abhalomolomo bhadalendaga; lugigela lushigu lumo Ngikulu umo mbibinja agang’wila: “Ginehe manwani, nibhuli dudagubhonaga uliyelela nulu bhazenganwa?” Nang’hwe ung’wana o Ntemi akashosha, “Ungoshone aganilugalilaga mukaya. Adahayile nafume hanze, angu nagubhipijiwa masala na bhanhu.”

Ungikulu ng’wunuyo unbibinja agang’wila ung’wana o ntemi: “Uligwa manwani, naguguwila inbisira: “Ungoshoko agagulugalilaga mukaya kugiki udizupandika gumana amito gakwe umuchalo. Alina bhanhya bhingi jagukumya. Adahayile ubhamane abhanwani bhakwe abha jikima. Ijinagongeja, naliguhugula nwani one: Bhizaga miso! Uludacholile bhugota bho samba nulu mhigi, ungoshoko agugupeja.” Nang’hwe ung’wana o ntemi agabhuja: “Nagubhufunilija heyi ubhugoga bho samba?”

Ungikulu ugashosha: “Unene nabhudebhile ubhugota bhunubho ubho samba. Nagugubhegeja. Iginhu ujo udakilwe ujite ili gunicholela jisanjo ijojigitanagwa ‘jingila’ ja gubhukalihya ubhugota bhutumame nimo chiza.” Ung’wana o ntemi agabhuja: “Ulihaya jisanjo ki ja bhugota?”

Ungikulu agashosha: “Ibhujiku, ahikanza umona ungoshoko olala, uumoge inzwili ijaha mhanda. Unenhele inzwili jinijo, nu nene nagugubhegeja ubhugota.”

Imhindi aho bhatali ugulala, ung’wana o ntemi agabhisa lugembe lukali ahasi ya myenda ya gwikumba. Omalaga gwibhegeleja gumhoga ungoshi ibhujiku.

Ungikulu ng’wunuyo unbibinja, agandya gunchola ungoshi o ng’wana o ntemi mpaga umpandika. Ung’wila: “Ng’wanone; ni bhuli mugwikenyaga nu nkima oko? Ginehe, digwile giki imazuli unkima oko alichola lushu angu alihaya gugubhulaga?” Nang’hwe unsumba ungoshi o ng’wana o ntemi ng’unuyo agashosha, “Nhana!” Ungikulu agayomba: “Ehe, ginhu jibhi noyi ahagati yako nu nke oko. Iyangalilage, ilelo yiniyi ibhujiku igugupandika mitale. Ikalaga Nzugulu matu!”

Ungoshi ng’wunuyo agazunya yose iyo owilagwa. Aho lyashiga ilikanza lya gulala, unshosha agalina habhulili wangu ugikumba ng’wenda, wiyitya gung’oola guti giki ali mutulo ndito. Aho ung’wana o ntemi ogema ugumisha ungoshi, unbehi wiyitya gulewa tulo.

Ahenaho ung’wana o ntemi umana giki, ungoshi odimagwa na tulo ndito. Huna ung’wana o ntemi usola lugembe bho mbisira alihaya gumoga ungoshi inzwili ja ha mhanda. Ahenaho unbehi uyo oliwigemya gulala tulo, umisha wangulija alimana giki ihaha jatimila iginhu, ohaya gusinzwa nu nke abhulagwe.

Haho na haho, unbehi nang’hwe, ulufunya ulushu lokwe ulukali; alilanghana. Aganchima unke ahajikubha! Ung’wana o ntemi ulila: “Ginehe ng’witugwi one ulinibhulaga?” Unbehi agashosha: “Nibhuli ubhebhe ulihaya gunibhulaga?”

Lidakulile ikanza, ung’wana o ntemi utinha ng’holo, ucha. Untemi aho ojipandika imhola ja lufu lo ng’wana okwe, agafunya amri pye abhadugu bha nkwilima bhabhulagwe. Ungikulu unomolomo ubhiza obhulaga ndugu ngima. Ninga iki bhalihoyi bhanishi bhingi umuchalo, bhudigelile bhubhi bho chiniko. Ubhubhi bhunubho bhugenhelejiwa na bhulomolomo, idi bhanishi. Lolaga Kugundua mbegu za Injili, bhukurasa 55.

Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Ushetani ali nomolomo na hangi ili kajile kakwe uguyomba bhulomolomo. Agandya nimo gokwe go gusambula bhulumani agati ya Mulungu na bhanhu bho nzila ya bhulomolomo. Kunzila yiniyo duhu agadula gubhalemba abhabyaji bhise abha gwandya Adamu nu Eva, giki ulu bhita guti umo uliobhawilila nibhabhiza guti Mulungu. Amafumilo ga jito jinijo gali bhulekani ahagati ya Mulungu na mhunhu.

Ku lufu na bhuhimbuki bho ng’wa Sebha wise UYesu Kristo, uMulungu B’ab’a agadulumanya nang’hwe hangi. Unimo gokwe ushetani nu bhulingisilo bhokwe ili gwenha widumi.

Mpaga lelo agitaga nimo gunuyu ugo gudujimija bho nzila ya bhulomolomo. Kuyiniyo dudizujimija mholele mukaya jise bho guyomba bhulomolomo, nulu guzunya mihayo iyo duliwilwa bho nduhu ugukengela ulu ili ya nhana nulu ya bhulomolomo.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 56.

Mwanzo 3:5.

Yohane 8:44.

Yakobo 3:5-6.

Yakobo 1:26.

KISWAHILI: HERI JIRANI ADUI KULIKO MWONGO.

Kwa kawaida, adui ni mtu asiye mkorofi; hapendi kumdhuru mtu yeyote hadi amekosana naye. Lakini, hata hivyo kabla adui hajachukua hatua ya kumdhuru mtu, hutoa ovyo au tahadhari. Iwapo wewe hutaafikiana naye na kuendelea kuwa kichwa maji, basi naye hutekeleza kweli nia yake kwa vitendo vibaya. Anaweza akakudhuru.

Lakini mtu mwongo hatulii. Yeye daima hutaka kuzua mambo mengi mabaya na ya uwongo ili kuchonganisha watu. Kwa mfano: Hapo zamani, palikuwapo na bwana mmoja akaoa binti mfalme. Watu hawa wawili, wakapendana sana. Hata bwana akamkataza binti mfalme kutembea ovyo kwa jirani, ili asijifunze mabaya.

Lakini kwa vile watu waongo hawatulii; kukatokea siku moja bi Kizee mmoja mwenye kilimilimi akamwambia: “Vipi shoga, mbona hatukuoni ukitembelea hata jirani?” Naye binti mfalme akajibu, “Mume wangu ananifungia ndani. Hataki nitoke nje, eti nitapotoshwa na watu.”

Bi Kizee huyo mwenye kilimilimi akamwambia binti mfalme: “Unasikia shoga, nitakuambia siri: “Mumeo hukufungia ndani ili usipate kujua visa vyake vya mitaani. Ana hawara wengi ajabu. Hataki uwajue hao rafiki zake wa kike. Zaidi ya hayo, nakutahadharisha shoga yangu: Uwe macho! Usipotafuta dawa ya mapenzi au hirizi, mume wako atakufukuza.” Naye binti mfalme akauliza: “Nitatoa wapi dawa ya mapenzi?”

Bi Kizee akajibu: “Mimi najua dawa hiyo ya mapenzi. Nitakufanyia. Jambo unalotakiwa kufanya ni kunitafutia kiungo maalum cha kuchochea hiyo dawa ifanye kazi vizuri “shingila”. Binti mfalme akauliza: “Unataka kiungo gani cha dawa?”

Bi Kizee kajibu: “Usiku, wakati ukimwona mumeo amelala, mnyoe nyele kidogo za utosini. Niletee hizo nywele, na mimi nitakutengenezea dawa.” Jioni kabla ya kulala, binti mfalme akaficha wembe mkali chini ya nguo za kujifunika. Tayari amejiandaa kumnyoa mumewe usiku.

Bi Kizee huyo mwenye kilimilimi, akaanza kumtafuta mume wa binti mfalme hadi akampata. Akamwambia: “Mwanangu; mbona mnagombana na mkeo? Vipi, tumesikia hivi majuzi kwamba mkeo anatafuta kisu eti ataka kukuua?” Naye kijana mume na yule binti mfalme akajibu, “Kweli!” Bi Kizee akasema: “Ndiyo, mambo mabaya sana kati yako na mkeo. Tahadhari, leo hii usiku yatakupata  makubwa. Kaa Chonjo!”

Yule mume akaamini yote aliyoambiwa. Hata ilipofika saa ya kulala, mwanaume akapanda kitandani mapema kajifunika nguo, kajisingizia kukoroma kama kwamba yu usingizini mzito. Pindi binti mfalme alipojaribu kumwamsha mumewe, bwana akajisingizia kuzidiwa usingizi.

Hapo binti mfalme akajua kwamba, mumewe kashikwa na usingizi mzito. Ndipo binti mfalme akachukua wembe kwa siri kutaka kumnyoa mumewe nywele za utosini. Hapo yule bwana ambaye alikuwa amejisingizia kulala usingizi, akaamka ghafla akijua kwamba sasa mambo yalikuwa tayari, ataka kuchinjwa na mkewe auawe.

Papo hapo bwana naye, akachomoa kisu chake kikali; akijikinga. Akamchoma mkewe kifuani! Binti mfalme akalia: “Vipi mpenzi wangu unaniua?” Bwana akajibu: “Mbona wewe ulitaka kuniua?”

Haujapita muda, binti mfalme akakata roho, akafa. Mfalme alipopata habari za kifo cha binti yake, alitoa amri jamii yote ya mtoto wa mkwewe wauawe. Bi Kizee mwongo akawa ameua jamii nzima. Ingawa kulikuwepo na maadui wengi kijijini, hapakutokea kuwepo na balaa kama hii. Balaa hii ilisababushwa na uwongo, siyo uadui. Rejea Kugundua mbegu za Injili, ukurasa 55.

Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Shetani ni mwongo na tena ni kawaida yake kusema uwongo. Alianza zamani kazi yake ya kubomoa uhusiano kati ya Mungu na watu kwa njia ya uwongo. Kwa njia hiyo hiyo tu aliweza kuwadanganya wazazi wetu wa kwanza Adamu na Eva, kwamba wangefanya kama alivyosema wangekuwa kama Mungu. Matokeo ya jambo hilo yalikuwa utengano kati ya Mungu na Binadamu.

Kwa kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Mungu Baba alitupatanisha naye tena. Kazi yake Shetani na lengo lake tu ni kuleta mafarakano.

Hadi leo anafanya kazi hii ya kutupoteza kwa njia ya uwongo. Kwa hiyo tusipoteze amani katika familia zetu kwa kusema uwongo, au kukubali maneno tunayoambiwa bila kuchunguza kama ni kweli ama sivyo.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 56.

Mwanzo 3:5. “Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

Yohane 8:44. “Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.”

Yakobo 3:5-6. “Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu katika ya viungo vya mwili wetu. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanam.”

Yakobo 1:26. “Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, bali hujidanganya moyoni mwake, dini yake mtu huyo haifai kitu.”

zenga beach

senga rwanda

ENGLISH: IT IS BETTER TO BE CLOSER TO AN ENEMY THAN A LIAR.

Normally an enemy is not a violent person. In case of any disagreement, he/she will not directly harm his/her enemy without any warning in advance. If the warning is being given and no one responds to it, that person can decide to harm the one who has caused that disagreement. It is quiet different from a liar. A liar will always keep on inventing his/her lies to antagonize people. For example, once upon time, there was a man who married a princess. This couple was always full of love and care. This strong love and care made the husband restrict his wife from leaving the house to visit their neighbours; the princess was to be indoor all the time while the man could go out with no restricitions. But since liars are not silent; One day, a certain old woman bumped into the princess and told her, “Oh, gosh, why don’t we see you visiting your neighbours?”

The princess answered, “My husband locks me inside. He doesn’t want me to leave the house for fear of being misled by people. ” The old woman said, “listern to me my darling, I’ll tell you the secret behind this restriction:“ Your husband locks you in in order to deny you information about his mistresses. He has so many wonderful mistresses. He doesn’t want you to know his girlfriends. I also warn you my darling: Be careful! If you do not look for love portion or charms, your husband will drive you away. ” Then the princess asked: “Where shall I get this love portin or charm?” The old woman replied: “I know where to get it. I will do it for you.

All you have to do is find a specific ingredient that will help to stimulate the charm and work on him properly. The princess asked: “Which ingredient do you want for medicine?” The old woman replied: “At night, when you see your husband asleep, shave off little hair from his head. Bring that hair to me, and I’ll make you some medicine.” The evening before going to bed, the princess hid a sharp razor under the beding . She was ready to shave her husband at night.

The same day, this old woman looked for the princess’ husband and had the following to tell him: “My son, why do you quarrel with your wife? I have heard that your wife is looking for a knife to kill you at night.” The man replied: true! Then the old woman said: “Yes, these are very bad things between you and your wife. Tonight, I caution you, stay tuned. Your wife is likely to harm you.”

The man believed everything he was told. At bedtime, the man went to bed very early before his wife. He was in his clothes; without undressing them and he pretended to be in deep sleep when his wife came around. When the king’s daughter tried to wake him up, the man pretended to be drowsy.

Then the princess knew that her husband was in a deep sleep. Then she carefully took a razor to shave her husband’s hair. At that moment the man, who pretended to be asleep, woke up suddenly, knowing that things were now ready, that he would be killed by his wife. He pulled his knife, as a means to defend himself, and stabbed the princess on her chest to death. The princess shouted, before death:”How is it that my dear one is killing me?” The man replied: “Why did you want to kill me?”

When the king (the father of the princess) learned of his daughter’s death, he ordered execution of his son-in-law’s entire family. The lies of the old woman have killed the whole community where the princess’ husband comes from. Although there were many enemies in the village, there was no such a plague. This malady was caused by lies, not hostility (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 55). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Patriarch Donald Sybertz, M.M., and Patriarch Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.

Satan is a liar and it is common for him to lie. He began his work of destroying the relationship between God and men in a false way. In the same way he was able to deceive our first parents Adam and Eve, that if they do as he told them they would be like God. The result was man’s separation from God..

Through the death and resurrection of our Lord Jesus Christ, God the Father reconciled us to Him again. His mission and purpose is not to cause division.

Today, Satan does this work of perverting us from being closer to God. So we should not lose our families’ peace by lying, or accepting the words we are told without confirming whether they are true or not (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 56).

Genesis 3: 5. John 8:44. James 3: 5-6. James 1:26.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.