“Imbulu yili jisumva ijo jilinajimile jimanyikile. Ulu yupandika ikoye igapelelaga hiwe wangu bho nduhu ugushoka inuma. Igahayiyagwa giki, ili jidamu noyi ugwiyinja imbulu uludamila hitale. Nulu ugituta bho nguvu nulu ugidima unkila goyo mpaga gugutinika, ilemile duhu ugwinga.
Ulusumo lunulu lugatumikaga nono ku bhanhu abho bhali na jimile jilebhe umuwikaji, guti mkima uyo alilema gulekana nu ngoshi okwe, nulu agapandika makoye ga mbika ki.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 74.
Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
“Uwikaji wise ubho jikristo bhudulile gulenganijiwa na lusumo lunulu. Imbulu uluyapandika ikoye igapelelaga hitale bho wangulija. Nulu igadutwa nulu gutinwa nkila, idadulile ugulilekela ilitale linilo. Igendeleyaga kulidimila duhu bho nguzu.
Nulu ayise bhakristo ulu dupandikwa na maluho nulu gugeng’wa go mbiga ki, dumpelele Yesu. Dudizuzunya ugulekanyiwa nang’hwe, uyo alijiganga jise na bhupelelo wise.
Ulusumo lunulu giko lulibhalola na bhanhu abha witoji bho Jiafrika ubho kale ubho bholi bhudamu ugubhinzika. Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 75.
Marko 10:8-9.
Yohane 15:9-10.
Waefeso 5:31-32.
Wafilipi 3:7-8.
KISWAHILI: KENGE AMENG’ATA JIWE.
“Kenge ni kiumbe mwenye msimamo halisi. Apipata hatari hukimbilia jiwe kwa haraka bila kurudi nyuma. Inasemekana kwamba, ni vigumu sana kumbandua kenge aking’ang’ania jiwe. Hata ikiwa unamvuta kwa nguvu au kumkamata mkia wake mpaka kukatika, anakataa tu kuondoka.
Methali hii hutumika hasa kwa watu wenye msimamo fulani maishani mwao k.m. bibi anayekataa kuachana na mume wake, hata akipatwa na shida ya namna gani.” Rejea Kugundua Mbegu ya Injili, ukurasa 74.
Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
“Maisha yetu ya ukristo yanaweza kulinganishwa na methali hii. Kenge akipata hatari hukimbilia jiwe kwa haraka. Hata kama akivutwa au kukatwa mkia, hawezi kuliacha lile jiwe. Anaendelea tu kulishika kwa nguvu.
Hata sisi Wakristo tukipatwa na mateso au majaribio ya namna gani, tumkimbilie Yesu. Tusikubali kutenganishwa naye, ambaye ndiye mwamba wetu na kimbilio letu.
Methali hii vile vile inawahusu watu wa ndoa za Kiafrika za zamani zilizokuwa ngumu kuvunjika.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 75.
Marko 10:8-9. “Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.””
Yohane 15:9-10. “Kama vile Baba alivyonipenda Mimi, hivyo ndivyo Mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo Langu. Mkizishika amri Zangu mtakaa katika pendo Langu, kama Mimi nilivyozishika amri za Baba Yangu na kukaa katika pendo Lake.”
Waefeso 5:31-32. ““Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe na hawa wawili watakuwa mwili mmoja.” Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa.”
Wafilipi 3:7-8. “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, sasa nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitayo kiasi ya kumjua Kristo Yesu Bwana wangu, ambaye kwa ajili Yake nimepata hasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo.”
ENGLISH: THE MONITOR LIZARD HAS STUCK ON A ROCK.
This proverb comes from a monitor lizard that, when it is in dangerous situation, it sticks on a rock. It is said that, when the monitor lizard sticks on a rock, it becomes very hard to remove it there. Even if one can try pulling its tail to the extent of breaking it, it won’t leave the rock.
This proverb can be compared to people who hold some positions in life. For example, this saying can be likened to a wife who refuses to divorce her husband and vice versa(Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 74). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.
Our Christian life can be compared to this saying. Like the monitor lizard, whatever trials Christians face they should run to Jesus. Let us not accept separation from Him, who is our rock and our refuge.
This proverb also can be compared to African old marriages which were difficult to separate (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 75).
Mark 10: 8-9. John 15: 9-10. Ephesians 5: 31-32. Philippians 3: 7-8.