714. YA NG’WA MACHIMANI IKAZUNYIWAGWA NUMA.

Aho kale olihoi nhingi o ndimu uyo oli nkumuku, witanagwa Machimani. Oli Buduhe umu nkoa go Shinyanga. Uweyi na bhalingi bhiye bhali bhamanila guja meatu umu nkoa go Simiyu mhangala ningi gujulinga ndimu ja mbika ningi.

UMachimani bhuli kwene uko ojaga gujulala oli azwalile jilatu, iki oli na mashaka, hamo bhagwiza bha masai, “Ulu nukungula ijilatu nagugaiwa ugogwita,” aliyo abhiye bhakungulaga ijilatu ahikanza ilya gulala guti gawaida.

Lushigu lumo agabhahugula abhiye, “bhabehi dubhize miso! Ilelo ibhujiku, dugwitujiwa na bhanishi bhise. Uluduligalala dudizukungula ijilatu umumagulu.” Abhiye kihamo bhaganemeja umhayo gokwe bhaling’wima Umachimani, “bhobha bhoko sebha bho bhule duhu, dulale na jilatu hangi? Ijilatu jako jiliduminya amagulu. Ubhehe uli nghala o mbika ki? Umanile kiyi Machimani?” Bhagandaraha noyi.

Aho wingila ubhujiku ubho ahati, bhahaimanila! Bhisanga bhitujiyagwa na bhanishi. Wigela wiyoja, bhandya gupela sagala. UMachimani uyo oliazwalile jilatu umumagulu gakwe agapela bho nduhu makoye, ubhaleka numa abhiye bhose, bhagapela bho nduhu jilatu, bhuching’wa shokolo na mifa. Bhuduma ugubhaleka abhanishi. Abhingi bhagading’wa bhusunduhala bhaliyomba, “bhuli bhuhubhi wise, ulu nidigwa ubhuhuguji bho ng’wa Machimani iyi yose nidadupandikile.”  “Gashinaga! ‘Ya ng’wa Machimani ikazunyiyagwa numa.”” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 76-77.

Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Umu jigano jiniji UMachimani oyombaga mihayo ya ng’hana gete aliyo abhiye bhadanzunilijije. Bhaganhalalika bhaliyomba, “Machimani bhebhe, umanile ki?”

Mpaga lelo UYesu Kristo aguyomgaga na yise. Atali agutangajaga Injili yakwe. Agayombaga mihayo ya ng’hana iyo igafumaga kuli Mulungu, mihayo iyo igenhaga bhupanga na bhupiji.

Aliyo ayise bhanhu dudadililaga. Dadumaga ugugwigwa umhayo gokwe ugogwikalana. Bhuli bhuhubhi wise. UYesu Kristo aho olihasi henaha okunywaga kunguno ya kuleka gunzunya go bhanhu (lolaga Marko 6:6, Luka 11:31-32).

Nulu ilelo UYesu Kristo atali agukumyaga kunguno ya gukija guzunya gwise. Imihayo ya ng’wa Machinani igazunyiyagwa numa. Aliyo idi mihayo ya ng’wa machimani duhu, aliyo yili mihayo ya ng’wa Yesu Kristo ng’winikili iyo igazunyiyagwa numa.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 77.

Marko 6:5-6.

Luka 11:31-32.

Luka 24:25.

Waroma 10:16, 21.

KISWAHILI: MANENO YA MACHIMANI HUSADIKIKA BAADAYE.

Hapo kale alikuwapo mwindaji maarufu, akiitwa Machimani. Alikuwa anaishi Buduhe katika Mkoa wa Shinyanga. Yeye na wawindaji wenzake walikuwa wamezoea kwenda Meatu katika Mkoa wa Simiyu mara nyingi ili kuwinda wanyama mbalimbali.

Machimani kila alipokwenda kulala alikuwa anavaa viatu, maana alikwa na shaka, labda Masai atakuja, “Nikivua viatu nitakosa la kufanya,” lakini wenzake walikuwa wanavua viatu wakati wa kulala kama kawaida.

Siku moja akawaonya wenzake, “Jamani tuwe macho! Leo usiku, tutashambuliwa na adui zetu. Tuendapo kulala tusivue viatu miguuni.” Wenzake kwa jumla walipinga waliloambiwa na Machimani wakisema, “Woga wako Bwana ni bure tu, tulale na viatu tena? Viatu vyako vinatuumiza miguu. Wewe ni mjinga wa namna gani? Unajua nini Machimani?” Walimdharau sana.

Hata ilipofika usiku wa manane, ghafula! Wakajikuta wanashambuliwa na maadui. Kukatokea ghasia, wakaanza kukimbia ovyo. Machimani ambaye alikuwa na viatu miguuni mwake akakimbia bila shida, akawaacha nyuma wenzake wote, wakakimbia bila viatu, wakachomwa mbigili na miiba. Wakashindwa kuwaacha maadui. Wengi wakashikwa wakasikitika wakisema, “Ni kosa letu, tungesikia onyo la Machimani haya yote hayangelitupata.” “Kumbe! ‘Ya ng’wa Machimani ikazunyiwagwa numa,’ yaani, “maneno ya Machimani husadikika baadaye.”” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 76-77.

Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Katika hadithi hii Machimani alikuwa akisema maneno ya kweli lakini wenzake hawakusadiki. Wakambishia wakisema, “Machimani we, unajua nini?”

Hadi lelo Yesu Kristo anasema nasi. Bado anatangaza injili yake. Husema maneno ya kweli yanayotoka kwa Mungu, maneno yanayoleta uzima na wokovu. Lakini sisi watu hatujali. Tumeshindwa kulikia neno lake la kuliishi. Ni kosa letu: Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa akishangaa kwa sababu ya kutokuamini kwa watu (tazama Marko 6:6, Luka 11:31-32).

Hata leo Yesu Kristo bado anashangaa kwa sababu ya kutokuamini kwetu. Maneno ya Machimani husadikika baadaye. Lakini siyo maneno ya Machimani tu, bali ni maneno yake Yesu Kristo mwenyewe husadikika baadaye.”  Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 77.

Marko 6:5-6. “Hakufanya miujiza yo yote huko isipokuwa kuweka mikono Yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. Naye akashangazwa sana kwa jinsi wasivyokuwa na imani.”

Luka 11:31-32. “Siku ya hukumu, Malkia wa Kusini atainuka pamoja na watu wa kizazi hiki akiwahukumu kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Solomoni. Lakini sasa, Yeye aliye mkuu kuliko Solomoni yuko hapa. Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu kwa sababu wao walitubu walipomsikia Yona akihubiri. Lakini sasa, Yeye aliye mkuu kuliko Yona yuko hapa.”

Luka 24:25. “Yesu akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii!”

Waroma 10:16, 21. “Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, ‘‘Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?’’ Lakini kuhusu Israeli anasema, “Mchana kutwa nimewanyoshea watu wakaidi na wasiotii mikono Yangu.’’

hunters hadzabe

hunters bushman

ENGLISH: THE WORDS OF MACHIMANI CAME TO BE UNDERSTOOD LATER.

Once upon a time, there was a famous hunter known by the name of Machimani. This hunter lived in Buduhe village, Shinyanga region. Machimani and his fellow hunters used to go to Meatu, in Simiyu region, for hunting different animals. Every time he goes to sleep, Machimani could sleep with his shoes on, but his fellows could took off their shoes as usual. Machiman could not take off his shoes because the Maasai men, considered their enemies, may come and attack them at night.

 One day Machimani warned his fellows saying: “Be careful! Tonight, we will be attacked by our enemies. When we go to bed with shoes it will be easy to run when attacked.” His colleagues rejected his proposition saying: to sleep with shoes again? By the way, your shoes hurt our feet at night. How stupid are you? What do you know about fighting? ” They despised him greatly. All over a sudden, at night the Maasai warriers attacked them and Machimani made his way and escaped.

Other hunters could not run well because they had no shoes thus suffered from thorn piercing in their feet. They were finally captured by the Maasai warriors. To remember what Machimani said to them, they said: “It is our fault, we would have heard all these warnings from Machimani.” The words of Machimani are remembered later but it is too late (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 76-77).

This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.

In this story Machimani was saying the words of truth but his colleagues did not believe it. They said, “Well, what do you know?”

Today, Jesus Christ speaks to us. He is still proclaiming His gospel. He speaks the words of truth that come from God, words that bring life and salvation. But we people don’t care. We have failed to hear His living word. It is our fault: When Jesus Christ was here on earth He was perplexed by the loss of belief of the people (See Mark 6: 6; Luke 11: 31-32).

Even today Jesus Christ is still astonished because of our loss of belief. The words of Machimani prove to be true later when we fall into a trap. It is not just the words of Machimani, but the words of Jesus Christ Himself that will be confirmed later when is too late for us to change our ways (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 77).

Mark 6: 5-6. Luke 11: 31-32. Luke 24:25. Romans 10:16, 21.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.