“Idi ginhu ja gukamaja ugumona munhu nhebhe alifunya sabho ja guntoja ng’wana okwe. Jili ginhu ja kawaida duhu. Aliyo jili ginhu ja gukumya gumona umunhu alinfunija sabho ng’wana ong’wa ungi ja gutolela. Ugwita yawiza nulu ugungunana munhu uyo adio ludugu loko, igabhizaga guti gumiliwe; giki ili jidimu gete na bhanhu abha bhalita giki bhali bhagehu duhu.
Ulusumo lunulo lulidulanga giki ili jilidimu ugwifunya kulya bhabhu abho bhadi bhandugu. “Mininga gali madito kukila minzi.”” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, bhukurasa 63.
Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
“Ulu nkristo aliifunya kulwa munhu uyo adio ndugu, ubhutogwa bho ng’wa Mulungu bhushikanile gete umugati yakwe nu ung’wunuyo hunkristo unshikanu.
Ikaya jise ija jikristo jidizubhiza kaya ijo jigacholaga solobho jajo duhu. Aliyo jibhize kaya ijo jigifunyaga gubhambilija abhangi abho bhadi bhandugu umu shida ja bhuli mbika.
Ugwifunya kulwa bhanhu bhose, nono abho bhadibhadugu bhise ili jidimu nghana. Ili kuti gumiliwe. Ugwikala jikristo guli nimo, na idi ligusha.
Umu kaya nu muwikaji bho jikristo ugwifunya jili ginhu ja kawaida, guti mayu uyoalifunya kulwa bhana, bhabyaji abho bhalifunya bho gubhalipila ada ja shule abhana. Giko na bhakristo, kaya na Jumuiya ndoo jidakililwe gwifunya noyi.” Lolaga Kugundua mbegu ja Injili, ukurasa 64.
Mambo ya Walawi 19:34.
Isaya 58:10.
Mathayo 5:46.
Mathayo 10:8.
KISWAHILI: KUMWOZA MTOTO WA MWENZAKO NI KUMEZA JIWE.
“Si jambo la kushangaza kumwona mtu fulani akitoa mahari kumwoza mwanaye. Ni jambo la kawaida tu. Lakini ni jambo la kustaajabisha kumwona mtu anayemtolea mahari mtoto wa mwingine. Kufanya wema au ufadhili kwa mtu asiye wa ukoo wako, huwa kama kumeza jiwe; yaani ni vigumu kweli na watu wanaofanya hivi ni wachache tu.
Methali hii inatufundisha kwamba ni vigumu kujitoa kwa ajili ya watu wasio ndugu. “Damu ni nzito kuliko maji.”” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 63.
Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
“Ikiwa mkristo anajitolea kwa ajili ya mtu asiye ndugu, upendo wa Mungu umekalimika kweli ndani yake na yeye ndiye mkristo kamili.
Familia zetu za kikristo zisiwe familia ambazo zinatafuta faida zao tu. Bali ziwe familia zinazojitolea kwa kuwasaidia wengine wasio ndugu katika shida mbalimbali.
Kujitolea kwa ajili ya watu wote, hasa wale wasio ndugu kwetu ni vigumu kweli. Ni kama kumeza jiwe. Kuishi kikristo ni kazi, na siyo mchezo.
Katika familia na maisha ya kikristo kujitoa ni kitu cha kawaida, k.m. mama anayejitoa kwa ajili ya watoto, wazazi ambao wanajitoa kwa kulipa ada za shule za watoto. Pia wakristo, familia na Jumuiya Ndogo Ndogo zinaitwa kujitoa zaidi.” Rejea Kugundua mbegu za Injili, ukurasa 64.
Mambo ya Walawi 19:34. “Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi BWANA Mungu wako.”
Isaya 58:10. “nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu na kutosheleza mahitaji ya walioonewa, ndipo nuru yenu itakapong’aa gizani, nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.”
Mathayo 5:46. “Kama mkiwapenda wale wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?”
Mathayo 10:8. “Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure.”
ENGLISH: PAYING DOWRY FOR YOUR FELLOW’S SON IS LIKE SWALLOWING A STONE.
It is not strange to see someone paying dowry for his son, but it is not easy to see someone paying dowry for someone’s son. Sacrificing your wealth for someone else is hard. It is like swallowing a stone.
This proverb teaches us that it is difficult to make sacrifice for for people who are not your relative. “Blood is thicker than water” (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 63). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.
If a Christian offers himself for a non-brother, then the love of God is firmly rooted in him and he is a complete Christian.
Our Christian families should not be families that are only seeking their own advantage. Rather, be families dedicated to helping others who are not brothers in various situations.
Volunteering for all people, especially those who are not our relatives, is really hard. It’s like swallowing a stone, but we need to abide by God’s commandments that we have to love and help each other in solving problems.
In Christian life, giving is a common practice, for example, helping widows, paying school fees, etc. Christians, families, and small christian communities are called upon to make a greater commitment on helping the needy people (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 64).
Leviticus 19:34. Isaiah 58:10. Matthew 5:46. Matthew 10: 8.