711. MASABHO MABHONWA BHUPANGA BHULAMBU.

“Ulusumo lunulu lugatumikaga ahikanza munhu ojimijaga sabho jakwe ijo ojipandikila kuluyilo. Jigemelo: Gwibhilwa ng’ombe. Agazunyaga gujimija sabho kukila bhupanga bhokwe aliyomba: “Masabho mabhonwa bhupanga bhulambu.” Isabho jili ndogu. Ubhupanga bhuli na solobho kukila sabho. Umunhu uyo ocha adadulile guchola sabho hangi.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, bhukurasa 61.

Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agadililaga bhupanga kukila sabho, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhalangaga na bhiye inzila jagubhulonja ubhupanga bho bhanhu bhabho, kukila umobhagajilongejaga isabho jabho. Hunagwene umunhu ng’wunuyo, agabhawilaga abhanhu giki, “masabho mabhonwa bhupanga bhulambu.”

 “Umuwikaji wise ubhupanga bho mili bhuli ginhu ja solobho ubhodubhutogilwe na dugabhulang’hanaga kuliko maginhu gose. Hangi dugatumilaga bhuli nzila bhudizujimila nulu bhudizukenaguka.

UYesu Kristo agiza ahasi adinhe bhupanga, idibhupanga bho mili, aliyo bhupanga bho ng’wa Mulungu ng’winikili. (Lolaga Yohane 10:10). UBhupanga bhunubhu bhugigelaga bho gunzunya Yesu Kristo uyo otung’wa na Mulungu B’ab’a (lolaga Yohane 3:16). Yilihoyi solobho ki uguyipandika pye uyamusi na gubhugaiwa ubhupanga ubho bhugigelaga bhule bho guzunya? Nulu yili na solobho ki ugwikomanya nu Mulungu?

Ulusumo lunulu lodulanga gubhudilila ubhupanga ubho bhulunga kele ubhobhudashilaga kukila gugadilila maginhu gamusi ayo gadalamaga (Lolaga 2Kor. 4:18). Hangi lodulanga gubhulang’hana ubhupanga wise ubho mili, na guiliga yose iyoidulile gubhubhipya ubhupanga bhunubho.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, 62.

Mathayo 19:16.

Marko 8:36.

Yohane 3:16.

Yohane 6:27.

Yohane 10:10.

KISWAHILI: BORA UHAI KULIKO MALI.

“Methali hii hutumika wakati mtu apotezapo mali yake aliyoichuma kwa jasho. Kwa mfano: Kuibiwa ng’ombe. Akakubali kupoteza mali kuliko maisha yake akisema: “Bora uhai kuliko mali iwezayo kupatikana tena.” Mali ni rahisi. Uhai ni bora kuliko mali. Mtu aliyekufa hawezi kutafuta mali tena.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 61.

Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule anayejali zaidi uhai wa watu kuliko mali, katika maisha yake. Mtu huyo hufundisha pia wenzake namna ya kuthamini zaidi uhai wa watu wao, kuliko wanavyothamini mali zao. Ndiyo maana mtu huyo huwaambia watu kwamba, “Bora uhai kuliko mali iwezayo kupatikana tena.”

“Katika maisha yetu uzima wa kimwili ni jambo muhimu ambao tunaupenda na kuutunza kuliko mambo yote. Tena tunatumia kila njia usipotee au usiharibike.

Yesu Kristo alikuja hapa duniani atupe uzima, siyo uzima wa kimwili, bali uzima wa Mungu mwenyewe. (Tazama Yohane 10:10). Uzima huu unapatikana kwa kumwamini Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu baba (tazama Yohane 3:16). Kuna faida gani kupata ulimwengu wote na kukosa uzima unaopatikana bure kwa imani? Au kuna faida gani kujitenga na Mungu?

Methali hii yatufundisha kuzingatia uzima wa milele unaodumu kuliko kuzingatia mambo yasiyodumu (Taz. 2Kor. 4:18). Tena yatufundisha kutunza uzima wetu wa kimwili, na kuepuka yote yanayoweza kuuharibu uzima ule.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 62.

Mathayo 19:16. “Mtu mmoja akamjia Yesu na kumwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?””

Marko 8:36. “Mtu atafaidiwa nini kama akiupata ulimwengu wote lakini akaipoteza nafsi yake?”

Yohane 3:16. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Yohane 6:27. “Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.”

Yohane 10:10. “Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele.”

masai1

nsabhi masai

bhatalii bha bhuganda

ENGLISH: LIFE IS BETTER THAN WEALTH.

This saying has its origin on losing wealth one has accumulated for a long time. One can lose wealth through being stolen, burnt by fire and other calamities. When this happens, as a way to comfort oneself, one can come up with this saying that ‘life is better than wealth.’ As long as one is still alive, he/she can look for more wealth but it is impossible for someone dead to look for properties (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 61).

This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.

This saying can be compared to a person who cares more about human life than material things. The person also teaches his/her colleagues how to value other people’s lives more than they value their property.

In our lives, physical well-being is the most important thing than anything else. We have to protect our life so that it doesn’t get lost or destroyed.

Jesus Christ came to earth to give us life, not physical life, but the life of God himself (See John 10:10). This life is obtained by believing in Jesus Christ sent by God the Father (see John 3:16). What good is it to gain the whole world and to lose  etenarl? Or what are the benefits of separating yourself from God?

This saying teaches us to focus on eternal life rather than perishable things (cf. 2 Cor. 4:18). It also teaches us how to take care of our physical well-being, and to avoid anything that might destroy that life (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 62).

Matthew 19:16. Mark 8:36. John 3:16. John 6:27. John 10:10.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.