Ikalagu yiniyi igalenganijiyagwa na linti lya nshishi ilo lilina bhushishi wingi nu mayu myaji uyo alonghya ng’wana okwe. Guti umo ligabyalilaga noyi ilinshishi bhushishi ubho mpaga bhugaginamyaga amatambi galyo, mpaga giki ung’wana agadulaga ugubhuyobha ubhushishi bholyo.
Giko umayu umyaji umo agang’ongheja na gunanhana ung’wana okwe. Ikalagu yiniyi ilidolekeja bhutogwa bho ng’wa mayu ukuli ng’wana okwe.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 43.
Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
“Ikalagu yiniyi ilidulanga guti umo umayu myaji atogelilwe ugunhanghana na gunhisha ung’wana okwe. Makanza gose umoyo gokwe ugojimayu guling’waje ukuli ng’wana okwe oseose.
Ubhutogwa bho ng’wa Mulungu ukubhise nghangala ningi umu Biblia bhugalinganijiyagwa na bhutogwa bho ng’wa mayu umyaji ukuli ng’wana okwe. UMulungu adutogilwe guti mayu umyaji umo antogelilwe ung’wana okwe. (Lolaga Isaya 49:14-15).
Umukabhila ya Bhamasai bhagang’witanaga UMulungu kulina lya ng’wa “Mayu uyo agonghyaga.” Hangi ilikanisa Alimayu wise. “Ulududuzunyaga ikigi Ikanisa alimayu wise nu Mulungu dudula uguyomba giki ali B’ab’a” (Mt. Augustino).
Uludulema ugulikumilija ilikanisa dulilema ugunkumilija UMulungu B’ab’a (lolaga Luka 10:16). IKanisa ali mayu uyo adutogilwe na agadulanghanaga ayise bhana bhakwe bho nduhu bhukomanya nulu bhubhaguzi. Makanza gose umoyo gokwe ugojimayu goling’waje uku bhana bhakwe. IKanisa ali mayu wise uyo agadubyalaga umuSakramenti ya bhatizimu (Lwinze lo bhatizimu hi nhumbi ya Kanisa), uyo agadulishaga na gudung’wisha umu Sakramenti ya Ekaristi.
Hangi UBikira Maria ali mayu. Ali mayu o ng’wa Yesu na mayu wise guti umo dulisomela umu Injili ya ng’wa Yohane (lolaga Yohane 19:26-27). Uweyi hu mayu uo Kanisa, hu mili gokwe UYesu Kristo. Guti nu mayu myaji umo agalumilagwa bhusungu mpaga ung’wana abyalwe, giko nu mayu wise u Bikira Maria agadubhonelaga bhupina ayise bhana bhakwe mpaga UKristo ashikane umugati yise.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 44.
Isaya 49:15-16.
Isaya 66:12-13.
Zaburi 133:2.
Wagalatia 4:26-27.
Luka 10:16.
KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.
MKWAJU WANGU UMEJAA KOCHOKOCHO. HATA MTOTO ANAWEZA KUCHUMA:- MATITI YA MAMA.
Kitendawili hiki kinafananisha mti wa mkwaju wenye matunda mengi na mama mzazi anayemnyonyesha mtoto wake. Kama mkwaju ukizaa sana, matawi huinama kiasi kwamba hata mtoto aweza kuchuma matunda yake.
Ndivyo mama mzazi anavyomnyonyesha na kumtunza mtoto wake. Kitendawili hiki kinatuonesha upendo wa mama kwa mtoto wake. Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 43.
Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
“Kitendawili hiki kinafundisha kama mama mzazi anavyopenda kumtunza na kumlisha mtoto wake. Daima moyo wake wa kimama uko wazi kwa mtoto wake yeyote.
Upendo wa Mungu kwetu sisi mara nyingi katika Biblia unalinganishwa na upendo wa mama mzazi kwa mtoto wake. Mungu anatupenda kama mama mzazi anavyompenda mtoto wake. (Tazama Isaya 49:14-15).
Katika lugha yao Wamaasai wanamwita Mungu kwa jina la “Mama Anyonyaye.” Tena kanisa ni Mama Yetu. “Tusipokubali kuwa kanisa ni mama yetu hata Mungu hatuwezi kusema kwamba ni Baba” (Mt. Agustino).
“Tukikataa kulisifu kanisa tunakataa kumsifu Mungu Baba (tazama Luka 10:16). Kanisa ni mama anayetupenda na kutulinda sisi watoto wake bila ugaguzi. Daima moyo wake wa kimama uko wazi kwa watoto wake. Kanisa ni mama yetu anayetuzaa katika Sakramenti ya Ubatizo (Kisima cha ubatizo ni tumbo la kanisa), anayetulisha na kutunywesha katika Sakramenti ya Ekaristi.
Pia Bikira Maria ni mama. Ni mama wa Yesu na Mama yetu kama tulivyosoma katika Injili ya Yohane (tazama Yohane 19:26-27). Yeye ndiye mama wa kanisa, yaani mwili wake Yesu Kristo. Kama mama mzazi anavyoona uchungu mpaka mtoto azaliwe, vilevile Mama yetu Bikira Maria anavyotuonea uchungu sisi watoto wake mpaka Kristo akamilike ndani yetu.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 44.
Isaya 49:15-16. ““Je, mama aweza kumsahau mtoto aliyeko matitini mwake akinyonya? Wala asiwe na huruma juu ya mtoto aliyemzaa? Ingawa anaweza kusahau, Mimi sitakusahau wewe! Tazama, nimekuchora kama muhuri katika vitanga vya mikono yangu, kuta zako zi mbele yangu daima.”
Isaya 66:12-13. “Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: “Nitamwongezea amani kama mto, nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho, utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake na kuchezeshwa magotini pake. Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.””
Zaburi 133:2. “Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.”
Wagalatia 4:26-27. “Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu. Kwa maana imeandikwa: “Furahi, wewe uliyetasa wewe usiyezaa, paza sauti, imba kwa furaha, wewe usiyepatwa na utungu, kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wa yule aliye na mume.’’”
Luka 10:16. ““Yeye awasikilizaye ninyi, anisikiliza Mimi, naye awakataaye ninyi, amenikataa Mimi. Lakini yeye anikataaye Mimi amkataa Yeye aliyenituma.””
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME
MY TAMARIND TREE HAS MANY FRUITS TO THE EXTENT OF MAKING CHILDREN PICK ITS FRUITS WITH EASY- MOTHER’S BREASTS.
This riddle comes from the fruit-bearing tree with the name tamarind. This tamarind tree is likened to a mother bcause of sharing the attribute of bearing fruits, something sweet for others to consume. In this tree, as its fruits develop, its branches become weak and begin bending down. They can bend down to the extent of making even young children to pick its fruits with easy. This scenario of a tamarind tree is compared to that of a woman who breastfeed her baby. This riddle shows us the mother’s love for her child (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 43).
This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.
This riddle teaches us to love and care for our chidren. The mother’s heart is always open to any of her children.
God’s love for us, as indicated in the Bible, is often compared to the love of a parent for a child. God loves us just as a loving mother loves her child (See Isaiah 49: 14-15).
In their language, the Maasai call God by the name of ” Breastfeeding Mother” to compare God with a breastfeeding mother. Again the church is Our Mother. “Unless we acknowledge that the church is our mother, God will not be our Father” (St. Augustine).
If we refuse to praise the church we refuse to praise God the Father (see Luke 10:16). The Church is a mother who loves and protects us her children without exception. The mother’s heart is always open to her children. The Church is our mother; giving birth to the Sacrament of Baptism (The Source of Baptism is the womb of the church), nourishing us in the Eucharist.
The Virgin Mary is also a mother. She is the mother of Jesus and our Mother as we have read in the Gospel of John (see John 19: 26-27). She is the mother of the church, the body of Jesus Christ. Just as a mother feels the pain until the baby is born, so does the Virgin Mary suffered for us children until Christ is completed in us (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 44).
Isaiah 49: 15-16. Isaiah 66: 12-13. Psalm 133: 2. Galatians 4: 26-27. Luke 10:16.