709. BHUJINGI WAKO NG’WANA INYAMI WALEMA KOYA.

“Umulyimbo linili ilya jisuguma Ningi umo Makwenu aganhugula ningi ng’wiye, Jibishi Ng’wana Inyami, ahigulya ya bhubhi bho kajile kakwe umuwikaji nono umubhujingi.

Ilyimbo linulo liligiki, “Ubhujingi bhoko nwani one Ng’wana Inyami walema koya. Nulu, duyombe ologelejiwa kubhujingi? Sengwa ishigu jako jilingehu, jidi kule makumi atano. Mujigila ugujikwa ndugu one, Ng’wana Inyami. Ugucha guti mva, iginhu jako ija bhujingi. Abhiyo hambohambo ng’ombe, ubhebhe isonga munhumbi. Sengwa lekaga ubhujingi bhoko, ishigu jako jidikule. Mujigila ugujikwa ndugu one, Ng’wana Inyami.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, bhukurasa 46.

Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Gwandija kale Ikanisa igadulangaga gwikala jitakatifu na guduhugula ahigulya ya kajile akabhubhi umuwikaji. Ulushigu lo bhatizimu yise dugazunya gubhuzula ubhumunhu wise ubho kale kihamo na miito gabho gose agabhubhi na gunzwala Yesu Kristo.

 Hangi giki, jilihoyi iginhu ijingi ijabhubhi ijojigajilanijaga na bhujingi, dugemele guti bhusatu bho BHUKIMWI (AIDS) ubho bhugagubhinhyaga bhupanga.

Nono ishigu jiniji bhuli nyanda nulu ng’waniki, alanhale ubhupanga bhokwe jisoga na abhize na bhulumani bho mugati nu Mulungu. Na bhose bhizuke giki umo guli unpango go ng’wa Mulungu umu witoji ya jizunya, ali ngosha umo na nkima umo. Uguyela na ungi ili hanze ya npango go ng’wa Mulungu.”  Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, bhukurasa 47.

Mathayo 5:27-28.

Mathayo 15:19.

1Wakorintho 6:18.

Wakolosai 3:8.

KISWAHILI: UASHERATI WAKO UMEZIDI RAFIKI YANGU MWANA INYAMI.

“Katika wimbo huu wa Kisukuma manju mmoja Makwenu anamwonya manju mwenzake, Jibishi mwana Inyami, kuhusu ubaya wa mwenendo wake maishani, hasa uasherati. Tafsiri ya wimbo huo kwa Kiswahili ni hii:

“Uhuni wako umezidi rafiki yangu, Mwana Inyami. Ama, tuseme umelogwa kwa hayo mambo ya kihuni? Sengwa siku zako chache, siyo mbali hamsini. Kaburini utazikwa ndugu yangu, Mwana Inyami. Utakufa kama mbwa, kwa mambo hayo ya kihuni. Wenzio bora ng’ombe, wewe mshale tumboni. Sengwa acha wako uhuni, siku zako siyo mbali. Kaburini utazikwa ndugu yangu, Mwana Inyami.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 46.

Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Tangu zamani kanisa linatufundisha kuishi kitakatifu na kutuonya kuhusu mwenendo mbaya maishani. Siku ya ubatizo wetu tulikubali kuvua utu wetu wa kale pamoja na matendo yake yote mabaya na kumvaa Yesu Kristo.

Tena kuna mambo mengine mabaya yanayoambatana na uasherati, kwa mfamo, ugonjwa wa UKIMWI (AIDS) unaofupisha maisha.

Hasa siku hizi kila kijana achunge maisha yake vizuri na awe na uhusiano wa ndani na Mungu. Pia wote wakumbuke kwamba kadiri ya mpango wa Mungu katika ndoa ya Kikristo kuna mume mmoja na mke mmoja. Kutembea na mwingine ni nje ya mpango wake Mungu.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 47.

Mathayo 5:27-28. “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini’. Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”

Mathayo 15:19. “Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.”

1Wakorintho 6:18-20. “Ikimbieni zinaa. Dhambi nyingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe. Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambazo ni mali ya Mungu.”

Wakolosai 3:8. “Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote, yaani: Hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu.”

singing flutes music sound

AFRICAN DANGIN GROUP

 

people singing

 

ENGLISH: YOUR FORNICATION BEHAVIOUR MY FRIEND INYAMI’S SON IS TOO MUCH.

This saying comes from one of the Sukuma song where a singer, Makwenu, warns his fellow singer Inyami’s son about his evil deeds; being a fornicator. The song goes as follows:

Your fornication is too much my friend  Inyami’s son. Are you bewitched? Stay away from your fornication, you have few days to live on eath, not more than fifty from now. You will soon be buried my brother, Inyami’s son. You will die like a dog, with those evil things (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 46).

This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.

The church has long taught us to live holy and has warned us about the bad ways of life. On the day of our baptism we agreed to strip off our old personality with all its evil deeds and put on Jesus Christ.

There are also other negative consequences associated with fornication, such as AIDS.

Every young man should look at his life well and have a close relationship with God. All should also remember that, according to God’s plan, for Christians, marriage has to do with one man, one woman. Having extramarital relationship is not God’s plan (See ‘Discovering Gospel Seeds,’ page 47).

Matthew 5: 27-28. Matthew 15:19. 1 Corinthians 6:18. Colossians 3: 8.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.