704. LIWELELO LITINA NDUGUYE. LIKATULYAGA PYE.

Lilihoyi lyimbo limo lya Jisuguma: “Liwelelo lidinabhukomanya. Ayise bhose dugucha nubhebhe mfumu. Aliyo ingelelo ugujikwa hasi. Lekaga namuwile unene. Iliyohoyi nzila imo duhu iya bhanhu. Mdizilemba giki bhulihoyi bhugota bho guhangija lufu. Ubhugota pye ubhose mugubhuleka.”

Ubhulangwa bho lyimbo linilo bhuli hape: Bhuli munhu agucha. Hunagwene ung’wimbi agimba giki, ‘Liwelelo litina nduguye. Likatulyaga pye.’ Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, bhukurasa 24.

Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Ilyimbo linilo lilidulanga higulya ya lufu. Ulufu luhihoyi bhuli lwande. Lulihoyi mubhuli nyango. Lulihoyi kulibhebhe lulihoyi kuli nene. Lugadukumyaga ayise bhose. Lugadulekanyaga na bhadugu bhise. Lugadupinihajaga noyi. Ludina bhugota nulu jaguluhangija. Ahigulya ya lufu dudina go gwita (lolaga Waebrania 9:27).

Aliyo ahigulya ya nzila ya gwikala dulinago ugogwita. Dudulile gwikala dulumanile nu Sebha. Uludikala dulumanile nu Sebha, ulufu lugwenha bhuyegi (lolaga Ufunuo 14:13).

Ilijidamu ukubhise ayise bhanhu ugugabokela amayange amatale guti lufu. Aliyo dulidakilwa gugabokela bho nduhu ugulalamika kunguno guli npango go ng’wa Mulungu ukubhise, na gudi npango ng’wa munhu oseose.” Lolaga Kugungua Mbegu za Injili, ukurasa 25.

Mwanzo 3:19.

Ayubu 1:21.

Mathayo 10:28.

Wafilipi 1:21.

Ufunuo 14:13.

KISWAHILI: MUNGU HANA UBAGUZI. SISI SOTE TUTAKUFA.

Kuna wimbo mmoja wa Kisukuma: “Liwelelo litina nduguye. Likatulyaga pye.” Tafsiri yake kwa Kiswahili ni:

“Mungu hana ubaguzi.  Sisi sote tutakufa hata uwe mganga. Lakini mwisho Utazikwa ardhini. Acha niwaambie mimi. Kuna njia moja tu ya watu. Msijidanganye kuwa mna dawa ya kuzuia kifo. Dawa zote mtaziacha.”

Maana ya mimbo huu ni wazi: Kila mtu atakufa. Ndiyo maana mwimbaji aliimba kwamba, ‘Mungu hana ubaguzi. Sisi sote tutakufa.’ Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 24.

Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

“Wimbo huu unatufundisha kuhusu kifo. Kifo kipo kwenye kila sehemu. Kipo kwenye kila mlango. Kipo kwako kipo kwangu. Kinatugusa sisi sote. Kinatuachanisha na wenzetu. Kinatuhuzunisha mno. Hakina dawa au kizuio. Kuhusu kifo hatuna la kufanya (tazama Waebrania 9:27).

Lakini kuhusu namna ya kuishi tunalo la kufanya. Tunaweza kuishi tumeungana na Bwana. Ikiwa tunaishi tumeungana na Bwana, kifo kinaleta heri (tazama Ufunuo 14:13).

Ni vigumu kwetu sisi binadamu kuyapokea matatizo makubwa kama kifo. Lakini yatusapa kuyapokea bila kulalamika kwa kuwa ni mpango wa Mungu kwetu, na siyo mpango wa mtu yeyote.” Rejea Kugungua Mbegu za Injili, ukurasa 25.

Mwanzo 3:19. “Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.”

Ayubu 1:21. Ayubu alisema, “…‘‘Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,   nami nitaondoka uchi, BWANA alinipa, naye BWANA ameviondoa, jina la BWANA litukuzwe.’’”

Mathayo 10:28. “Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanam.”

Wafilipi 1:21. “Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.”

Ufunuo 14:13. “Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa.” “Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka katika taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.’’”

bhabhini bha benini

singing musicians-

 

singing

ENGLISH: GOD DOES NOT SEGREGATE PEOPLE; ALL OF US ARE SUBJECT TO DEATH.

There is a Sukuma song that goes like “God is not seggregative . We will all die.” This means that human beings are mortal beings; they are subject to death however much they can avoid it. Even traditional doctors who provide medicines to cure people they will one day face death. The song goes further narrative that human beings should not deceive themselves that they won’t die (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 24). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.

This song teaches us about death. Death is everywhere. It’s on every door. It touches us all. It sets us apart from our fellows. It hurts us a lot. There is no medication or restriction. Regarding death we have nothing to do (see Hebrews 9:27).

About how the way we live, there is one thing we can do; we can live in union with the Lord. If we live in union with the Lord, death brings happiness (see Revelation 14:13).

It is difficult for us humans to accept such serious problems as death. But it does help us to accept it without complaining because it is God’s plan for us, not anyone else’s plan (See Discovering the Gospel Seeds, page 25).

Genesis 3:19. Job 1:21. Matthew 10:28. Philippians 1:21. Revelation 14:13.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.