“Lusumo lunulu ulyigembe lugatumilagwa golecha bhupinihazu ubho bhuli mpandika uyo ochilwa na bhadugu bhakwe bhingi. Iligembe ilo ligatumilagwa gulima jiliwa, ulu munhu ucha, ligagalukijiyagwa akatumamililwe bho gusimbila jigila ja ng’wa munhu ng’wunuyo. Ugwene huguyomba, “Igembe lyamala bhadugu bhane.” Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, bhukurasa 24.
Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agolechaga miito ga lisungu lya mili bho gubhajika abhachi. Umunhu ng’wunuyo, agapinihalaga kihamo na bhiye abho bhapandika mayange, ukunhu alibhizuka na bhadugu bhakwe abho bhinga kuwelelo.
Uweyi amanile igiki umunhu ulu uzumalika ililazima ajikwe, bho gusimbilwa jigila. Iki unimo gunuyo ugo gusimba jigila gugatumamagwa na munhu bho gutumila igembe, uweyi agalikolanijaga iligembe nu uyo alinabhudula bho gung’winja umunhu musi gubhitila lufu. Hunagwene umunhu ng’wunuyo, agayombaga giki, ‘Igembe lyamala bhadugu bhane.’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhuzunya bhudula bho ng’wa Mulungu ubho gung’winja munhu musi, gubhitila lufu, na golecha miito gi sungu lya mili bho gubhajike abhanhu abho bhazumarikaga, umuwikaji bhobho.
Mwanzo 3:19.
Ayubu 1:21.
Mathayo 10:28.
Wafilipi 1:21.
Ufunuo 14:13.
KISWAHILI: JEMBE LIMEMALIZA NDUGU ZANGU.
“Methali hii ya jembe hutumika kwa kuonyesha masikitiko yanayompata mtu aliyefiwa na ndugu zake wengi. Jembe ambalo hutumika kwa kulima chakula, mtu akifa, hugeuzwa kwa mtumizi ya kuchimba kaburi lake huyu mtu. Yaani, kusema “Jembe limemaliza ndugu zangu.” Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 24.
Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu anayeonesha matendo ya huruma kwa mwili kwa kuwazima wafu. Mtu huyo, husikitika pamoja na wenzake waliofiwa huku akiwakumbuka pia ndugu zake waliofariki.
Yeye anafahamu kwamba mtu akiaga dunia ni lazima azikwe, kwa kuchimbiwa kaburi. Kwa vile kazi hiyo ya kuchimba kaburi hufanywa na mtu kwa kutumia jembe, yeye hulifananisha jembe hilo, na yule ambaye ni mwenye uwezo wa kumuondoa mtu duniani kupitia kifo. Ndiyo maana mtu huyo, husema kwamba, ‘Jembe limemaliza ndugu zangu.’
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuuamini uwezo wa Mungu wa kumuondoa mtu duniani kupitia kifo, na kuonesha matendo ya huruma kwa mwili kwa kuwazika waliofariki dunia, maishani mwao.
Mwanzo 3:19. “Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.”
Ayubu 1:21. Ayubu alisema, “…‘‘Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi, nami nitaondoka uchi, BWANA alinipa, naye BWANA ameviondoa, jina la BWANA litukuzwe.’’”
Mathayo 10:28. “Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanam.”
Wafilipi 1:21. “Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.”
Ufunuo 14:13. “Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa.” “Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka katika taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.’’”
ENGLISH: THE HOE HAS FINISHED MY BRETHREN.
This saying has its origin on grief one has for losing many relatives. The hoe is always used for farming in order to have food and thus ensuring survival. The same hoe, when one dies, it is used to a dig grave to bury the dead fellow. This is why people came with the saying that ‘the hoe has finshed my brethren’ to communicate the number of relatives one has buried (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means, ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 24). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.
This saying can be compared to a person who shows compassion for the dead people by burying them. Such person grieves along with his/her bereaved relatives, is also remembering his/her deceased relatives.
He/she realizes that when a person dies he/she must be buried by digging a grave. Since the work of digging the grave is done using a hoe then one compares the hoe with the power to take human beings out of the world through death. That is why the man says, ‘The hoe has finished my brethren.’
The saying teaches people to believe in God’s ability to remove human beings from earth through death and to show acts of compassion for the body by burying the dead in their lives.
Genesis 3:19. Job 1:21. Matthew 10:28. Philippians 1:21. Revelation 14:13.