701. B’ULI HIWE B’UGIMBILIGWA.

Ulusumo lunulo, lyandija kuli ‘mayu uyo oshaga bhusiga hiwe. Umayu ng’wunuyo wilungujaga bho gwimba kugiki adule gwiyumilija umunimo gunuyo na gugutumama mpaga ha nhalikilo. Ugusha ahiwe jili ginhu ijo jidijinogu nu mayu agapandikaga bhukoyi. Aliyo kunguno ya matwajo ga nimo gokwe ayo galigelage ahanuma ya bhukoyi aliyumilija bho bhuyegi bho nduhu ugubhudilila ubhukoyi bhunubho.

Ulusumo lunulo lugatumilagwa kubhatinbwa ng’holo abhanhu abho bhali na makoye, nulu abhatumami kugiki bhikomeje umumakoye nulu umumilimo kunguno ubhukamu bhobho bhugubhiza bhuyegi ukubhoyi ahabhutongi na bhagulya matwajo ga nungula yabho.

Hangi ulusumo lunulo, lugatumilagwa kuli munhu uyo alikoyiwa na bhusatu bhulebhe. Ukuli munhu o mbika yiniyi ilidudaka gundilila umubhusatu bhokwe bho nduhu ugubhinzika moyo.’ Lolaga Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 12.

Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gutumama milimo bho wiyumilija na gubhatinbya ng’holo abhanhu bhabho, kugiki bhadule gutumama chiza imilimo yabho, na kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

“Yadudaka ayise gwiyumilija umugunondela UYesu Kristo bho nduhu ugugwa ng’holo dikale na wisagiji bho gupandika matwajo ga nungula yise aho bhutongi. Dubhize guti mayu uyo oshaga bhusiga umo agiyumiligija bho bhuyegi na bho nduhu ugudilila ubhukoyi bhosebhose kunguno ya matwajo ga milimo yakwe ayo galigele aha bhutongi yaho.

Padre Emmanuli Makolo wi Jimbo lya Shinyaga, Tanzania agalwandika ulusumo lunulu: “Buli hiwe bukimbiligwa” umu kadi yakwe iya bhupadirisho. Giki, agagulenganija unimo go bhubadiri nu mayu uyo Alisha.” Lolaga Kugundua Mbegu ya Injili, 13.

Waroma 12:11.

Wagalatia 6:9.

Mathayo 24:13.

Yohane 16:21.

Ufunuo 2:10.

Luka 9:62.

KISWAHILI: ULIOKO KWENYE JIWE HUIMBIWA  (MSAGAJI HUJIFARIJI KWA KUIMBA).

Methali hiyo, ilianzia kwa ‘mama anayesaga mtama kwenye jiwe. Mama huyo hujifariji kwa kuimba aweze kuvumilia katika kazi hiyo na kuifanya mpaka mwisho. Kusaga kwenye jiwe ni jambo lisilo rahisi na mama huwa anapata masumbufu. Lakini kwa sababu ya matunda ya kazi yake yatakayopatikana baadaye huwa anajikaza kwa furaha bila kujali masumbufu hayo.

Methali hii hutumika kwa kuwatia moyo watu wenye shida au wafanyakazi ili wajitahidi katika shida au kazi, kwa sababu bidii yao itakuwa furaha kwao baadaye na watakula tunda la jasho lao.

Tena methali hiyo hutumika kwa mtu anayezidiwa na ugonjwa fulani. Kwa mtu wa namna hii inatupasa kumjali katika ugonjwa wake bila kukata tamaa.’ Rejea Kugundua Mbegu za Injili, ukurasa 12.

Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kufanya kazi kwa uvumilivu na kuwatia moyo watu wao ili waweze kuyatekeleza majukumu yao vizuri na kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

“Yatupasa sisi kupiga moyo konde katika kumfuata Yesu Kristo bila kukata tamaa tukiwa na tumaini la kupata matunda ya jasho letu hapo baadaye. Tuwe kama mama mwenye kusaga mtama anavyojikaza kwa furaha bila kujali masumbufu yoyote kwa sababu ya matunda ya kazi yake yatakayopatikana baadaye.

Padre Emmanueli Makolo wa Jimbo la Shinyanga, Tanzania aliandika methali hii: “Buli hiwe bukimbilagwa” kwenye kadi yake ya upadrisho. Yaani, alifananisha kazi ya upadre na kazi ya mama mwenye kusaga.’ Rejea Kugundua Mbegu ya Injili, ukurasa 13.

Waroma 12:11. “Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.”

Wagalatia 6:9. “Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.”

Mathayo 24:13. “Atakayemumilia mpaka mwisho, ataokoka.”

Yohane 16:21. “Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni.”

Ufunuo 2:10. “Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”

Luka 9:62. “Yesu akamwambia, “Mtu ye yote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.””

stone-grinding.2

stone-grinding

 

ENGLISH: THE GRINDER OF SORGHUM SINGS TO COMFORT HERSELF.

This proverb comes from a woman who was singing while grinding sorghum. This woman was able to console herself through singing until she finishes grinding. That is why people came with the proverb ‘the grinder of sorghum sings to comfort herself’ to describe this situation. Grinding sorghum on the stone is not an easy task; it needs courage and perseverance.

This proverb is used to encourage distressed people or workers to work and be courageous enough in performing some tasks because they will benefit in future. Also this proverb can be used in the context of sickness where the sick person needs to tolerate without despair (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means, ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ page 12). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.

This proverb teaches people to work patiently and inspires people to be courageous in their lives. Patience and courage will make people to be responsible in whatever they decide to do in life. “We need to be heartfelt in following Jesus Christ without giving up hope of finding the fruit of our sweat. May we be like the grinding woman who happily presses herself with no worries because of the fruit of her labour.

Fr. Emmanuel Makolo from Shinyanga diocess, Tanzania, wrote the same proverb in his sovernior . That is, he likened the work of a priest to the work of a grinding mother (See Gospel Seed Discoveries, page 13).

Romans 12:11. Galatians 6: 9. Matthew 24:13. John 16:21. Revelation 2:10.Luke 9:62.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.