Ulusumo lunulo lwandija kuli munhu uyo wiyumilijaga gutumama nimo go gusha mpaga ugumala. Dugemele: umayu uyo alushaga bhusiga adulile guguleka unimo gokwe, kunguno ndebhe na ubhutula ubhusiga hanhelo, “kwanzula”. Aliyo agwiza agumalije.
Ulusumo lunulo lugatumilagwa kuli munhu uyo ali na wiyumilija umumilimo. Umunhu umpanga, uyo adinsadu, adadulile uguguleka unimo go gusha na guguleka sagala. Aliyo agiyumilijaga mpaga gushile.” Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘mpanga wa kusha na kwangula.’ Lolaga kugundua mbegu ya Injili, ukurasa 12-13.
Ijitabho jinijo jigandikwa na Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora, ijojigahaririwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gutumama milimo mpaga guyimala umulikanza ilobhalibhapanga, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.
Ulusumo lunulo, hangi, ‘lulidulanga higulya ya bhatizimu. Idina solobho ugubhatijiwa na gushoka nyuma hangi. Umayu uyo oshaga bhusiga, uluwitanwa ku nimo gungi, otulaga ubhusiga lwande, “kwanzula”. Aliyo kuli kanza duhu, hanuma yaho, agwiza ugugumalija unimo gokwe. Adadulile uguguleka unimo gokwe sagala. Uluuduma ugugumala unimo gokwe agusekwa na bhanhu. Gitumo UYesu agayombela ahigulya ya munhu uyo ohayaga guzenga nnala aliyo agaduma ugumalija abhanhu bhuyomba, “Umunhu uyu agandya guzenga aliyo adamalile” (Luka 14:29-30).
Giko nu munhu uyo obhatijiwa na gushoka numa adafaile umu Bhutemi bho ng’wa Mulungu, kunguno agagulekaga unimo gokwe sagala bho nduhu ugugumalija. Lolaga Kugundua mbegu ya Injili, ukurasa 13-14.
Waroma 12:11.
Wagalatia 6:9.
Mathayo 24:13.
Yohane 16:21.
Ufunuo 2:10.
Luka 9:62.
KISWAHILI: MZIMA WA KUFANYA KAZI MPAKA KUMALIZA.
Methali hiyo ilianzia kwa mtu anayevumilia kufanya kazi ya kusaga nafaka mpaka anaimaliza. Kwa mfano: mama mwenye kusaga mtama anaweza kuacha kazi yake, kwa sababu fulani na kuweka mtama pembeni, “kwanzula”. Lakini atakuja kuimalizia.
Methali hii hutumika kwa mtu mwenye bidii katika kazi. Mtu mzima, asiye mgonjwa, hawezi kuianza kazi ya kusaga na kuiacha ovyo. Bali anavumilia mpaka imalizike.” Ndiyo maana watu humuita ‘mzima wa kufanya kazi mpaka kumaliza.’ Rejea kugundua mbegu ya Injili, ukurasa 12-13.
Kitabu hicho, kiliandikwa na Kamati ya Utafiti wa utamaduni Bujora, kilichohaririwa na watafiti: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1993.
Methali hiyo hutufundisha juu ya kujibidisha kufanya kazi mpaka kuzimaliza wakati tukiwa wazima, ili tuweze kupata mafanikio mengi, katika maisha yetu.
Methali hii pia ‘inafundisha kuhusu ubatizo. Haina maana kubatizwa na kurudi nyuma tena. Mama anayesaga mtama, kama akiitwa kwa kazi nyingine, anaweka mtama pembeni, “kwanzula”. Lakini kwa muda tu, baadaye atakuja kumaliza kazi yake. Hawezi kuiacha kazi yake ovyo. Akishindwa kumaliza kazi yake atachekwa na watu. Kama Yesu alivyosema kuhusu mtu mwenye kutaka kujenga mnara lakini akashindwa kumaliza watu wakasema, “Mtu huyu alianza kujenga lakini hakumaliza” (Luka 14:29-30).
Vile vile mtu yule aliyebatizwa na kurudi nyuma hafai kwa Ufalme wa Mungu kwa sababu anaiacha kazi yake ovyo bila kuimaliza. Rejea Kugundua mbegu ya Injili, ukurasa 13-14.
Waroma 12:11. “Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.”
Wagalatia 6:9. “Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.”
Mathayo 24:13. “Atakayemumilia mpaka mwisho, ataokoka.”
Yohane 16:21. “Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni.”
Ufunuo 2:10. “Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
Luka 9:62. “Yesu akamwambia, “Mtu ye yote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.””
ENGLISH: HE/SHE IS HEALTHIER ENOUGH TO FINISH HIS/HER WORK.
This saying comes from someone who managed to grind her cereals until she finished them. A woman who is grinding her millet on a stone can be courageous enough; she can work until she finishes the millet she has arranged to grind. Even if it happens that someone interrupts her in her grinding, she will come back after that interruption and finish grinding her millet.
This saying can be compared to a person who is a hard worker. It can be likened to a person who feels sick but does not give up working (Refer to Kugundua Mbegu za Injili, which means ‘Discovering the Seed of the Gospel,’ pages 12-13). This book was written by the Bujora Cultural Research Committee, edited by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1993.
The proverb teaches us to work hard in order to achieve more in our lives.
This proverb also teaches people about baptism. It does not mean to be baptized and go back to sin again. A grinding mother, even if she is called for other tasks, can put her millet aside so that she continues with grinding when she comes back. She cannot give up her work. Failing to finish her job means she will be laughed at by people. As Jesus said, of a man who wanted to build a tower but could not finish, people said, “This man began to build but did not finish it ” (Luke 14: 29-30).
Likewise, the person who is baptized and goes back to sin is unfit for the Kingdom of God because he or she undermines the work of God (See ‘Discovering the Gospel Seed,’ pages 13-14).
Romans 12:11. Galatians 6: 9. Matthew 24:13. John 16:21. Revelation 2:10. Luke 9:62.