Aho kale olihoyi munhu uyo oliogaiwa jiliwa ahikanza lya nzala. Umunhu ng’wunuyo, ojaga agucholaga jiliwa uko usimizilaga. Lushigu lumo agajipandika ijiliwa ulya mpaga wiguta. Oho omala ugulya, aganyela haho olilaga ijiliwa jilinijo, adizukaga igiki alashoka hoyi alye hangi. Hunagwene abhanhu bhagandya guyung’wila giki, ‘aho ukalilag haho ukanyelaga.’
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo okaribhushiyagwa chiza ha kaya ya ng’wa munhu. Ubhegejiyawa chiza guti ndugu ohakaya yiniyo, bhuyulya kihamo na gwendelea.
Aha ngelelo yaho, umunhu ng’wunuyo, ushiya nu mayu uoha kaya yiniyo, nulu, wibha ginhu hoyi, nulu wita jito jose jose ijo jidijawiza.’ Ugubhilitia ya bhubhi abhanhu bhenabho, yikolile na gunyela oholilaga, umunhu ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, ‘aho ukalilag haho ukanyelaga.’ Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 70.
Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhulumbi ukubhanhu abho bhalibhitila ya wiza, bho kuleka ugubhitila iyabhubhi, kugiki bhadule gwendelea gwiyambilija chiza, umuwikaj bhobho.
“Abhanhu abho dugabhitililaga yabhubhi bhali bhanhu abho dugikalaga kihamo nabho. Dugemele: ugushiya nu nkima o nzenganwa, gung’wibhila nwani, na gwendelea.
Hangi iyiniyo yili jigemelo ukubhumani wise nu Yesu Kristo uyo agadubokelaga kuwizang’holo na gwifunya gete kubhise guti nwani. Ningiki odutogwa, bho miito gise mabhi duganhemaga na gundalaha.
Hangi umusakramenti ya Ekaristia tugadumaga ugunkuja kunguno dugalyaga mili gokwe na gung’wa mininga gakwe bho nduhu ugwigelelwa. Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 71.
Zaburi 55:12-14.
Mathayo 26:49-50.
Yohone 13:21, 25-26.
1Wakorintho 11:27.
KISWAHILI: UNAPOKULA PAPO HAPO UNAPOKWENDA HAJA.
Hapo zamani alikuwepo mtu aliyekosa chakula wakati wa njaa. Mtu huyo, alienda kutafuta chakula kule alipotembelea. Siku moja alipata chakula, akala mpaka agatosheka. Alipomaliza kula, alijisaidia papo hapo alipolia chakula. Ndiyo maana watu wakaanza kumwambia, kwamba, ’unapokula papo hapo unakokwenda haja.’
Methali hiyo hulinganisha kwa mtu yule ambaye amekaribishwa vizuri kwenye nyumba ya mtu. Akatendewa vizuri kama mmoja wa jamaa, wakila pamoja na kadhalika.
Mwishowe mtu huyo, huzini na mama wa kaya hiyo, au huiba au hutenda kitendo chote chote, ambacho si kizuri. Kuwafanyia ubaya watu hao, hufanana na kunyea pale alipolia chakula mtu huyo. Ndiyo maana watu humwambia mtu huyo, kwamba ‘unapokula papo hapo unapokwenda haja. Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 70.
Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na shukrani kwa watu wanaowatendea mema kwa kuacha kuwatendea mabaya, ili waweze kuendelea kusaidiana vizuri, katika maisha yao.
“Watu ambao tunawatendea mabaya ni watu (wale) ambao tunaokaa pamoja nao. Kwa mfano: Kuzini na bibi wa jirani, kumwibia rafiki, na kadhalika.
Tena hii ni mifano kwa uhusinano wetu na Yesu Kristo anayetupokea kwa ukarimu na kujitoa kwetu kabisa kama rafiki. Ijapokuwa ametupenda, kwa matendo yetu mabaya, huwa tunamkataa na kumdharau.
Tena katika sakramenti ya Ekaristi huwa tunashindwa kumheshimu kwa sababu tunakula mwili wake na kunywa damu yake bila kustahili.” Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 71.
Zaburi 55:12-14. “Kama aliyenitukana ni adui yangu ningevumilia, kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, ningejificha asinione. Kumbe ni wewe, mwenzangu, mshiriki na rafiki yangu wa karibu, ambaye wakati fulani tulifurahia ushirika mzuri tulipokuwa tukienda katikati ya umati hekaluni mwa Mungu.”
Mathayo 26:49-50. “Mara akamjia Yesu na kumsalimu, “Salaam, Rabi!’’ Akambusu. Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya kile ulichokuja kufanya hapa.”
Yohane 13:21, 25-26. “Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, ‘‘Amin, amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.’’ Yule mwanafunzi akiwa amemwegemea Yesu akamwuliza, ‘‘Bwana tuambie ni nani?’’ Yesu akajibu, ‘‘Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.’’ Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.”
1Wakorintho 11:27. “Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana.”
ENGLISH: YOU DEFACATE WHERE YOU ATE FOOD FROM.
Once upon a time ago, there was a person who had no food during famine. One day this person travelled in search for food. He reached somewhere where he got food, ate it to his satisfaction. When he had satisfied with the food he defacate on that place. This is why people say ‘you defacate where you ate food from.’
This saying can be compared to a person who is most welcomed in someone’s house. Such a person was well treated. Finally, instead of appreciating for the kindness, turns around the host by embarrassing him/her. This embarrassment can be stealing from his/her host or anything that disturbs their relationship (Refer to Kueneza Injili kwa Methali’ which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 70). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.
This saying teaches people to be thankful to people who do good for them. They don’t have to return embarrassment for good things they have done to them.
The people we are abusing are the people we are living with. For example, committing adultery with a neighbor’s wife, robbing a friend, and so on.
Again these are examples of our association with Jesus Christ, who graciously accepts us and gives Himself completely as a friend. Although He loves us, by our evil deeds, we often reject and despise him.
And in the sacrament of the Eucharist we often fail to honor Him because we eat His flesh and drink His blood unworthily (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 71).
Psalm 55: 12-14. Matthew 26: 49-50. John 13:21, 25-26. 1 Corinthians 11:27.