696. NZUGA (NZUGILA) LUSEKO, NULU, NDEKA LUSEKO.

Aho kale olihoyi nkima umo uyo wikalaga ha chalo jilebhe. Lushigu lumo apandika ngeni uyo oliofumila kulipande lya kule. Ungeni  ng’wunuyo, oliotuubha noyi kunguno ya gusiminza lugendo lulihu.

Umayi ng’wunuyo, uyo oliombokela ungeni okwe, agandya mahoha higulya ya ginhu ja mbika ningi. Umumahoya genayo, ungenihwa omanaga wisekeleja bho nduhu ugunzugila ijiliwa ungeni okwe ng’wunuyo.

Nose ungeni ng’wunuyo, ubhona ubhujiku bhulingila bho nduhu uguzugilwa ijiliwa, ubadija giki, umayu uyo aliyitya wizang’holo bho golecha luseko lo hanze, gashinaga umugati ya ng’holo yakwe adahayile ungeni alye ijiliwa jakwe.

Ungeni ng’wunuyo, agagema gunhaga ung’wenyeji okwe, kugiki abhone niagushosha ginehe, bho guyomba, ‘mlihoyi unene nashoke kaya.’ Umayu uyo agashosha, ‘sawa dugwibhona lushiku lungi.’ Hunagwene abhanhu bhagandya guyung’witana umayu ng’wunuyo, giki ‘nzuga (nzugila) luseko.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyolechaga bho hanze giki ali ng’wizang’holo, aliyo umugati yakwe, ali ming’holo. Umunhu ng’wunuyo agamanaga useka na kuhoya kihamo nu ngeni bho nduhu ugunzugila ijiliwa.

Ulu munhu adatogilwe nulu adahayile ugugwitila ginhu jilebhe idilazima aguwile giki, nadagutogilwe au nadahayile; ugudula gudebha bho shitwa shakwe, guti numo agitila umayu uyo oliombokela ngeni. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘nzuga (nzugila) luseko.’ Lolaga kueneza Injili Kwa Methali, bhukurasa 66.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizang’holo bho ng’hana gufumila mu ng’holo jabho, gutinda ugubhiza bhibheleja giki wizang’holo, bho hanze duhu, aliyo bhiming’holo umumioyo yabho, kugiki bhadule gubhagola chiza abhageni bhabho, umuwikaji bhobho.

“Umuwikaji wise ubho ng’wa Kristo, amiito gali na solobho gukila imihayo. UYesu Kristo adayombile mihayo duhu bho nduhu miito. Aliyo wikalaga agubhitilaga ya wiza abhanhu mpaga uduchila ha nsalabha.

Ulu munhu adagutogilwe idilazima aguwile, “Nadagutogilwe” nulu “nadahayile.” Ugudula gumaga bho shitwa shakwe, guti nu kuli nkima uyo adazugaga jilila, aliyo guseka duhu.

Nulu ayise bhakristo ilijidamu noyi ugung’wila UYesu, “Nadagutogilwe”, nulu, nadahayile”. Aliyo dugampejaga bho miito gise mabhi. Dudanzugilaga UYesu Kristo, dugayombaga, “Sebha! Sebha! bho nduhu ugwikala gitumo bhuli ubhulangwa bhokwe.” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 66.

Yakobo 2:15-17.

1Yohane 3:18.

Mathayo 15:8.

Mathayo 7:21.

KISWAHLI: MPIKA KICHEKO.

Hapo zamani alikuwepo mama mmoja aliyeishi katika kijiji fulani. Siku moja alitembelewa na mgeni aliyetoka sehemu za mbali. Mgeni huyo alishikwa na njaa kwa sababu ya kusafiri safari ndefu.

Mama huyo alimpokea mgeni wake wakaanza maongezi yaliyohusu mambo mbalimbali. Katika maongezi hao, mwenyeji wake alikuwa akicheka sana bila kumpikia chakula mgeni wake huyo.

Mwishowe yule mgeni akaona usiku unaingia bila kupikiwa chakula, akagundua kwamba, mama yule anajifanya mkarimu kwa kuonesha kicheko cha nje, kumbe ndani ya moyo wake hataki mgeni huyo ale chakula chake.

Mgeni huyo, aliamua kujaribu kumuaga mwenyeji wake, ili aone kama atakubali au la, kwa kusema, ‘kwa heri mimi narudi nyumbani.’ Mama yule alijibu, ‘sawa tutaonana siku nyingine.” Ndiyo maana watu wakaanza kumuita mama yule, ‘mpika kicheko.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu anayejionesha kwa nje kuwa ni mkarimu, lakini kwa ndani ni mchoyo. Mtu huyo, huwa anacheka na kuzungumumza pamoja na mgeni, bila kumpikia chakula.

Ikiwa mtu hakupendi au hataki kukufanyia jambo fulani si lazima akuambie sikupendi au sitaki; utaweza kujua kwa vitendo vyake, kama alivyofanya yule mama aliyepokea mgeni. Ndiyo maana watu humuita mtu huyo huwa ni ‘mpika kicheko.’ Rejea kueneza Injili kwa methali, ukurasa 66.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kweli kutoka mioyoni mwao, badala ya kuwa wanafiki, ambao huuonesha ukarimu kwa nje tu, lakini kwa ndani ni wachoyo, ili waweze kuwatunza vizuri wageni wao, katika maisha yao.

“Katika maisha yetu ya Kikristo matendo yana maana kuliko maneno. Yesu Kristo hakusema maneno tu bila matendo. Bali alikuwa akiwatendea mema watu mpaka katufia msalabani.

Ikiwa mtu hakupendi si lazima akuambie, “Sikupendi” au “sitaki”. Utaweza kujua kwa matendo yake. Kama kwa mwanamke asiyepika chakula, ila kucheka tu. Hata sisi wakristo ni vigumu sana kumwambia Yesu, “Sikupendi”, au “sitaki”. Lakini huwa tunamfukuza kwa matendo yetu mabaya. Hatumpikii Yesu Kristo, tukisema “Bwana! Bwana!”, bila kuishi kadiri ya mafundisho yake.” Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 66.

Yakobo 2:15-17. “Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, mmoja wenu akamwambia, ‘‘Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,’’ pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini? Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa.”

1Yohane 3:18. “Watoto wangu wadogo, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na katika kweli.”

Mathayo 15:8. “‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.”

Mathayo 7:21. “Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”

african happy women

adult2

adults

 

ENGLISH: A COOK OF LAUGHTER.

Once upon a time ago there was a woman who lived in a certain village. One day this woman was visited by visitor and this visitor had walked for a long distance and she needed food. The host received her visitor and began conversation on different issues. The host could burst into laughter most of the time. She never thought of cooking for her guest. When the night was about to fall, the guest suggested to leave and the host replied , ‘Good luck, we will meet sometime.’ This why people began calling this host woman as someone who cook laughter.

This saying can be compared to a person who outwardly displays a generous heart, but inwardly, he/she is greedy. These are the people who will laugh and talk without thinking of cooking for their visitors.

If someone doesn’t like you or doesn’t want to do something for you, they don’t have to tell you ‘I don’t like you or I don’t want you;’ you will know by their actions. That’s why people call this host a ‘cook of laughter.’ (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 66). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

The saying teaches people to be genuinely generous from their heart, rather than hypocrites. In so doing, they can take good care of their guests in their lives.

“In our Christian life actions are more meaningful than words. Jesus Christ didn’t just say words without actions. But he was doing good to the people until He died on the cross.

If someone doesn’t love you he/she doesn’t have to tell you, “I don’t like you” or “I don’t want you”. You will know by their actions. As for a woman who does not cook food, only to laugh, even we Christians are very hard to say to Jesus, “I don’t love you”, or “I don’t want you”. But we usually expel Him through our evil deeds. We deny Jesus Christ by saying, “Lord! Lord! ”, without living up to His teachings (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 66).

James 2: 15-17. 1 John 3:18. Matthew 15: 8. Matthew 7:21.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.