695. WABYALILWA HIKULU.

Ulusumo lunulo, lwandija kubhanhu abho bhagankaribhusha ng’wichabho uyo agabhasanga bhalilya jiliwa bho gung’wila giki, ‘wabyalilwa hikulu.’ Mumho giki, wabyalilwa ha kaya iyo ili najiliwa, nulu hakaya ya ntemi.

“Ikale ulu munhu winhiwa bhutemi nu ubhutemi bhokwe bhubhiza na nzala agupejiwa umubhutemi, nu ulu ijiliwa jubhiza ja shili na ndulu, na gwendelea, ntemi ng’winuyo witanagwa ntemi obhakima. Ulu jiliwa ja bhusiga bhingi, agwitanwa ntemi o “Bhagosha”.

Ulu bhanhu bhumala ugulya bhagatulaga magofi guti numo bhitila ikale abho bhangishaga untemi, mumho giki, bhagasunde ijiliwa, kunguno utemi omalaga gubhita. Bhamalaga ugulya.” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, 64.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizang’holo bho gubhakaribhusha abhanhu aha jiliwa jabho, kunguno ijiliwa jili na solobho umugubhulang’hana ubhupanga bho bhanhu bhose.

“Umuwikaji bho munhu ijiliwa nulu ubhugali hi ginhu ja solobho noyi. Ubhugali hu ntemi wise kunguno agadulang’hanijaga ubhupanga wise.

Hangi UMhayo go ng’wa Sebha guli jiliwa ijojigadinhaga bhupanga bho ng’wa Mulungu ng’winikili ubho bhudakenagukaga.

ISakramenti iya Ekaristi jili jiliwa ng’hana na ja solobho noyi ijojibhugalang’hanaga na gubhujamya ubhupanga ubho bhuli bho ng’wa Mulungu umugati yise. “Uyo agulyaga mili gone na gun’gwa mininga gane, agikalaga mugati yane nu nene mugati yakwe.” (Yohana 6:56).

Uluushiga Mukanisa ugunsanga Untemi oko UYesu Kristo, alimo umu shimile sha Ngate umugati ya Tabarnakulo. Adingaga, nulu adabhitaga. Uguzunya gwise ugojigatoliki guliduwila na guduhagigish’ija giki, UYesu Kristo alimo nhana umu shimile sha ngate umu Sakramenti ya Ekaristia. Kuyiniyo, igeleliwe gunamya na gunkuja umu Sakramenti yiniyi Uweyi uyo Ali Ntemi wise bho guntulila mgofi.” Lolaga, Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 65.

Kumbukumbu 8:3.

Yeremia 15:16.

Yohane 4:34.

Yohane 6:11-15.

Yohane 6:51, 57.

Mathayo 6:11.

KISWAHILI: UMEZALIWA IKULUNI.

Methali hiyo, ilianzia kwa watu waliomkaribisha mwenzao aliyewakuta wakila chakula kwa kumwambia kwamba, ‘umezaliwa ikuluni.’ Maana yake amezaliwa kwenye kaya yenye chakula, au kaya ya mtemi.’

“Zamani ikiwa mtu amepewa utemi, na utawala wake ukawa na njaa, atafukuzwa katika utemi, na kama mavuno yatakuwa ya kunde, choroko, na kadhalika, mtemi huyo huitwa mtemi wa wanawake. Kama mavuno ya mtama ni tele, huitwa mtemi wa “Bagosha” wanaume.

Ikiwa watu wamekwisha kula huwa wanapiga makofi kama walivyofanya zamani wakimsalimu mtemi, maana yake wachukue vyombo, kwa kuwa mtemi amekwisha pita. Wamemaliza kula.” Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 64.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha watu kwenye chakula chao, kwa sababu chakula ni muhimu katika kutunza uzima wa mwanadamu wote.

“Katika maisha ya mtu chakula au ugali ni kitu muhimu sana. Ugali ni mtemi wetu kwa kuwa unatutunzia uzima wetu.

Tena Neno la Bwana ni chakula ambacho kinatupa uzima wa Mungu ndani yetu, uzima wa Mungu mwenyewe usioharibika.

Sakramenti ya Ekaristi ni chakula kweli na cha maana sana kinachotunza na kuimarisha uzima ule wa Mungu ndani yetu. “Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, akaa ndani yangu nami ndani yake.” (Yohane 6:56).

Ukifika kanisani utamkuta mtemi wako Yesu Kristo yumo katika maumbo ya mkate ndani ya Tabernakulo. Haondoki au kupita. Imani yetu ya kikatoliki yatujulisha na kutuhakikishia kwamba Yesu Kristo yumo kweli katika maumbo ya mkate katika sakramenti ya Ekaristi. Kwa hiyo yatupasa kumwabudu na kumtukuza katika sakramenti hii yeye aliye mtemi wetu kwa kumpigia makofi.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 65.

Kumbukumbu 8:3. “Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha BWANA.”

Yeremia 15:16. “Maneno yako yalipokuja, niliyala, yakawa shangwe yangu na furaha ya moyo wangu, kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA Mungu, Mungu Mwenye Nguvu.”

Yohane 4:34. “Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.”

Yohane 6:11-15. “Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wamekaa kwa kiasi walichohitaji. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadri alivyotaka. Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee cho chote.’’ Hivyo wakavikusanya wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vilivyobaki vya ile mikate mitano na samaki wale wawili wadogo.

Baada ya watu kuona mwujiza ule Yesu aliofanya, walianza kusema, “Hakika huyu ndiye Nabii ajaye ulimwenguni!’’ Yesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke Yake.”

Yohane 6:50- 57. “Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’

Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?’’ Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu.

Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.”

Mathayo 6:11. “Utupe leo chakula chetu tunachohitaji.”

food woman

food-5

food-4

 

ENGLISH: YOU WERE BORN IN PALACE.

This saying comes from a certain person who arrived at his fellow’s house and found them eating food. As a way to welcome him, they said ‘you were born in palace’ to mean the land of plenty and abundance; a house of the king. In the past, when someone is installed as a king in a certain area he was to ensure that his people do not suffer from hunger and if the harvest will be only crops such as cowpeas, groundnuts and other food crops, he was regarded as a king of women. But if people will manage to have good harvests of crops such as sorghum, he will be regarded as the king of men.

Kings, in the past, were highly respected. This is why people could stand and cheer him up by clapping hands when he passes around. The same to food, people will tend to clap hands when they finish eating, in the same way they used to cheer up their king. In this case, their clapping of hands means calling someone responsible to collect the vessels after they have finished eating. They clap hands to mean that the ‘king has already gone’ Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 64). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

This saying teaches people about the generosity of welcoming people to their food, because food is essential to the wellbeing of the human body and life in general.

“In a person’s life food is the most important thing. Food is our king in that it gives us life.

Again the Word of the Lord is the food that gives us the life of God in us, the life of God Himself who is immortal.

The sacrament of the Eucharist is a true and very important food that sustains and enhances the life of God in us. “Whoever eats my flesh and drinks my blood dwells in me and I in him” (John 6:56).

When you get to the church you will find your Lord Jesus Christ in the form of bread in the Tabernacle. He doesn’t leave. Our Catholic faith informs us and assures us that Jesus Christ is indeed in the form of bread in the sacrament of Eucharist. Therefore, we must worship and glorify in this sacrament. ” (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 65).

Deuteronomy 8: 3. Jeremiah 15:16. John 4:34. John 6: 11-15. John 6:51, 57. Matthew 6:11.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.