694. WASANGA NTEMI WABHITA.

Ulusumo lunulo, lwandija kuli munhu uyo agabhasanga abhiye bhamalaga ugulya ijiliwa. Umunhu ng’wunuyo, agawilwa giki, ‘wasanga Ntemi wabhita.’ Ukwene, huguhaya giki, wasanga bhamalaga ugulya.

“Ikale untemi uluubhasanga abhanhu bhalihalibhilimga, nulu ha nimo, bhimilaga na gungisha. Aliyo untemi ulubhasanga bhalilya, goli ng’wiko ugwimila na gungisha. Ulunibhangisha niobhaobhalemeja na gubhawila: “Unene nadalang’hanalaga ubhupanga wing’we, ubhugali hugabhulang’hanaga ubhupanga wing’we; hangi bhugalang’hanaga ubhupanga bhone. Unene nadi ntemi wing’we. Ijiliwa, nulu ubhugali hu ntemi wing’we. Idichiza ugunkuja ntemi gulebha ijiliwa.”

Mpaga lelo uluubhasanga bhanhu bhalilya guling’wiko ugwigisha, kunguno bhalihoya na ntemi obho. Ulubhumala ugulya bhagatulaga magofi kugiki bhize gwinja jiseme, mumho giki, untemi omalaga gubhita. Bhamalaga ugulya.” Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba ukuli munhu uyo osangaga abhiye bhamalaga ugulya, giki, ‘wasanga ntemi wabhita.’ Lolaga kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 64.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gudebha solobho ya jiliwa bhogolecha ikujo, kunguno hijene hijo jigadinhaga nguzu ja gwendelea gwikala na guitumama chiza imilimo yise.

“Umuwikaji bho munhu ijiliwa nulu ubhugali hi ginhu ja solobho noyi. Ubhugali hu ntemi wise kunguno agadulang’hanijaga ubhupanga wise.

Hangi UMhayo go ng’wa Sebha guli jiliwa ijojigadinhaga bhupanga bho ng’wa Mulungu ng’winikili ubho bhudakenagukaga.

ISakramenti iya Ekaristi jili jiliwa ng’hana na ja solobho noyi ijojibhugalang’hanaga na gubhujamya ubhupanga ubho bhuli bho ng’wa Mulungu umugati yise. “Uyo agulyaga mili gone na gun’gwa mininga gane, agikalaga mugati yane nu nene mugati yakwe.” (Yohana 6:56).

Uluushiga Mukanisa ugunsanga Untemi oko UYesu Kristo, alimo umu shimile sha Ngate umugati ya Tabarnakulo. Adingaga, nulu adabhitaga. Uguzunya gwise ugojigatoliki guliduwila na guduhagigish’ija giki, UYesu Kristo alimo nhana umu shimile sha ngate umu Sakramenti ya Ekaristia. Kuyiniyo, igeleliwe gunamya na gunkuja umu Sakramenti yiniyi Uweyi uyo Ali Ntemi wise bho guntulila mgofi.” Lolaga, Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 65.

Kumbukumbu 8:3.

Yeremia 15:16.

Yohane 4:34.

Yohane 6:11-15.

Yohane 6:51, 57.

Mathayo 6:11.

KISWAHILI: UMEKUTA MTEMI AMEPITA.

Methali hiyo ilianzia kwa mtu aliyewakuwa wenzie wamekwisha kula chakula. Mtu huyo, aliambiwa na wenzake hao kwamba, “umekuta mtemi amepita,” Maana yake, amewakuta wamemaliza kula.

“Zamani mtemi akiwakuta watu kwenye mkutano au kazini, walisimama na kumsalimu. Lakini akiwakuta wanakula, ilikuwa mwiko kusimama na kumsalimu. Kama wangelimsalimu, angeliwakataza na kuwaambia: “Mimi situnzi maisha yenu, ugali hutunza maisha yenu; tena hutunza maisha yangu. Mimi si mtemi wenu. Chakula au ugali ni mtemi wenu. Si vizuri kumtukuza mtemi kuliko chakula.”

Mpaka leo ukiwakuta watu wanakula ni mwiko kusalimiana, kwa maana wanaongea na mtemi wao. Wakimaliza kula wanapiga makofi ili waje kuondoa vyombo, maana yake mtemi amekwisha pita. Wamemaliza kula.” Ndiyo maana watu walianza kusema kwa mtu aliyewakuta wamekula, kwamba, ‘umekuta mtemi amepita.’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 64.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kutambua umuhimu wa chakula kwa kuonesha heshima kwa sababu, hicho ndicho kinachowapatia uhai, na nguvu za kuendelea kuishi na kufanya kazi zao vizuri.

“Katika maisha ya mtu chakula au ugali ni kitu muhimu sana. Ugali ni mtemi wetu kwa kuwa unatutunzia uzima wetu.

Tena Neno la Bwana ni chakula ambacho kinatupa uzima wa Mungu ndani yetu, uzima wa Mungu mwenyewe usioharibika.

Sakramenti ya Ekaristi ni chakula kweli na cha maana sana kinachotunza na kuimarisha uzima ule wa Mungu ndani yetu. “Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, akaa ndani yangu nami ndani yake.” (Yohane 6:56).

Ukifika kanisani utamkuta mtemi wako Yesu Kristo yumo katika maumbo ya mkate ndani ya Tabernakulo. Haondoki au kupita. Imani yetu ya kikatoliki yatujulisha na kutuhakikishia kwamba Yesu Kristo yumo kweli katika maumbo ya mkate katika sakramenti ya Ekaristi. Kwa hiyo yatupasa kumwabudu na kumtukuza katika sakramenti hii yeye aliye mtemi wetu kwa kumpigia makofi.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 65.

Kumbukumbu 8:3. “Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha BWANA.”

Yeremia 15:16. “Maneno yako yalipokuja, niliyala, yakawa shangwe yangu na furaha ya moyo wangu, kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA Mungu, Mungu Mwenye Nguvu.”

Yohane 4:34. “Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.”

Yohane 6:11-15. “Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wamekaa kwa kiasi walichohitaji. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadri alivyotaka. Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee cho chote.’’ Hivyo wakavikusanya wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vilivyobaki vya ile mikate mitano na samaki wale wawili wadogo.

Baada ya watu kuona mwujiza ule Yesu aliofanya, walianza kusema, “Hakika huyu ndiye Nabii ajaye ulimwenguni!’’ Yesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke Yake.”

Yohane 6:50- 57. “Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’

Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?’’ Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu.

Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.”

Mathayo 6:11. “Utupe leo chakula chetu tunachohitaji.”

food6

ntemi zulu-kingdom-

child eating food

ENGLISH: YOU HAVE FOUND THE CHIEF GONE.

This proverb has its origin from someone who found his fellows had finished eating food. To report to him that they had already eaten food, they told him that “you found the chief gone” meaning that they had finished eating food.

“In the past when the chief walked in for meeting or any business, people around him were to stand up and greet him as a sign of respect. But if the chief reaches a certain place and finds people eating, he was not allowed to stop them from eating. Even if people can stand to greet him he could stop them saying that food keeps peoples’ lives but the chief does not. He (chief) also respects food because it gives him life. Until today, when people are eating they don’t have to speak to each other because they are busy with their chief, food. When they finish eating, they clap hands as a sign of calling the one responsible to collect the vessels used for eating. This is the time one can say ‘the chief has gone’ (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 64). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

The proverb teaches people to recognize the importance of food by showing respect because that is what gives them life and the power to continue living and doing their jobs.

In a person’s life food is the most important thing. Food is our chief in that it gives us life.

Again the Word of the Lord is the food that gives us the life of God in us, the life of God Himself who is immortal.

The sacrament of the Eucharist is a true and very important food that sustains and enhances the life of God in us. “Whoever eats my flesh and drinks my blood dwells in me and I in him” (John 6:56).

When you get to the church you will find your Lord Jesus Christ in the form of bread in the Tabernacle. He does not go away or pass away. Our Catholic faith informs us and assures us that Jesus Christ is indeed in the form of bread in the sacrament of Eucharist. Therefore, we must worship and glorify Him through this sacrament (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 65).

Deuteronomy 8: 3. Jeremiah 15:16. John 4:34. John 6: 11-15. John 6:51, 57. Matthew 6:11.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.