693. KUGULU KULI NG’OMBE IDAKO ILALIJA.

Ulusumo lunulo, lwingilile muwikaji bho bhanhu bhabhili, abho bhikalaga heke bhuli ng’wene. Uumo olatogilwe kusiminza, uungi olatogilwe gwigasha ha kaya.

Uyo olatogilwe gusiminza, agayela ugapandika milimo, umubhuyeji bhokwe bhunubho. Imilimo yiniyo, igang’wambilija gupandika ng’ombe na sabho ningi. Umunhu ng’wunuyo, agasabha noyi kunguno ya ng’ombe yakwe yiniyo, gwendelea gubyala mpaga nose, ubhiza nsabhi ntale, umuwikaji bhokwe.

Ung’wiye uyo olatogilwe gwigasha hakaya, agamala ijiliwa uyukoyiwa na nzala nhali, ahakaya yake yiniyo. Wiyangula guja gujulomba wambilijiwa ukuli ng’wiye, unsabhi ng’wunuyo.

Ahogambilijiwa bho gwinhiwa jiliwa nu ng’wiye ng’wunuyo, agadebha igiki ubhusiminzi bhuli na solobho nhale, gutinda uwigashi bho aha kaya, ubho bhugenhaga makoye ga nzala. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Kugulu kuli Ng’ombe idako ilalija.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagasusanyaga ugutumama imilimo. Umunhu ulu wigasha duhu adupandika josejose. Ulu uhaya gupandika ililazima wimile asiminze guja gujuchola. Uluuleka uguchola agulalila. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Kugulu kuli Ng’ombe idako ilalija.’ Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 62.’

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gugatumila amakanza gabho mugwigulambija gutumama milimo, kugiki bhadule gupandika jiliwa, jiswalo na bhulalo, umuwikaji bhobho.

 “Dulidakiwa dutumame milimo yise ya bhuli lushigu bho bhukamu. Unimo jiliginhu ijojigatulilagwa ikujo na gusungulilwa lubhango nu Mulungu. Ulu dulitumama milimo dulishugulika kihamo nu Mulungu umumilimo yakwe ya gubhumba. Kuyiniyo, imilimo jiliginhu ja solobho noyi umuwikaji bho bhanhu.

Giko dulidakilwa guchola jiliwa ijo jidakenakuguka, ijene hubhupanda ubho ng’wa Mulungu ubho bhugigelaga umu gunzunya Yesu Kristo.

Idinatosha, duchole hangi ijiliwa ija ng’hana ijoduling’hiwa umu Sakramenti ya Bhukaristia.” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, 62-63.

Methali 28:19.

Methali 20:13.

1Wathesalonike 4:11.

Yohane 6:27.

KISWAHILI: MGUU NI NG’OMBE TAKO NI JAA.

Methali hiyo, ilitokea kwenye maisha ya watu wawili waliokuwa na mapendelo tofauti. Mmoja alipenda kutembea, mwingine alipenda kukaa nyumbani.

Yule aliyependa kutembea alifanikiwa kupata kazi katika kutembea kwake. Kazi hiyo, ilimwezesha kupata ng’ombe na mali zingine, katika maisha yake. Kupitia ng’ombe huyo, alifanikiwa kuwa tajiri mkubwa baada ya ng’ombe kuendelea kuzaana zaidi na zaidi.

Yule aliyependa kukaa nyumbani aliishiwa chakula, akawa anasumbuliwa na tatizo la njaa kali katika familia yake. Ikabidi yeye aende kuomba msaada kwa yule tajiri, aliyependa kutembea. Baada ya kupatiwa msaada huo kwa kupewa chakula, alielewa kuwa, kumbe kupembea kunafaida ikiwemo hiyo ya kupata mafanikio hayo, kuliko kukaa nyumbani, ambako kunaleta tatizo la njaa. Ndiyo maana watu wakaanza kusema kwamba, ‘mguu ni ng’ombe, tako ni njaa.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wale ambao wanajishauri kufanya kazi. Mtu akikaa tu hatapata chochote. Akitaka kupata lazima asimame atembee kwenda kutafuta. Asipotafuta atalala akiwa na njaa. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘mguu ni ng’ombe tako ni njaa.’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 62.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao katika kujibidisha kufanya kazi zao za kila siku, ili waweze kujipatia chakula, nguo na malazi, katika maisha yao.

“Yatupasa kufanya kazi zetu za kila siku kwa bidii. Kazi ni jambo linaloheshimiwa na kubarikiwa na Mungu. Tunapofanya kazi tunashughulika na Mungu katika kazi yake ya kuumba. Kwa hiyo, kazi ni kitu cha maana sana katika maisha ya watu.

Vile vile yatupasa kutafuta chakula kisichoharibika, yaani uzima wa Mungu unaopatikana kwa kumwamini Yesu Kristo.

Isitoshe tutafute tena chakula cha kweli tunachopewa katika Sakramenti ya Ekaristi.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, 62-63.

Methali 28:19. “Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,  bali afuataye mambo ya upuzi atakuwa na  umaskini wa kumtosha.”

Methali 20:13. “Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.”

1Wathesalonike 4:11. “Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza pale awali.”

Yohane 6:27. “Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.””

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.