692. TUKOBHE SHA MBULA.

Ulusumo lunulo, lwandija kubhanhu abho bhikomelejaga guchola ja mbula. Iginhu jinijo, jili jiliwa. Uumo agang’wila ung’wiye, ‘ilikanza lya mbula lyashikaga dujage dugalime.’ Ung’wiye agashosha, ‘ng’hana dujage dugachole matwajo ga mbula, agene hi jiliwa.’

Gashigana, amatwajo aga mbula genayo, ili gutumama milimo ya gulima kugiki bhadule gwipandikila jiliwa.’ Hunagwene abhanhu bhagikomelejaga gutumama milimo ya gubhapandikila jiliwa, bho guyomba giki, ‘tukobhe sha mbula.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhatubhaga ahikanza lya gutumama milimo, guti ya gulima, guzenga numba, na yingi. Bhagamanaga bhiwila, “tukobhe sha mbula”, mumho, duchole matwajo ga mbula, nulu, dulye.

Hangi ulusumo ulu, lugatumilagwa gubhakomeleja abhanhu gutumama milimo bho bhukamu, bhalime kugiki bhapandike matwajo ga mbula, ayo gali jiliwa.

Abhanhu bhenabho, bhagabhakomelejaga abhichabho, gutumama milimo bho bhukamu bhutale gubhitila kikalile kabho. Hunagwene bhagabhawilaga abhanhu giki, ‘tukobhe sha mbula.’ Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 62.’

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gugatumila amakanza gabho mugwigulambija gutumama milimo, kugiki bhadule gupandika jiliwa, jiswalo na bhulalo, umuwikaji bhobho.

 “Dulidakiwa dutumame milimo yise ya bhuli lushigu bho bhukamu. Unimo jiliginhu ijojigatulilagwa ikujo na gusungulilwa lubhango nu Mulungu. Ulu dulitumama milimo dulishugulika kihamo nu Mulungu umumilimo yakwe ya gubhumba. Kuyiniyo, imilimo jiliginhu ja solobho noyi umuwikaji bho bhanhu.

Giko dulidakilwa guchola jiliwa ijo jidakenakuguka, ijene hubhupanda ubho ng’wa Mulungu ubho bhugigelaga umu gunzunya Yesu Kristo.

Idinatosha, duchole hangi ijiliwa ija ng’hana ijoduling’hiwa umu Sakramenti ya Bhukaristia.” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, 62-63.

Methali 28:19.

Methali 20:13.

1Wathesalonike 4:11.

Yohane 6:27.

KISWAHILI: TUTAFUTE CHA MVUA (CHAKULA).

Methali hiyo, ilianzia kwa watu waliokuwa wakihimizana kutafuta kile kinachotakana na mvua. Kitu hicho ni chakula. Mmoja alimwambia mwenzake, ‘wakati wa mvua umekalibia twende shambani tukalime.’ Mwenzake alijibu, ‘kweli twende tukatafute matunda ya mvua, yaani chakula.’

Kumbe matunda hayo, ni kufanya kazi ya kulima kwa ajili ya kujipatia chakula. Ndiyo maana watu huhimizana kufanya kazi za kuwapatia chakula, kwa kusema, ‘tutafute cha mvua.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wale ambao wanajisikia njaa wakati wa kufanya kazi kama vile kulima, kujenga nyumba n.k. Huwa wanasema “tukobe sha mbula”, yaani, tutafute matunda ya mvua au tule.

Tena methali hii hutumika kwa kuwahimiza watu wafanye kazi kwa bidii, walime ili wapate matunda ya mvua, yaani chakula. Watu hao, huwahimiza wenzao kufanya kazi zao kwa bidii, kupitia maisha yao. Ndiyo maana wao huwaambia watu kwamba, ‘tutafute cha mvua.’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 62.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao katika kujibidisha kufanya kazi ili waweze kujipatia chakula, nguo na malazi, katika maisha yao.

“Yatupasa kufanya kazi zetu za kila siku kwa bidii. Kazi ni jambo linaloheshimiwa na kubarikiwa na Mungu. Tunapofanya kazi tunashughulika na Mungu katika kazi yake ya kuumba. Kwa hiyo, kazi ni kitu cha maana sana katika maisha ya watu.

Vile vile yatupasa kutafuta chakula kisichoharibika, yaani uzima wa Mungu unaopatikana kwa kumwamini Yesu Kristo.

Isitoshe tutafute tena chakula cha kweli tunachopewa katika Sakramenti ya Ekaristi.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, 62-63.

Methali 28:19. “Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,  bali afuataye mambo ya upuzi atakuwa na  umaskini wa kumtosha.”

Methali 20:13. “Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.”

1Wathesalonike 4:11. “Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza pale awali.”

Yohane 6:27. “Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.””

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.