691. NKUNGA LYOCHI.

Nkunga lyochi, luli lusumo ulo lwandija kuli munhu uyo ojaga ulilila jiliwa aha kaya iyo obhonaga lilizuka lyochi. Uweyi oli adalimaga aha kaya yakwe, kunguno ya gumalina guja ulya aho obhonaga lilizukila ilyochi linilo. Nose, abhanhu bhagandya guyung’watana giki, ‘Nkunga Lyochi.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alingokolo ugutumama imilimo. Umunhu ng’wunuyo, atogilwe gulya jiliwa duhu bho nduhu ugujitumamila milimo ijo alijilya, kunguno ahikanza ilya gutumama milimo, uweyi agibhisaga halebhe, oyulola aho lilifumilila ilyochi.

Abhanhu bhagang’witanaga Nkunga Lyochi, bhogundalaha, kunguno ali munhu uyo agacholaga aha kaya iyo bhalizucha lyochi, odebha igiki bhalizuga jiliwa, oja hoyi gujulwa.

Uweyi ulu ubhona lyochi, agafumilaga wangu na kujulya aha kaya yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘Nkunga Lyochi.’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, 60.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka bhugokolo bho gutumama milimo, ibadala yaho, bhikomeje kuitumama chiza imilimo yao, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umukikalile kabho.

“Ubhugokolo bhudarahilwe na Bhasuguma. Hangi bhulemilwe nu Mulungu. Ubhugokolo mugutumama milimo yise iya bhuli lushugu, guti gulima, nulu, bhugokolo umumihayo ya moyo, guti, gukija gujusalila ulushigu ulo Jumapili, guleka gusalia aha kaya, guleka guntumamila Mulungu bho bhukamu, na yingi guti yiniyo, yilemilwe pye iyose.

 Hangi dudizubhiza bhanhu abho guhebhilwe na bhikumvi bho jiliwa nulu walwa. Uwikaji bhudi jiliwa duhu, bhubhitilile noyi. Bhuli munhu alina nhumbu ya gulya jiliwa. Dubhize na nzala ya gumbokela Sebha wise Yesu Kristo, umu Sakramenti ya Bhukaristia. Dubhize na nhumbu ya gulya jiliwa ja ng’wa Sebha. Dubhize na bhuyegi uludulimbokela umujigukulu jakwe. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 60-61.

Mwanzo 25:34.

Waebrania 12:16.

2Wathesalinike 3:10.

Waroma 4:17.

Methali 28:19.

KISWAHILI: MVIZIA MOSHI AU MTU MWENYE KUANGALIA (KUTAFUTA) MOSHI.

Mvizia moshi ni methali ambayo ilianzia kwa mtu aliyekuwa anakula chakula kwenye familia za watu kwa kuvizia pale unapotakea moshi. Yeye alikuwa halimi au hafanyi kazi, kwenye familia yake, kwa sababu ya kuutumia muda wake huo, katika kuvizia familia inayopika chakula, kwa kuangalia pale unatopokea moshi. Mwishowe watu, walimgundua kuwa, anavizia chakula kwa kuangalia moshi, wakaanza kumuita, ‘mvizia moshi.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mzembe katika kufanya kazi. Mtu huyo, hupenda kula tu bila kukifanyia kazi kile anachokila, kwa sababu, wakati wa kufanya kazi, yeye hujificha mahali fulani ili kungojea moshi au kuvizia moshi unapotokea.

Watu humwita mvizia moshi, kama njia ya kuonesha dharau kwake, kwa sababu ni mtu anayetafuta familia ile ambayo inatoa moshi, na kufahamu kwamba wanapika chukula pale. Mtu huyo akiona moshi mara moja hujitokeza kwenye chakula. Ndiyo maana watu humuita ‘mvizia moshi.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, 60.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha uzembe wa kufanya kazi, badaya yake, wajibidishe kuyatekeleza vizuri majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika maisha yao.

“Uzembe umedharauliwa na Wasukuma. Tena umekataliwa na Mungu kama ni uzembe katika kufanya kazi yetu ya kila siku, kwa mfano kulima, au uzembe katika mambo ya kiroho, kwa mfano kutosali Jumapili, kutosali nyumbani, kutomtumikia Mungu kwa bidii, n.k.

Tena tusiwe watu ambao tunatawaliwa na tamaa ya chakula au pombe. Maisha si chakula tu, bali ni zaidi. Kila mtu ana haja ya kula chakula. Tuwe na njaa ya kumpokea Bwana Wetu Yesu Kristo katika sakramenti ya Ekaristi. Tuwe na haja ya kula chakula cha Bwana. Tuwe na furaha tunapokuwa kwenye karamu yake.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 60-61.

Mwanzo 25:34. “Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake. Kwa hiyo Esau alidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.”

Waebrania 12:16. “Angalieni miongoni mwenu asiwepo mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja aliuza haki ya uzaliwa wake wa kwanza.”

2Wathesalinike 3:10. “Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri ili kwamba: ‘‘Mtu ye yote asiyetaka kufanya kazi, wala asile.’’”

Waroma 14:17. “Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu.”

Methali 28:19. “Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.”

smoke1

smoke2

ENGLISH: HE WHO WAITS TO SEE WHERE THE SMOKE COMES FROM.

This saying comes from someone who is fond of eating food from other people’s homes. This person does not work in his/her farm to get food but he/she just stays home looking for where the smoke comes from and follow it because he/she knows that he/she can get food. When this happened, people labeled him/her as someone who is pushed by smoke thus coming with the saying that ‘he who waits to see where the smoke comes from.’

This saying can be compared to a person who is negligent in working. This person likes eating without working out what he/she eats. When others are working in their farms he/she hides himself/herself, waiting to see where the smoke comes from. People, as a way of despising such behaviour, can call such a person as someone who looks where the smoke comes from. He/she easily associates smoke and food ‘Refer to ‘Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ ukurasa wa 60). This book was written by searchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

The proverb teaches people to stop negligence and, on the other hand, make a commitment to carry out their responsibilities so that they can achieve more in their lives.

“Negligence is discouraged by the Sukuma people. God also, through holy scriptures, discouraged negligence in, for example, gardening, or spiritual neglect; not praying on Sunday, not praying at home, not serving God diligently, etc.

And we must not be people who are ruled by a desire for food or alcohol. Life is not just food, but more than food. Everyone has a need to eat food. May we be hungry to receive Our Lord Jesus Christ in the sacrament of the Eucharist. We need to eat the Lord’s Supper. Have joy while we’re at his banquet ” (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ pages 60-61).

Genesis 25:34. Hebrews 12:16. 2Thessalonians 3:10. Romans 4:17. Proverbs 28:19.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.