690. SEKELA MIDEKO.

Sekela mideko luli lusumo ulo lulingisilile kuli munhu uyo agayegelaga aha gulya jiliwa, kulebha ugujichola. Galihoyi mahoya ga bhanhu bhabhili, uungi atogilwe ugutumama imilimo, uungi adatogilwe. Uyo atogilwe ugutumama imilimo akayomba, ‘tujage dugatumame milimo kunguno ilikanza lyashigaga.’ Uyo adayitogilwe imilimo agashosha bhobhuzongu aliyomba, ‘naduduja ugujutumama imilimo, kunguno naliigwa shibhi.’

Uyo aitogilwe imilimo agang’wila, ‘bhasi, dujage gugalwe jiliwa kugiki umili goko gupandike nguzu chiza.’ Uweyi agashosha kubhuyegi ukunu alimila, ‘nahene dujage.’ Hunagwene abhanhu bhagandya guyung’witana giki, ‘sekela mideko.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alingokolo umugutumama imilimo. Umunhu ng’wunuyo, atogilwe gulya jiliwa duhu bho nduhu ugujitumamila milimo ijo alijilya. Abhanhu bhagang’witanaga sekala mideko bhogundalaha, kunguno ali munhu uyo agasekaga ahikanza lya gulya jiliwa, aliyo ahikanza ilya gutumama milimo, agasunduhalaga. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, ‘sekela mideko.’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, 60.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka bhugokolo bho gutumama milimo, ibadala yaho, bhikomeje kuitumama chiza imilimo yao, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.

“Ubhugokolo bhudarahilwe na Bhasuguma. Hangi bhulemilwe nu Mulungu. Ulu bhugokolo mugutumama milimo yise iya bhuli lushugu, guti gulima, nulu, bhugokolo umumihayo ya moyo, guti, gukija gujusalila ulushigu ulo Jumapili, guleka gusalia aha kaya, guleka guntumamila Mulungu bho bhukamu, na yingi guti yiniyo, yilemilwe pye iyose.

 Hangi dudizubhiza bhanhu abho guhebhilwe na bhikumvi bho jiliwa nulu walwa. Uwikaji bhudi jiliwa duhu, bhubhitilile noyi. Bhuli munhu alina nhumbu ya gulya jiliwa. Dubhize na nzala ya gumbokela Sebha wise Yesu Kristo, umu Sakramenti ya Bhukaristia. Dubhize na nhumbu ya gulya jiliwa ja ng’wa Sebha. Dubhize na bhuyegi uludulimbokela umujigukulu jakwe. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 60-61.

Mwanzo 25:34.

Waebrania 12:16.

2Wathesalinike 3:10.

Waroma 4:17.

Methali 28:19.

KISWAHILI: MCHEKEA CHAKULA.

Mchekea chakula ni methali ambayo humaanisha mtu anayefurahia kula chakula, kuliko kukitafuta. Kulikuwa na maongezi ya watu wawili, mmoja anapenda kufanya kazi mwingine hapendi. Anayependa kufanya kazi alisema, ‘twende tukafanye kazi kwa sababu wakati umefika.’ Asiyependa kufanya kazi, alijibu kwa unyonge akisema, ‘siwezi kwenda kufanya kazi kwa sababu najisikia vibaya.’

Mpenda kazi akamwambia, ‘basi twende tukale chakula ili mwili wako upate nguvu vizuri.’ Yeye alijiku kwa furaha huku akiwa amesimama, ‘sawa twende.’ Ndiyo maana watu wakaanza kumuita, ‘mchekea chakula.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mzembe katika kufanya kazi. Yeye anapenda kula tu bila kukifanyia kazi kile anachokila. Watu humwita mchekea chakula kama njia ya kuonesha dharau kwake, kwa sababu ni mtu anayecheka wakati wa kula, lakini wakati wa kazi husikitika. Ndiyo maana watu humuita ‘Mchekea chakula.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, 60.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha uzembe wa kufanya kazi, badala yake, waongeze bidii ya kuyatekeleza vizuri majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

“Uzembe umedharauliwa na Wasukuma. Tena umekataliwa na Mungu kama ni uzembe katika kufanya kazi yetu ya kila siku, kwa mfano kulima, au uzembe katika mambo ya kiroho, kwa mfano kutosali Jumapili, kutosali nyumbani, kutomtumikia Mungu kwa bidii, n.k.

Tena tusiwe watu ambao tunatawaliwa na tamaa ya chakula au pombe. Maisha si chakula tu, bali ni zaidi. Kila mtu ana haja ya kula chakula. Tuwe na njaa ya kumpokea Bwana Wetu Yesu Kristo katika sakramenti ya Ekaristi. Tuwe na haja ya kula chakula cha Bwana. Tuwe na furaha tunapokuwa kwenye karamu yake.” Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 60-61.

Mwanzo 25:34. “Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake. Kwa hiyo Esau alidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.”

Waebrania 12:16. “Angalieni miongoni mwenu asiwepo mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja aliuza haki ya uzaliwa wake wa kwanza.”

2Wathesalinike 3:10. “Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri ili kwamba: ‘‘Mtu ye yote asiyetaka kufanya kazi, wala asile.’’”

Waroma 14:17. “Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu.”

Methali 28:19. “Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.”

laugh

laugh children

ENGLISH: LAUGHING FOR FOOD.

This saying comes from someone who enjoys eating food rather working for it. One day, two people were in conversation, one of them was fond of working while the other one not. In the course of conversation one of them said ‘Let’s go to work because the time has come.’ The other fellow who doesn’t like to work replied saying ‘I can’t go to work because I feel bad.’ The one who likes to work, later, told his/her fellow workmate that ‘let’s go eat some food so that your body can be healthy.’ The statement on going to eat was received with the greatest joy, ‘let’s go.’

This saying can be compared to a person who doesn’t like working. This person likes to eat without working for what he/she eats. People can ridicule him/her as someone who laughs whenever he/she sees food but feels bad whenever the question of working is mentioned (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 60). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

The saying teaches people to stop negligence and, instead, increase the effort to carry out their responsibilities so that they can achieve more in their lives.

The Sukuma people tend to hate negligence. God also hates negligence manifested in, for example, not farming, not praying, not attending Sunday church services, not diligently serving God, etc. We must not be people who are ruled by a desire for food or alcohol. Life is not just food, but more than food. Everyone has a need to eat food. May we be hungry to receive Our Lord Jesus Christ in the sacrament of the Eucharist. We need to eat the Lord’s Supper. Have joy while we’re at his banquet (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 60-61).

Genesis 25:34. Hebrews 12:16. 2Thessalonians 3:10. Romans 4:17. Proverbs 28:19.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.