698. AHO UKADAHILAGA NA HAHO BUNYELO.

Ikale olihoyi munhu uyo olimulugendo lo guja halebhe. Aliyo lulu, umunhu ng’wunuyo, agakolwa nota noyi. Ukubahati ya wiza, agashiga mumongo umo agadula gukumba lyinzi ung’wa aminzi mpaga ufula inota yakwe.

Oho omala ugung’wa aminzi gaha lyinzi lunulo, aganyela mumo lyinzi  lunulo, ulo odahilaga aminzi genayo, adizukaga igiki alakolwa nota hangi wiza gung’wa minzi hoyi.  Hunagwene abhanhu bhagandya guyung’wila giki, ‘aho ukadahilaga na haho bhunyelo.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo okaribhushiyagwa chiza ha kaya ya ng’wa munhu. Ubhegejiyawa chiza guti ndugu ohakaya yiniyo, bhuyulya kihamo na gwendelea.

Aha ngelelo yaho, umunhu ng’wunuyo, ushiya nu mayu uoha kaya yiniyo, nulu, wibha ginhu hoyi, nulu wita jito jose jose ijo jidijawiza.’ Ugubhilitia ya bhubhi abhanhu bhenabho, yikolile na gunyela oho agadahilaga minzi, umunhu ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, ‘aho ukadahilaga na haho bhunyelo.’ Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 70.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhulumbi ukubhanhu abho bhalibhitila ya wiza, bho kuleka ugubhitila iyabhubhi, kugiki bhadule gwendelea gwiyambilija chiza, umuwikaj bhobho.

“Abhanhu abho dugabhitililaga yabhubhi bhali bhanhu abho dugikalaga kihamo nabho. Dugemele: ugushiya nu nkima o nzenganwa, gung’wibhila nwani, na gwendelea.

Hangi iyiniyo yili jigemelo ukubhumani wise nu Yesu Kristo uyo agadubokelaga kuwizang’holo na gwifunya gete kubhise guti nwani. Ningiki odutogwa, bho miito gise mabhi duganhemaga na gundalaha.

Hangi umusakramenti ya Ekaristia tugadumaga ugunkuja kunguno dugalyaga mili gokwe na gung’wa mininga gakwe bho nduhu ugwigelelwa. Lolaga kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 71.

Zaburi 55:12-14.

Mathayo 26:49-50.

Yohone 13:21, 25-26.

1Wakorintho 11:27.

UCHOTEAPO NDIPO UNAPONYEA.

Zamani alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa katika safari yake ya kwenda sehemu fulani. Lakini basi mtu huyo, alijisikia kiu kali sana. Kwa bahati nzuri, alifika mtoni ambamo alifaulu kuchimba kisima akanywa maji mpaka akakidhi kiu yake.

Alipomaliza kunywa maji ya kwenye kisima hicho, alinyea kwenye kisima hicho alimoyachotea maji hayo, bila kukumbuka kwamba atajisikia kiu tena na kurudi pale kung’wa maji. Ndiyo maana watu wakaanza kumwambia kwamba, ‘uchoteapo ndipo unaponyea.’

Methali hiyo hulinganisha kwa mtu yule ambaye amekaribishwa vizuri kwenye nyumba ya mtu. Akatendewa vizuri kama mmoja wa jamaa, wakila pamoja na kadhalika.

Mwishowe mtu huyo, huzini na mama wa kaya hiyo, au huiba au hutenda kitendo chote chote, ambacho si kizuri. Kuwafanyia ubaya watu hao, hufanana na kunyea pale achoteapo maji mtu huyo. Ndiyo maana watu humwambia mtu huyo, kwamba ‘uchoteapo ndipo unaponyea.’. Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 70.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na shukrani kwa watu wanaowatendea mema kwa kuacha kuwatendea mabaya, ili waweze kuendelea kusaidiana vizuri, katika maisha yao.

“Watu ambao tunawatendea mabaya ni watu (wale) ambao tunaokaa pamoja nao. Kwa mfano: Kuzini na bibi wa jirani, kumwibia rafiki, na kadhalika.

Tena hii ni mifano kwa uhusinano wetu na Yesu Kristo anayetupokea kwa ukarimu na kujitoa kwetu kabisa kama rafiki. Ijapokuwa ametupenda, kwa matendo yetu mabaya, huwa tunamkataa na kumdharau.

Tena katika sakramenti ya Ekaristi huwa tunashindwa kumheshimu kwa sababu tunakula mwili wake na kunywa damu yake bila kustahili.” Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 71.

Zaburi 55:12-14. “Kama aliyenitukana ni adui yangu ningevumilia, kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, ningejificha asinione. Kumbe ni wewe, mwenzangu, mshiriki na rafiki yangu wa karibu, ambaye wakati fulani tulifurahia ushirika mzuri tulipokuwa tukienda katikati ya umati hekaluni mwa Mungu.”

Mathayo 26:49-50. “Mara akamjia Yesu na kumsalimu, “Salaam, Rabi!’’ Akambusu. Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya kile ulichokuja kufanya hapa.”

Yohane 13:21, 25-26. “Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, ‘‘Amin, amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.’’ Yule mwanafunzi akiwa amemwegemea Yesu akamwuliza, ‘‘Bwana tuambie ni nani?’’   Yesu akajibu, ‘‘Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.’’ Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.”

1Wakorintho 11:27. “Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana.”

drinking water

water-fetchers.1

water-fetchers

 

ENGLISH: YOU DEFACATE WHERE YOU FETCH WATER FROM.

Once upon a time ago, there was a man who was travelling to a certain place. This man reached a point when he was feeling thirsty. To quinch his thirsty, he went to a waterlogged place and dag a small hole where he can get water to drink. When he drank water to his satisfaction, he never thought of wanting water again. He defecated in the water and left. This is where the saying ‘you defacate where you fetch water from’ came from.

This saying can be compared to a person who is well received by his/her host but, instead of appreciating him/her for the kindness, he/she turns around abusing him/her. The abuse can be like committing adultery with the wife/husband of the host, stealing some of the host’s properties, etc. (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 70). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.

This saying teaches people to be thankful to people who do good to them. People should stop doing evils in order to have good life and good relationship with others.

The people we are abusing are the people we are living with. For example, committing adultery with a neighbor’s wife, robbing a friend, and so on.

Again these are examples of our association with Jesus Christ, who graciously accepts us and gives Himself completely as a friend. Although He loves us, by our evil deeds, we often reject and despise Him.

And in the sacrament of the Eucharist we often fail to honor Him because we eat His flesh and drink His blood unworthily (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 71).

Psalm 55: 12-14. Matthew 26: 49-50. John 13:21, 25-26. 1 Corinthians 11:27.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.