699. BUGALI WA HENAHA WA KUGULA IDAKO.

Yalihoyi kaya imo ya bhanhu bhabhili, ngosha na nkima. Ungosha wipunaga guja gungunda gujulima,  oneka unkima alizuga jiliwa ja guchala ukumilimo yabho, kugiki bhagalye kihamo. Aliyo lulu, unkima ng’wunuyo, okelejaga noyi bhuli lushiku uguchala ijiliwa jinijo.

Lushigu lumo, ungoshi agang’wila unke okwe, ‘intondo dugwipuna pye abhose dugalime mpaga ikanza ilebhe, hunadugushoka kaya gwiza gulya jiliwa. Unke okwe ashosha, ‘nahene dugwipuna dugalime ulu dushoka nagwiza nazuge ijiliwa dulya.’

Aho wela ubhujiku, bhagipuna diyu bhugalima mpaga lyushika ikanza ilebhe bhushoka kaya gwiza gulya jiliwa. Ungosha ung’wila unke, ‘zugaga lulu ijiliwa dulye.’ Unke ushosha, ‘nahene nazuge.’

Unkima ng’wunuyo, agandya guzuga hado hado nose ungosha, unoga ugwigasha. Umuja, ‘umukaya  ng’wabisha ijiliwa?’ Unke okwe ushosha, ‘degelaga.’ Ungosha agankomeleja, ‘kangilijaji uguzuga, nose gayusada amadako ugwishasha.’

Oganoga unke okwe obhisha ijiliwa na gujitenga, unkabhulisha ungoshi, ‘karibhu lulu dabisha ijiiwa.’ Ungoshi wiza ugulya aliyomba, ‘bugali wa henaha wa gugula idako.’ Ubhunubho huwandijo bho gutumimalwa go lusumo lunulo.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli ngosha nulu ng’wimeji ulu nke okwe alikeleja gubisha jiliwa kunguno ya bhugokolo, nulu bhugulu bhokwe. Ugugula idako  yili guyomba: Ulilipa bho wiyumilija bho madako kunguyo ya gulindila jiliwa kuli kanza lilifu. Udulipaga hela aliyo ulilipa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘bugali wa henaha wa kugula idako.’ Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 72.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhukamu bhutale ubho gubhambilija uguitumama chiza imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

“Dulidakilwa gutumama milimo ku bhukamu bhuli ikanza ilo dulibhatumamila abhigusu nulu ulu dulintumamila Sebha. UMulungu adatogishiyagwa nu munhu uyo agantumimalaga bho nduhu bhukamu nulu moyo go gutogwa.

Dudizubhiza  hagatigati umuguntumamila Sebha, aliyo dubhize moto, giki, duntogwe ku moyo gwise gose, masala gise gose, na nguzu jise jose. Hangi dulidakilwa gubhatumamila abhigisu bho bhukamu na moyo go bhutogwa gitumo agitila UYesu Kristo ng’winikili.” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 72.

Wakolosai 3:23-24.

Ufunuo 3:16.

Waebrania 6:12.

Waroma 12:11.

KISWAHILI: UGALI WA HAPA NI WA KUNUNUA TAKO.

Ilikuwepo familia moja yenye watu wawili, mme na mke. Mwanamume alikuwa alijilawa asubuhi na mapema kwenda kulima shambani, alimuacha mke wake akipika chakula cha kupeleka shambani ili wakale huko kwa pamoja. Lakini basi, mwanamke huyo, alikuwa akichelewa sana kila siku kupeleka chakula hicho.

Siku moja, mwanamume alimwambia mke wake, ‘kesho tutaamuka mapema wote twende shambani tukalime mpaka wakati fulani ndipo tutarudi nyumbani kuja kula chakula.’ Mke wake akajibu, ‘sawa tutaamuka mapema asubuhi tukalime tukirudi nitakuja kupika chakula tule.’

Kesho yake waliamuka asubuhi kwenda shambani kulima mpaka ukafika wakati fulani, wakarudi nyumbani kula chakula. Mwanamume alimwambia mke wake, ‘pika basi chakula tule.’ Mke wake akajibu, ‘sawa napika.’

Mwanamke huyo, alianza kupika pole pole, mwishowe mume wake, akashoka kukaa. Akamuuliza, ‘humo ndani mmeivisha chakula?’ Mke wake akajibu, ‘tumekaribia.’ Mume wake akamhimiza, ‘fanyeni haraka, mwishowe matako yameanza kuuma kukaa.’

Mwishowe mke wake aliivisha chakula, akakipeleka mezani na kumkaribisha mumewe akisema, ‘karibu basi tumeivisha chakula.’ Mume wake alinuka kwenda kula chakula mezani akisema, ‘ugali wa hapa ni wa kunulua tako.’ Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kutumika kwa methali hiyo.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa bwana au mtani ikiwa mke wake anachelewa kuivisha chakula kwa sababu ya uvivu au ujeuri wake. Kununua tako ni kusema: Unalipa kwa maumivu ya matako kwa sababu ya kusubiri chakula kwa muda mrefu. Hulipi pesa lakini unalipa. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘ugali wa hapa ni wa kunulua tako.’ Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 72.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methail hiyo, hufundisha watu juu ya kuyatekeleza majukumu yao kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi katika maisha yao.

“Yatupasa kufanya kazi kwa bidii kila tunapowatumikia wenzetu au tunapomtukika Bwana. Mungu hapendezwi na mtu anayemtumikia bila bidii au moyo wa kupenda. Tusiwe vuguvugu katika kumtumikia Bwana, bali tuwe moto, yaani tumpende kwa moyo wetu wote, akili zetu zote na nguvu zetu zote. Tena yatupasa kuwatumikia wenzetu kwa bidii na moyo wa upendo kama alivyofanya Yesu Kristo mwenyewe.’ Rejea Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 72.

Wakolosai 3:23-24. “Lo lote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana na si wanadamu. Kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana kuwa thawabu yenu”

Ufunuo 3:16. “Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani Mwangu.”

Waebrania 6:11-12. “Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi.”

Waroma 12:11. “Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.”

ghana1

ghana child-

food1

 

ENGLISH: UGALI IN THIS HOUSE IS BOUGHT THROUGH YOUR BUTTOCKS.

There was one family with two people, husband and wife. The man would wake up very early in the morning going to the farm. And the woman could delay a bit because she has to cook some meal and carry it with her to the farm and eat with her husband. But this woman used to be late everyday to bring food for the man.

One day the man told his wife that all of them have to leave home very early in the morning without carrying food and that, food will be eaten when they come back from the farm. The wife agreed with the man and left for the farm. When they came back from the farm, the woman went to the kitchen and spent a lot of hours cooking the food until the man became tired of waiting for food. The man kept on asking for food and the woman could reply, wait; it will be done soon.

The man waited until his buttocks began to pain for too much sitting. When the food was ready, the man was invited to eat and he said ‘ugali in this house is bought through your buttocks.’ This marked the beginning of this saying.

This saying can be compared to a person who is lazy or cruel in his/her life. Such a person will not help others easily during distress times. People of this nature will enjoy seeing others suffer (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 72). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., published by Benedictine Publications Ndanda – Peramiho, 1984.

This saying teaches people how to carry out their tasks with great effort so that they can achieve more success in their lives.

We must work hard every time we serve our fellowmen or when we serve the Lord. God is displeased with someone who serves Him with little effort. Let us not be slothful in serving the Lord, but zelous, loving Him with all our heart, mind, and strength. We must serve our fellow men with as much zeal and love as Jesus Christ Himself (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 72).

Colossians 3: 23-24. Revelation 3:16. Hebrews 6:12. Romans 12:11.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.