Ulusumo lunulo, lwingilile ku mahoya ga bhageni na bhanikili kaya yiniyo. Uumo o bhanikili kaya agabhasumbila abhageni aliyomba, ‘makaribhu ng’wigashe mumasumbi.’ Uweyi agashosha, ‘umunhu adadulile gwigasha hisumbi ulu adina bhisagilwa bho gupandika jiliwa.’ Nang’hwe agashosha, ‘guli gonghana ubho nduhu jiliwa umu nda, ugwikala hoyi idinasolobho.’ Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba giki, ‘isumbi lili mu nda.’
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo na wisagilwa bho gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhokwe. Umunhu adadulile gwita nimo uyo gudina solobho.
Isolobho yiniyo, bhuli wisagilwa ng’wa munhu uyo alizunya gwigasha hisumbi kunguno ya kumana igiki agupandikia jiliwa. Giko lulu, umunhu ulu ugaiwa ijiliwa, ihingi, agingaga haho na haho, kunguno adalazunya ugwigasha bho nduhu gulya aho kaya yiniyo. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ubhukurasa 40.
Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Umunhu ng’wunuyo agatumamaga milimo yakwe bho bhukamu ubho bhudulile gumpandikila matwajo mingi, umuwikaji bhokwe, ayo gagikolanijiyagwa na jiliwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘isumbi lili mu nda.’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kubhiza na wizagilwa bho gubhambilija ijinagongeja bhukamu bho gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.
Ijina moyo, dulidakilwa gwikala wikaji bho nyazunya aise bhazunya bha ng’wa Yesu Kristo, na gunondela weyi, bho gubhiza na bhisagilwa bhutale giki dulapandika bhupanga ubho bhudashilaga.
Ulu dubhiza dudina wisagilwa bho gupandika bhupanga ubho bhudashilaga, munho ugunondela gwise UYesu Kristo, gugubhiza gudina solobho, nulu nimo go bhule duhu. Kuti numo Untume Paulo aliyombela, ‘ulu Yesu Kristo adajukile, uguzunya gwise guli bhule.’
Ulu munhu agazunya gwiyumilija gwikala hizumbi, bho gwigasha ahisumbi linilo, ali na wisagiji bho gupandika jiliwa, nayise bhazunya igelelilwe gwiyumilija, guja kwikelesia, bhuli lushugu ulo Mfungo, kunguno dumanile igiki dugulwa Jiliwa na Sebha, na gulangwa Mhayo go ng’wa Mulungu, uyo gugailishaga imioyo yise.
Aliyo uwiza bho jizunya, (guti bhutumami ukubhangi, bhugubhiza bhulihoyi bhuying’wene, na bhutumami bho nduhu gulindila gulipwa) bhuli na solobho nhale gukila ulusumo ulo Jisuguma. Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa bho 40-41,
Yohane 6: 26-27.
Luka 2:25-32.
Marko 10:29-30.
2Timotheo 4:6-8.
KISWAHILI: KITI KIMO TUMBONI.
Methali hiyo ilianzia kwenye maongozi ya watu wageni na wanafamilia. Mmoja ya wanafamilia aliwakaribisha wageni akisema, ‘karibuni mketi kwenye kiti.’ Mmoja wa wageni alijibu, ‘mtu hawezi kuketi kitini isipokuwa ana tumaini la kupata chakula.’ Yeye akajibu, ‘ni kweli kiti bila chakula kwenye tumbo hakina maana.’ Ndiyo maana watu wakaanza kusema kwamba, ‘kiti kimo tumboni.’
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu anayefanya kazi kwa kutumaini kupata mafanikio mengi kwenye kazi yake hiyo. Mtu hawezi kufanya kazi bila kuwa na faida. Faida hiyo ni kama matumaini ya mtu anayekubali kuketi kwenye kiti kwa sababu ya kuelewa kwamba atapata chakula.
Hivyo mtu akikosa chakula huondoka mara moja kwa sababu hatakubali kukaa bila kula kwenye familia hiyo. Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 40.
Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.
Mtu huyo hufanya kazi zake kwa bidii ya kumwezesha kupata mafanikio yanayofananishwa na chakula. Ndiyo maana watu husemwa kwamba, ‘kiti kimo tumboni.’
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na matumaini ya kumwezesha kuongeza bidii katika kuyatekeleza vizuri majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio ya kutosha kuyandesha vizuri maisha yao.
Kiroho, tunahitaji kuishi maisha ya Kikristo na kumfuata Yesu Kristo, kwa kuwa tuna tumaini la kwamba tutatunukiwa uzima wa milele. Ikiwa hatuna tumaini la kuupata uzima huo wa milele, kumfuata Yesu Kristo hakuna maana, au ni kazi bure tu. Kama Mtakatifu Paulo aliyosema, “ikiwa Yesu Kristo hakufufuka imani yetu ni bure.”
Kama mtu aliyekubali kuvumilia kukaa kitini kuwa ana tumaini la kupata chakula, ndiyo sisi waamini yatupata kuvumilia kwenda Kanisani kila Jumapili kwa sababu tuna hakika kwamba tutakula chakula cha Bwana, na kufundishwa Neno la Mungu linalotulisha mioyo yetu.
Lakini ubora wa ukristo (kama huduma kwa wengine, kutakuwa na ubinafsi na huduma bila kutumaini malipo) unaleta maana kubwa zaidi kuliko methali hii ya Kisukuma. Rejea Kueneza Injili Kwa Methali, ukurasa 40-41.
Yohane 6: 26-27. “Yesu akawajibu, “Amini, amini nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.’”
Luka 2:25-32. “Basi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Roho Mtakatifu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Kristo wa Bwana.
Simeoni akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu, alikwenda hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Sheria, ndipo Simeoni akampokea mtoto mikononi mwake na kumsifu Mungu, akisema: “Bwana Mungu Mwenyezi, maana macho yangu yameuona wokovu Wako, ulioweka tayari machoni pa watu wote, nuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu Mataifa na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.””
Marko 10:29-30. “Yesu akasema, “Amini, nawaambia, hakuna mtu ye yote aliyeacha nyumba, ndugu waume, au ndugu wake, mama, baba, watoto au mashamba kwa ajili Yangu na kwa ajili ya Injili, ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu, nyumba, ndugu waume, ndugu wake, mama, baba, watoto, mashamba pamoja na mateso kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”
2Timotheo 4:6-8. “Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya kuondoka imetimia. Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimelinda. Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile, wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kuja Kwake.”
ENGLISH: A SEAT WITHOUT FOOD IS NOTHING.
This saying comes from the conversation between visitors and the host family. One of the family members welcomed the guests saying, ‘welcome and have a seat’ then the visitor replied saying that ‘a seat without food is nothing.’
The saying can be compared to a person who works with hopes to gain something in his/her work. One cannot work without knowing how much will he/she going to benefit from that work. That benefit is like the prospects that can make someone agree to sit on a chair. When a visitor doesn’t see any sign of getting food, he/she can leave the house (Refer to Kueneza Injili kwa Methali which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 40.) This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Publications, Ndanda – Peramiho, 1984.
People can work hard in order to achieve food-related successes.
This saying teaches people about how to increase their efficiency in performing their tasks. This can make them to be successful in their lives.
Spiritually, we need to live the Christian life and follow Jesus Christ, for we have the hope of being blessed with eternal life. If we have no hope of attaining that eternal life, following Jesus Christ is useless, or even futile. As St. Paul puts it, “if Jesus Christ had not risen, our faith would be in vain.”
As someone who has agreed to stay in the chair having the hope of finding food, then we believers have endured going to church every Sunday because we are confident that we will eat the Lord’s Supper, and be taught the Word of God that warms our hearts.
But the quality of Christianity (as a service to others, it is special because it is a service without hope of reward) makes much more sense than this Sukuma proverb (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 40-41)
John 6: 26-27. Luke 2: 25-32. Mark 10: 29-30. 2Timothy 4: 6-8.