680. DESHI AKALEKA JULALA.

Deshi lili lina na noni iyo ikagalyaga miswa ijo jigitanagwa kidetemela mbula. Lushigu lumo, uDeshi agaja aha jigulu aha tuzengile utujidetemela mbula tunuto.

Aho oshika hoyi, agajibhona jilifuma imoimo umulipundu. Bhuli yene iyo yafumaga, UDeshi uyitulaga munomo. Agendelea gwita giko ku likanza lilihu. Iki imiswa jigendelea gufuma duhu kulikanza lilihu, UDeshi agiguta na guduma ugujimila, nose imiswa jigaikindika gung’wiyungulila na gubhita umumiso gakwe.

UDeshi agandya guhaya, “ingaji, nose muliningilila mumiso.” Agashoka na gujileka jilifuma. Hunagwene abhanhu bhagandya guyuyomba ulu bhalya jiliwa bhiguta na gujileka, giki, ‘Deshi agaleka julala.’

Intondo yahoo, UDeshi agaja hangi, mujigulu atubhile na ukunhu alimba. “itagi kiti igolo, itagi kiti igolo.” Ahikanza lya mhindi agimbaga giki, “Mukutudisha, mukutudisha.” Lolaga Kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 38.

Ijitabho jinijo jigandikwa na bhakengeji bha: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na guchapishiwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagalyaga jiliwa mpaga bhiguta na guleka, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, ulu bhalya mpaka bhiguta, bhagaluyombaga ulusumo lunulo guti nzila ya goyela gujilya ijijiwa jinijo, iki bhajidumaga ugujimala, giki, ‘Deshi agaleka julala.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na jipimilo ja gwiyangula gujileka ijojabhalemelaga. Hangi, lobhalanga abhanhu bhenabho, gubhiza na wizang’holo bho gubhakaribhusha abhageni na gubhalila bho gubhinha jiliwa, kugiki abhanhu bhenabho, bhadule gulya na kupandika nguzu ja gwikomeja guminza chiza, umulugendo lobho.

Igelelilwe gubhitila yawiza abhigisu. Bhuli ikanza ilo dulibhitila ya wiza abhigizu, dugung’witilaga Yesu Kristo iya wiza yiniyo. UYesu obhitilaga yawiza abhanhu, umuwikaji bhokwe.

Ijinagongeja, ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya Ng’wa Yesu uyo agabhalishaga jiliwa, ijo jili mili na mininga gakwe, umu Isakramenti lya Ekaristi Nhagatifu.

Undimi untengeke agabhalishaga abhanhu jiliwa, bho gubhalanga Mhayo go Mulungu, uyo gugabhinhaga bhupanga. UYesu Kristo, hung’wene uyo ali ‘ha ng’wa Lutubhila gule.’ Ukwene huguhaya giki, ahali Uweyi bhagatubhilaga kule. Uyo agajaga kuli Weyi adubhona inzala. Uyo alinzunya Weyi, adiigwa inota gete. Rejea Kueneza Injili kwa Methali, bhukurasa 39.

Isaya 25:6.

Ezekekieli 34: 1-2.

Marko 6:41-44.

Yohane 10:9-10.

Yakoko 2:15-17.

Luka 10:30-37.

Mathayo 25:31-46.

KISWAHILI: DESHI ALIAKA KUMBIKUMBI WAKARUKA.

Deshi ni jina la ndege ambaye hula jamii ya kumbikumbi wadogo (kidetemela mbula). Siku moja Deshi alikwenda kwenye kuchuguu (nyumba ya kidetemela mbula).

Alipofika hapo, alikuta kumbikumbi wanatoka mmoja mmoja shimoni. Kila kilichotoka Deshi alikiweka mdomoni. Akaendelea kufanya hivi kwa muda mrefu. Kwa vile waliendelea kutoka tu kwa muda mrefu, Deshi alishiba na kushindwa kuwameza, hata wakawa wanaruka kumzunguka na kupita machoni pake.

Deshi alianza kusema, ‘Ondokeni, mwishowe mtaniingia machoni.” Alirudi na kuwaacha kumbikumbi hao, wanatoka. Ndiyo maana watu wakaanza kusema wanaposhiba chakula na kukiacha, kwamba, ‘Deshi aliacha kumbikumbi wakaruka.”

Kesho yake, Deshi alikwenda tena kwenye kichuguu akiwa na njaa akiimba. “itagi kiti igolo, itagi kiti igolo” (fanyeni kama jana, fanyeni kama jana”). Wakati wa jioni huwa anaimba hivi, “Mukutudisha, mukutudisha” (mtatuingia machoni, mtatuingia machoni”). Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 38.

Kitabu hicho, kiliandikwa na watafiti ambao ni: Padri Donald Sybertz, M.M., na Padri Joseph Healey M.M., na kuchapishwa na Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu waliokula chakula mpaga wakashiba na kusaza, katika maisha yao. Watu hao, wanapokula mpaka kutosheka, huisema methali hiyo kama njia ya kuacha kula chakula, kwa vile wameshindwa kukimaliza, kwamba, ‘Deshi aliacha kumbikumbi wakaruka.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuwa na kiasi katika maisha, kwa maana ya kuamua kuacha kula chakula, baada ya kutosheka. Pia huwafundisha watu hao, kuwa na ukarimu wa kuwakaribisha wageni na kuwaandalia chakula, ili wageni hao waweze kula na kupata nguzu za kuwawezesha kuendelea vizuri na safari yao.

Yatupata kuwatendea wenzetu mema. Kila tunapomtendea mwenzetu mema tunamtendea mema Yesu Kristo. Kila tunapokosa kumtendea mwenzetu mema, tunakosa kumtendea Yesu Kristo mema hayo. Yesu alikuwa mtu aliyetenda wema kwa wengine.

Zaidi ya hayo, methali hiyo, yatufundisha juu ya Yesu Kristo anayetulisha na kutushibisha chakula, yaani mwili na damu yake katika Sakramenti ya Ekaristi Takatifu.

Mchungaji mwema huwalisha watu chakula, yaani huwafundisha neno la Mungu linalowapatia watu wokovu. Yesu Kristo ndiye “lutubhila kule,” yaani kwake njaa iko mbali. Anayekwenda kwake hataona njaa. Anayemwamini Yeye hataona kiu kamwe. Rejea kueneza Injili kwa Methali, ukurasa 39.

Isaya 25:6. “Na katika mlima huu Bwana wa Majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.”

Ezekekieli 34: 1-2. “Neno la Bwana likanijia kusema, mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam hao wachungaji Bwana Mungu asema hivi, ole wao wachungaji wa Israeli wanaojilisha wenyewe. Je, wachungaji kuwalisha kondoo?”

Marko 6:41-44. “Kisha Yesu akatwa ile mikate mitano na wale sakaki wawili akatazama juu mbinguni akamshukuru Mungu, akaimeja mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu na wale samaki wawili pia. Akawagawia wote, watu wote wakala wakashiba wakaokota mabaki ya mikate na samaki pia, wakaja vikapu kumi na viwili.”

Yohane 10:9-10. “Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na atapata malisho.”

Yakoko 2:15-17. “Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula. Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: Nendeni salama, mkaote moto na kushiba bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?”

Luka 10:30-37. “Mfano wa Msamalia Mwema.”

Mathayo 25:31-46. “Hukumu ya Mwisho.”

bird eating insects

ants1

ants

 

ENGLISH: DESHI LEFT THEM TO FLY.

Deshi is the name of a bird that feeds on flying ants. One day deshi went to the anthill where flying ants live. When it got there, it found that the flying ants were coming out of their hole. What deshi did is setting its mouth closer to the entry of the hole so that the flying ants can enter straight into deshi’s mouth. It ate the flying ants to its satisfaction. Later on, because of satisfaction, the flying ants began flying around to surround deshi and, at this time, deshi had no any appetite to continue eating them. When the flying ants were doing so, deshi told them: “Get out, and finally you will enter our eyes.” He went back and left them, and they left to their hole. That is why people, when have eaten to their satisfaction, say “deshi left them to fly.”

The next day, deshi went back to the anthill while singing: “Itagi giti igolo, itagi git igolo” (do as you did yesterday, do as you did yesterday ). While the day before, it was singing “you will enter our eyes, you will enter our eyes” (Refer to Kueneza Injili kwa Methali’ which means ‘Spreading the Gospel through Proverbs,’ page 38). This book was written by researchers: Fr. Donald Sybertz, M.M., and Fr. Joseph Healey M.M., and published by Benedictine Pubhications Ndanda – Peramiho, 1984.

This proverb can be compared to greedy people who will tend to eat food to their satisfaction and later on begin to abuse it.

The proverb also teaches people to do good to fellows. Whenever we do good to one another, we do good to Jesus Christ. Whenever we fail to do good to one another, we fail to do good to Jesus Christ. Jesus was a man who did good to others.

Further, the proverb teaches us about Jesus Christ who nourishes and satisfies us with food, that is, his flesh and blood in the Sacrament of the Holy Eucharist.

The good shepherd feeds the people, that is, teaches them the word of God for salvation. In Jesus Christ hunger is far away. Whoever goes to Him will not be hungry. He who believes in Him will never feel thirsty (Refer to ‘Spreading the Gospel in Proverbs,’ page 39).

Isaiah 25: 6. Ezekiel 34: 1-2. Mark 6: 41-44. John 10: 9-10. James 2: 15-17. Luke 10: 30-37. Matthew 25: 31-46.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.