Imbuki ya lusumo lunulo, ilolile wibhembu bho mva iyo igang’waga magi. Imva yiniyo, igibhelejaga bho gwiyolecha giki iliya wiza ukuli nsugi oyo, kugiki akije uguibadija igiki igang’waga maji. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘mva nyibheleja huna ng’wi ya magi.’
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ng´wibhembu, aliyo ubho mgati adi o wiza, aling´wibheleja duhu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agiyolechaga ukubhanhu giki ali ntengeke, aliyo gashinaga alinkenaguji, umugati yakwe. Uweyi agikalaga bho gwibheleja duhu, kugiki abhanhu bhakije ugumbadija agiki aliobhubhi.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni mva yiniyo inyibheleja, aliyo hing’wi ya magi, kunguno nuweyi alina wibhembu bho gwibheleja hanze dulu, umgati yakwe, agiganikaga mihayo ya bhukenaguji, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘mva nyibheleja huna ng’wi ya magi.’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka gwita mihayo bhubhi, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umuwikaji bhobho.
Yohana 12:43.
Luka 6:26.
Luka 11:43.
KISWAHILI: MBWA MNYENYEKEVU NDIYE MNYWAJI WA MAYAI.
Chanzo cha methali hiyo, chaangalia unyenyekevu wa mbwa, ambaye ndiye mnywaji wa mayai. Mbwa huyo, hujionesha kama ni mwema kwa nje tu, ili asijulikane kuwa ndiye mnywaji wa mayai hayo. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘mbwa mnyenyekevu ndiye mnywaji wa mayai.’
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mnyenyekevu kwa nje, lakini kwa ndani siyo mzuri, maishani mwake. Mtu huyo, ni mpenda sifa kwa kujionesha kuwa yeye ni mwema, lakini kumbe ni mharifu, maishani mwake. Yeye huishi maisha ya kujionesha kuwa ni mwema ili watu wasimtambue kuwa ni mharifu.
Mtu huyo, hufanana na yule mbwa mwenye unyenyekevu wa kujionesha, lakini kumbe ndiye mnywaji wa mayai, kwa sababu naye hujionesha kwa nje kuwa ni mwema lakini kumbe kwa ndani, ndiye mharifu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘mbwa mnyenyekevu ndiye mnywaji wa mayai.’
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kutenda uovu, katika maisha yao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.
Yohana 12:43. “Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.”
Luka 6:26. “Ole wenu watu watakapowasifu, kwani ndivyo baba zao walivyowasifu manabii wa uongo.””
Luka 11:43. “Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni.”
ENGLISH: THE HUMBLE DOG IS THE EGG EATER.
The source of this proverb is the humbleness of a dog that, in fact, is the bad one. This kind of dog will always appear very humble to the extent of not predicting anything bad coming from it. But, as this proverb describes, this type of dogs are even worse than the ones that can demonstrate their theft in public. This is why people came with the proverb that ‘the humble dog is the egg eater.’
This proverb can be compared to a person who is humble in his/her appearance but the reality is he/she is not. He/she can pretend to be well mannered and therefore good to others while the reality on the ground is, he/she is a bad person. Such people are compared to humble dogs that hide their true colours of being egg eaters.
The proverb teaches people to stop doing bad things in their lives. It also teaches people to live in peace with others.
John 12:43: “They loved the praise of men more than the praise of God.”
Luke 6:26: “Woe to you when men praise you, for so did their fathers to the false prophets.”
Luke 11:43; “Woe to you Pharisees, because you love to sit in the synagogues and be greeted with respect in the marketplaces.”