672. HANGAYA YABHELEKA.

Imbuki ya kahayile kenako, yingilile ku Sonda iyo igafumaga dilu makingilima Isonda yiniyo, uluyafuma  igamanyichaga giki ubhujuku wela, kugiki abhanhu bhaje ku milimo iki wizaga bhupe. Ubhupe bhunubho, bhugolechaga ikanza lya gwandya kutumama milimo, kunguno bhuli ng’wene agadulaga ugubhona chiza. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘Hangaya yabheleka.’

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ntumami ogwipunha dilu oja ukumilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agalitumilaga chiza ilikanza ilya Limi, bho gwanguha gujigulambija gutumama milimo yakwe yiniyo. Uweyi adebhile isolobho ya gulitumila chiza ilikanza lyake lya Limi linilo. Isolobho jinijo, jilikihamo na gwipandikila matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolola ni sonda iyo igabhelekaga dulu, kunguno nuweyi agipunhaga dulu makingilima, ogigulambija gutumama milimo yakwe, iyo igang’winhaga matwajo mingi, umuwikaji bhokwe.

Uweyi agabhinhaga nabhiye bhulangwa bho gulitumila ilikanza lya limi jinagwigulambija uguitumama imilimo yabho yiniyo chiza, umukikalile kabho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘Hangaya yabheleka.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gulitumila ilikanza lyabho ilyalimi bho gwigulambija guitumama na bhukamu bhutale imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo agagujibheja chiza ikaya jabho.

Luka 1:73.

Mathayo 16:3.

2 Wakorintho 6:1.

Luka 2:32.

Waebarania 1:1…

KISWAHILI: SAYARI/NYOTA IMETOKEA.

Chanzo cha msemo huo, chatokea kwenye Nyota ile inayotoka asubuhi na mapema. Nyota hiyo, ikitokea huonesha kwamba usiku umekucha, ili watu waende kufanya kazi kwa vile mwanga umekuja.

Mwanga huo, huonesha wakati wa kuanza kufanya kazi, kwa sababu ya kila mmoja kuweza kuona vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘Sayari/Nyota imetokea.’

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mfanya kazi anayeamka asubuhi na mapema, na kwenda kufanya kazi zake, katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia vizuri muda wake wa mchana, kwa kujibidisha kuyatekeleza  kwa bidii majukumu yake hayo. Yeye anafahamu faida ya kuutumia vizuri muda wake huo wa mchana. Faida hizo, ni pamoja na kujipatia mafanikio mengi, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na Nyota ile inayotokeza asubuhi, kwa sababu naye hujilawa asubuhi na mapema kwenda kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yake, yanayompatia mafanikio mengi, katika maisha yake.

Yeye pia huwapatia mafundisho wenzake, ya kuutumia muda wao wa mchana, katika kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao vizuri, katika maisha yao. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘Sayari/Nyota imetokea.’

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao wa mchana kwa kujibidisha kuyatekeleza kwa bidii kubwa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio ya kuziendeleza vizuri familia zao.

Luka 1:73.

Mathayo 16:3.

2 Wakorintho 6:1.

Luka 2:32.

Waebarania 1:1…

star

star2

bhakima bhatumami

 

ENGLISH: THE MORNING STAR HAS APPEARED.

The source of this saying is the morning star that communicates that a new day has come. When this star appears it sweeps away darkness and invites light to mean that people have to wake up and continue with their daily activities. This scenario of making people wake up and proceed with their daily routine can be described using the saying that ‘the morning star has appeared.’

This saying can be compared to a person who wakes up early in the morning and goes to work. Such a person values time and knows when to wake up and what to do. People of this nature are likely to have achievements in life because of the way they are organized in their responsibilities. They also teach others about valuing time.

The saying teaches people about how to use their time in their daily activities. People have to work hard in order to achieve success in life.

Luke 1:73. Matthew 16: 3. 2 Corinthians 6: 1. Luke 2:32. Hebrews 1: 1.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.