670. MABHELE MANOGU ISAB´A ILAMBU.

Imbuki ya lusumo lunulo, yilolile bhulogu bho gupandika mabhele na bhudamu bho gusabha ng’ombe. Amabhele gali manogu, kunguno umunhu adulile guja ha ng’wa nsab’i ugagalila.

Aliyo lulu, umunhu ng’wunuyo adadulile ugulombe ng’ombe na gwunhiwa ya bhule, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘mabhele manogu isab’a ilambu.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agigulambijaga kutumama milimo yakwe, mpaga ojipandika isabho, umuwikaji bhobho. Umunhu ng’wunuyo, agalimaga bho bhukamu bhutale ahikanza lya mbula, mpaga ojibisha ijiliwa.

Ijiliwa jinijo, agajilyaga na mpaga ojijinja ijingi ijo jigang’wenhelaga sabho. Uweyi agabhalangaga na abhanhu bhakwe ahigulya ya guitumama imilimo yiniyo bho wigulambijaga bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, alijigemelo ikubhiye ijagutumama milimo bho wigulambija mpaga gupandika matwajo mingi, kunguno ya bhukamu bhokwe, umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu agabhawilaga giki, ‘mabhele manogu isab’a ilambu.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho, bho bhukamu bhutale, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika sabho ijagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Waebrania 12:14.

Luka 13:24.

2 Petro 1:10.

KISWAHILI: MAZIWA MARAHISI UTAJIRI MGUMU.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia urahisi wa kupata maziwa, na ugumu wa kupata ng’ombe. Maziwa ni marahisi kwa sababu mtu anaweza kwenda kwa tajiri na kupewa maziwa hayo ambayo huyatumia kama mboga.

Lakini basi, mtu huyo hawezi kwenda kwa tajiri kuomba ng’ombe wa bure na kupewa, maishani mwake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘maziwa marahisi utajiri mgumu.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kufanya kazi mpaga anapata mali, maishani mwake. Mtu huyo, hulima kwa bidii kubwa wakati wa mvua, mpaga anafaulu kupata chakula.

Chakula hicho, hukitumia kama chakula kwenye familia yake, na kingine hukiuza kwa ajili ya kujipatia mali. Yeye huwafundisha pia watu wake juu ya kuyatekeleza majukumu yao, kwa bidii hiyo, katika maisha yake.

Mtu huyo, ni mfano wa kuigwa kwa wenzake, katika kujibidisha kufanya kazi mpaga kufikia hatua ya kuyapata mafanikio mengi, kwa sababu ya bidii yake hiyo, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, ‘maziwa marahisi utajiri mgumu.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufayatelekeza majukumu yao kwa bidii kubwa, katika maisha yao, ili waweze kupata mafakinio ya kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Waebrania 12:14. “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana.”

Luka 13:24. “Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba, kwa maana, nawaambia, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.”

2 Petro 1:10. “Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuuthibitisha wito wenu na uteule wenu, kwa maana mkifanya hivyo, hamtajikwaa kamwe.”

cow milk-

cow-1

cow-2

 

ENGLISH: IT IS EASIER GETTING MILK THAN GETTING A COW.

The source of this proverb is the value of milk in relation to the value of cow. When you visit someone, you can easily get milk as present, but not cow. This is associated with value; milk is less valued while cows have more value. This is why people can say ‘it is easier getting milk than getting a cow.’

This proverb can be compared to a person who works hard to earn a living in his life. This person can spend well the rain season to cultivate his/her farm with an expectation to have good harvest at the end of season. Such a person teaches others that it is easier succeeding in life if deliberate efforts are taken seriously.

The proverb teaches people to work hard to carry out their responsibilities with great efforts in their lives. In so doing they can become very successful in life.

Hebrews 12:14: “Strive for peace with all men, and for the holiness without which no one will see the Lord.”

Luke 13:24: “Strive to enter by the narrow door; for many, I tell you, will seek to enter and will not be able.”

2 Peter 1:10: “Therefore, brethren, be the more zealous to confirm your call and election, for if you do this you will nevel fall.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.