646. KALAGU – KIZE. BHANHYA BHAMILENGANILO:- MASHIGA.

Imbuki ya kalagu yiniyo, yingilile kukalenginilile ka wiyambilija bho katumamile ka mashiga. Amashiga genayo, gali mawe nulu madafali adatu ayo gagikalaga galenganilile chiza, kugiki gadule gudimila nungu, nulu sufulila iyaguzugila ijiliwa.

Ubhulenganiji bhogo bhunubho, bhulolile bhutale, nulu bhudoni ubho bhulinganilile.  Agoyi gagikolanijiyagwa na bhaniki, kunguno nabho bhagazugaga jiliwa aha kaya. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘bhanhya bhamilenganilo:- Mashiga.’

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhalina ng’wigwano go gwiyambilija uguitumama imilimo yabho, umuwikaji bhobho. Abhanhu bhenabho, bhali na bhutogwa ubho bhugabhalumanyaga kihamo, umukikalile kabho. Abhoyi bhagapandikaga matwajo mingi, umumilimo yabho guti numo gagajisijaga ijiliwa amashiga genayo.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga na mashiga, kunguno nabho bhali na ng’wigwano go gwiyambilija halumo uguitumama chiza imilimo yabho, umukikalile kabho.

Abhoyi bhagalangaga na bhichabho, ahigulya ya gubhiza na bhutogwa bho gwiyambilija halumo ijinaguitumama chiza imilimo yabho yiniyo, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagabhaganilaga abhichabho giki, ‘bhanhya bhamilenganilo:- Mashiga.’

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’wigwano go gwiyambilija halumo uguitumama na bhutogwa imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwaho mingi, umuwikaji bhobho.

Mathayo 28:16-20. Jiligemelo ja Utatu Mtakatifu.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA:-

WASICHANA WANAOLINGANA:- MAFIGA.

Chanzo cha kitendawili hicho, chatokea kwenye ulinganifu wa mafiga katika kusaidiana kufanya kazi. Mafiga hayo, ni mawe au matofali matatu yanayolingana vizuri, kiasi cha kutosha kukishikilia chungu au chombo cha kupikia chakula. Yenyewe huwa yamelingana kwa maana kwa kuwa na ukubwa unaoendana, au kama ni madogo, yote yawe udogo unaolingana.

Mafiga hayo, hufananishwa na wasichana kwa sababu nao hufanya kazi za kupika chakula katika familia.  Yenyewe, huacha nafasi katikati ambapo huwekwa kuni zinawashwa moto na kuendelea kuchochewa mpaka chakula kinaifa vizuri. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘washichana wanaolingana:-  Mafiga.’

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale ambao wana uelewano wa kusaidiana katika kufanya kazi zao. Watu hao, wana upendo ambao huwaunganisha pamoja, maishani mwao. Wao hupata mafanikio mengi katika utekelezaji wa majukumu yao, kama yanavyoivisha chakula Mafiga hayo.

Watu hao, hufanana na mafiga, kwa sababu nao, wana uelewano wa kusaidiana pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao, maishani mwao. Wao huwafundisha pia wenzao, juu ya kuwa na upendo huo wa kusaidiana pamoja katika kuzitekeleza vizuri kazi zao. Ndiyo maana watu hao, huwahadithia wenzao kwamba, ‘washichana wanaolingana:-  Mafiga.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na ushirikiano wa kusaidiana pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Mathayo 28:16-20. Ni mfano wa Utatu Mtakatifu.

cooking1

mashiga1

mashiga

nzugi

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

THREE GIRLS OF SIMILAR ATTRIBUTES – THREE COOKING STONES.

The source of this riddle is the cooking stones. These stones always appear in the kitchen and one of their central functions is to hold a cooking pot or saucepan when cooking. These three cooking stones are characterized by having similar attributes; they have similar size and height in order to facilitate easy holding of the pot or saucepan.

The three stones are always arranged in such a way that they leave a space between them where one can make fire. This is why people came with this riddle ‘three girls of similar attributes – cooking stones’ to communicate the resemblance of cooking stones.

This riddle can be compared to people who tend to help each other in doing something. Such peple tend to regard themselves as one solid unit who can work together in order to achieve something of great impact to the society. These people also teach others about the need for helping each other in doing their jobs well.

This riddle teaches people about how to work together to help each other in fulfilling their responsibilities so that they can achieve more in their lives.

Matthew 28: 16-20. It is an example of the Holy Trinity.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.