635. MBISILA YA NCHI AIMANILE UYO ALING`OJA.

Imbuki ya lusumo lunuo, yilolile bhoja bho nchi, nulu mimba go munhu. Ubhoja bho mimba bhunubho, bhugang’wenhelejaga ung’oja gumana mbisila ningi ija mimba gokwe umunhu uyo ozumalikaga ng’wunyo.

Imbisila jinijo, jigambilijaga ugudebha umo wikalilaga unjimiji, umushigu ja bhulamu bhokwe. Ung’oja okwe ng’wunuyo, agajilang’hanaga imbisila jinijo, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘mbisila ya nchi alimanile uyo aling’oja.’

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agailanghana chiza imihayo ya mukaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adaiyombaga sagara imihayo ya mugati ya numba yakwe, kunguno adebhile ugujidimila imbisira ja kaya yakwe. Uweyi agaibhejaga chiza ikaya yakwe bho gwikala na bhuyegi na bhiye, umuwikaji bhobho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu ng’oja o nchi, kunguno nuweyi agayibhejaga chiza ikaya yakwe, bho gujilang’hana imbisila ja mukaya yakwe, umukikalile kakwe. Akikalile kakwe kenako, kagabhalangaga abhiye ahigulya ya kujibheja chiza ikaya jabho, bho guilang’hana imihayo ya mukaya jabho. Hunagwene uweyi agabhawilaga abhanhu giki, ‘mbisila ya nchi alimanile uyo aling’oja.’

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gujibheja chiza ikaya jabho, bho gujilanghana imbisila ja mukaya yabho jinijo, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala bho bhuyeji na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Mithali 25:9.

Daniel 2:22.

Luka 8:10.

Wakolosai 1:26-27.

1Wakorintho 15:51.

Waefeso 1:9.

KISWAHILI: SIRI YA MAITI AIJUAYE MWOSHA.

 Chanzo cha methali hiyo, chaangalia uoshaji wa maiti. Uoshaji huo wa maiti, humwezesha yule anayeosha kuzifahamu siri ya marehemu, kwa sababu ya kupata nafasi ya kumuangalia mwili mzima.

Siri hizo husaidia kuyaelewa maisha ya marehemu huyo yalivyokuwa katika enzi za uhai wake. Yeye huzitunza sili hizo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘siri ya maiti aijuaye mwosha.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huzitunza vizuri siri za ndani ya familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hayaongei hovyo maneno ya ndani ya familia yake hiyo, kwa sababu anafahamu namna ya kuzitunza siri za familia yake. Yeye huijenga vizuri familia yake kwa huishi kwa furaha na wenzake, maishani mwao.

Mtu huyo, hufanana na mwoshaji wa maiti azitunzaye siri za maiti, kwa sababu naye huwa anaijenga vizuri familia yake, kwa kuzitunza siri za familia yake hiyo, katika maisha yake.

Maisha yake hayo, huwafundisha wenzake namna ya kuzijenga familia zao, kwa kuzitunza vizuri siri za ndani ya familia zao hizo. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, ‘siri ya maiti aijuaye mwosha.’

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuzijenga vizuri familia zao, kwa kuzitunzia siri zake, katika maisha yao, ili waweze kuishi kwa furaha na wenzao, maishani mwao.

Mithali 25:9.

Daniel 2:22.

Luka 8:10.

Wakolosai 1:26-27.

1Wakorintho 15:51.

Waefeso 1:9.

active couple

couple africans

family kids

ENGLISH: THE CLEANER KNOWS THE SECRET OF THE DEAD.

The foundation of the overhead proverb is the washing of dead bodies. This cleaning of the corpse enables the one who washes them to discover the mystery of the deceased, because he/she gets an opportunity to look at the whole body.
Such secret helps to understand the deceased’s life during his/her lifetime. He/she takes care of those jewels, in lifetime. That is why people say, ”the cleaner knows the secret of the dead.’

Such proverb is compared to the man who takes good care of secrets of his family, in his life. Such man does not speak to any person his family’s words, because he knows how to keep his family secret. He builds his family well by living happily with others, in their lives.

The man is like a corpse cleaner who treats the mysteries of the dead, because he also builds his family well, by keeping his family’s secret, in his life.
In his own life, he teaches his family members on how to build their families, by taking good care of the secrets of their families. That is why he tells people, ‘the cleaner knows the secret of the dead.’

This proverb imparts in people an idea on how to properly build their families, by safeguarding their secrets, in their lives, so that they can live happily with others, in their lives.

Proverbs 25: 9.
Daniel 2:22.
Luke 8:10.
Colossians 1: 26-27.
1Corinthians 15:51.
Ephesians 1: 9.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.