Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile minzi. Aminzi genayo gagatumilagwa na bhanhu bho nzila ningi giti gung’wiwa, guzugilwa jiliwa, guzengelwa numba, goga, gufulila myenda na gogeja jiseme. Agoyi nulu munhu ugatema gadatinikaga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘nali nang’wanone ulu nuntema adatinikaga’ bhashosha, ‘Minzi.’
Ikalagu yiniyo igalenganijigwa kuli munhu uyo alina widohya bho guzunya gulangwa ginhu jilebhe, nulu na munhu uyo ali ndoo ukuli weyi. Umunhu ng’wunuyo adebhile giki ing’wanangwa idashilaga.
Uweyi agiikolaga na minzi ayo gagatumilagwa na bhanhu kunzila ningi, kunguno nang’hwe azunije ugulangwa nabhiye iyo atali uguyimana. Umunhu ng’wunuyo agabhutumilaga uwidohya bhokwe bho gutumama milimo yakwe kihamo na bhiye, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho. Hunagwene abanhu bhagiganilaga giki, ‘nali nang’wanone ulu nuntema adatinikaga’ bhashosha, ‘Minzi.’
Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu gubhiza na widohya bho guzunya gulangwa na bhichabho iyo bhatali uguyidebha, kugiki bhadule gwiyambilija gutumama milimo iyagubhandikila matwazo mingi umuwikaji bhobho.
(Mathayo 18:15-17; 2Wakorintho 2:5-11; Mithali 4:20-27).
KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA: NINA MWANANGU NIKIMKATA HAKATIKI – MAJI
Chanzo cha kitendawili hiki chaangalia maji. Maji hutumika kwa namna mbalimbali kama vile kunywa, kupikia, kujengea nyumba, kuoga, na kufulia nguo na kuoshea vyombo. Yenyewe hata kama mtu akiyakata hayakatiki. Ndiyo maana watu hutegeana kitendawili kwamba ‘nina mwanangu nikimkata hakatiki’ na kujibu, ‘Maji.’
Kitendawili hiki hulinganishwa kwa mtu yule mwenye unyenyekevu wa kukubali kufundishwa kitu kipya, hata na mtu yule ambaye ni mdogo kwake. Mtu huyo anafahamu kwamba elimu haina mwisho. Yeye hufanana na maji yanayotumika kufanyia kazi mbalimbali, kwa sababu naye hukubali kufundishwa kile asichokifahamu, hata na mtu yule aliye mdogo kwake. Mtu huyo huutumia unyenyekevu wake kufanya kazi pamoja na wenzake, ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi maishani mwao. Ndiyo maana watu hutegeana kitendawili kwamba ‘nina mwanangu nikimkata hakatiki’ na kujibu, ‘Maji.’
Kitendawili hiki hufundisha watu kuwa na unyenyekevu wa kukubali kufundishwa na wenzao kile wasichokijua, ili waweze kusaidiana vizuri katika kuyatekeleza majukumu yawezayo kuwapatia mafanikio mengi maishani mwao.
(Mathayo 18:15-17; 2Wakorintho 2:5-11; Mithali 4:20-27).
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME: I HAVE MY BABY, WHEN I CUT HIM/HER HE/SHE DOES NOT BREAK APART – WATER.
The origin of thisriddle is water. Water is used in a variety of ways, including drinking, cooking, building houses, bathing and washing dishes and clothes. When a person tries cutting it, it does not break apart. That’s why people pose a riddle, ‘I have my baby, when I cut him/her, he/she does not break apart, and respond, ‘Water.’
This riddle, is used comparatively to refer to a person who has the humility to be willing to be taught something new, even by the person who younger or of lesser status than him/her. The person realizes that human beings never stop learing. He/she is like water that is used to do a variety of tasks, because he, too, is willing to be taught what he does not know, even by a person who younger or of lesser status than him/her. The person uses his/her humility to work together with others, so that they can achieve notable success in their lives. That is why people pose a riddle, ‘I have my baby, when I cut him/her, he/she does not break apart, and respond, ‘Water.’
This riddle teaches people about the humility of accepting what they are taught by their peers, especially something they do not know, so that they can help each other in fulfilling roles that can give them the success they desire in their lives.
(Matthew 18: 15-17; 2 Corinthians 2: 5-11; Proverbs 4: 20-27).