519. KALAGU – KIZE: UNTOLWA NG’WUNUYU NG’WAYI UKUMILIMO:- MOTO.

Imbuki ya kalagu yiniyo ilolile bhukali bho moto. Umoto ulu gupembwa gugabhakaga bho bhobhukali ubho bhukomile gumbisha munhu. Hugukaya giki, umoto ulu gubhaka gugikala ng’wayi, kunguno gugabhizaga gusebhu noyi. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘untolwa ng’wunuyu ng’wayi ukumilimo’ bhashosha, ‘Moto’.

Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kuli ng’winga o hakaya uyo alintumami o milimo. Ung’winga ng’wunuyo agaitumamaga imilimo yakwe bho nyakamu, niyo bho wanguwangu. Uweyi agikolaga n’umoto uyo gugabishaga jiliwa, kunguno nang’hwe alinkamu ugutumama imilimo yakwe, niyo agatuamamaga bho wanguwangu. Umunhu ng’wunuyo adebhile ugubhalanja abhiye inzila ja guyitumama imilimo yiniyo nyakamu na wanguwangu. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘untolwa ng’wunuyu ng’wayi ukumilimo’ bhashosha, ‘Moto.’

Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu  gwigulyambija gutumama milimo yabho bho wanguwangu, kugiki bhadule gupandika sabho ja gujilang’hanila chiza ikaya jabho.

(Mithali 14:7; Yoshua Bin Sira 26:1-3; Mithali 31:10-31).

KISWAHILI: KITENDAWILI     –    TEGA: MWALI HUYU NI MKALI KAZINI – MOTO.

Chanzo cha kitendawili hiki chaangalia ukali wa moto. Moto ukiwashwa huwa mkali kiasi cha kutosha kumuunguza mtu. Ndiyo kusema kwamba, moto ukiwashwa huwaka kwa ukali kwa sababu ya hali yake hiyo. Ndiyo maana watu hutegeana kitendawili kwamba, mwali huyu ni mkali kazini’ na kujibu, ‘Moto.’

Kitendawili hiki hulinganishwa kwa mwali aliyeolewa katika familia fulani ambaye hufanya kazi zake kwa bidii na kwa haraka. Mtu huyo huyatekeleza vizuri majukumu yake na kwa haraka inavyotakiwa. Yeye hufanana na moto unaoivisha chakula kwa sababu naye hufanya kazi zake kwa bidii na haraka. Mtu huyo anafahamu kuwafundisha wenzake namna ya kuyatekeleza majukumu yao kwa bidii na kwa haraka. Ndiyo maana watu hutegeana kitendawili kwamba, ‘mwali huyu ni mkali kazini’ na kujibu, ‘Moto.’

Kitendawili hiki hufundisha watu kuwa na bidii ya kufanya kazi zao kwa haraka, ili waweze kupata mafanikio mengi yawezayo kuziendeleza vizuri familia zao.

(Mithali 14:7; Yoshua Bin Sira 26:1-3; Mithali 31:10-31).

moto

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME: THIS BRIDE IS HARDWORKING ONE: – FIRE.

The origin of this riddle is the severity of fire heat. When a fire is lit, it becomes hot enough to burn a person. Yes, when a fire is lit it burns violently because of its condition. That’s why people pose a riddle, ‘This bride is a hard working one:- ‘Fire.’

This riddle is used comparatively with reference to a newly married bride who who performs her duties diligently and quickly. The bride performs her duties properly and promptly. She is like a fire that cooks food, for she works hard and quickly. The bride of this kind knows how to teach other people how to carry out their responsibilities diligently. That’s why people pose a riddle, ‘This bride is hard working one:- Fire.’

This riddle teaches people to be diligent in doing their work, so that they can achieve notable successes that can sustain their families well.

(Proverbs 14: 7; Joshua Bin Sira 26: 1-3; Proverbs 31: 10-31).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.