Imbuki ya kalagu yiniyo yilolile ndimu iyo igitanagwa nungu. Inungu kali kalimu kadoo ako kali na mifa pye umili gogo. Amifa genayo kagagatumilaga bho gubhachimila abhanishi bhako, ulu bhukubhukila. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘alitaama masonga nubhuta adinabho’ bhashosha, ‘Nungu’.
Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agateganilaga nimo nulu mhayo uyo adagudulile. Umunhu ng’wunuyo agajimijaga makanza mingi, kunguno ya gulihadika kulitumama ilinimo ilo lidalenganilile n’ubhudula bhokwe.
Uweyi alemile nulu gulomba wambilijiwa bho gugutumama unimo gunuyo gufumila kubhiye. Abhiye abho bhadebhile igiki adinabho ubhudula ubho gugushisha unimo gunuyo bhagang’wilaga giki, ‘alitaama masonga nubhuta adinabho’ bhashosha, ‘Nungu.’
Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu gwideta chiza haho bhatali ugwandya uguitumama imilimo yabho, kugiki bhadizutegana sagala bho gujimija makanza na nguzu jabho kunimo uyo bhadagudulile.
(Luka 14:28-32).
KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA: ANARUSHA MISHALE ILHALI HANA UPINDE –NUNGUNUNGU.
Chanzo cha kitendawili hiki chaangalia mnyamapori aitwaye nungunungu. Mnyama huyo ni mdogo, ambaye ana miiba mwili mzima. Miiba hiyo huitumia kuwachomea maadui zake wanapomvamia. Ndiyo maana watu hutegeana kitendawili kwamba, ‘anarusha mishale ilhali hana upinde’ na kujibu, ‘Nungunungu.’
Kitendawili hiki hufananishwa kwa mtu yule ambaye hujidai kufanya kazi ambayo hana uwezo nayo. Mtu huyo hupoteza muda mwingi bure kwa sababu ya kulazimisha kuifanya kazi iliyo nje ya uwezo wake. Yeye hataki hata kuomba msaada kutoka kwa wenzake ambao wanaweza kuifanya vizuri kazi hiyo. Wenzake wale wanaomfahamu kwamba hana uwezo wa kuifanya kazi hiyo humwambia kwamba ‘anarusha mishale ilhali hana upinde’ na kujibu, ‘Nungunungu.’
Kitendawili hiki chafundisha watu kufikiri kwanza kabla ya kuamua kufanya kazi zao, ili wasiharakishe ovyo wasije wakapoteza muda katika kufanya kazi wasizoziweza.
(Luka 14:28-32).
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE- LET IT COME: HE/SHE SHOOTS ARROWS WITHOUT A BOW – A PORCUPINE.
The origin of this riddle is a porcupine. This is a small wild rodent with squills or spines all over its body. The animal uses the squills for defence against its enemies. That is why people pose a riddle, ‘He shoots arrows without a bow’ and reply, ‘A porcupine.’
This riddle is used to warn people who force themselves to perform tasks that are beyond their capabilities. A person who tries to do that wastes one’s time because of forcing himself/herself to do something he/she is not capable of. Such a person doesn’t even want to ask for help from his/her colleagues, who can do the job well. His/her colleagues who know that he/she is unable to do the job tell him/him the riddle, ‘He shoots arrows without a bow’ whose reply is ‘a porcupine.’
This riddle teaches people to think first before doing their jobs, so that they do not hurry, lest they waste time in performing tasks they are not capable of.
(Luke 14: 28-32).