504. LYABHUMENDE GITI LIJISINZA.

Imbuki ya kahayile kenako yilolile ginhu ijo jigitanagwa jisinza. Ijisinza nulu jigasimbilwa hasi, uyo agulimaga agujipunila jitali jilijidimu, giti numo jalili aha gwandya.  Ijoyi nulu jigagwila gutu, jigikalaga jidimu duhu, jidagalukaga. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘lyabhumende giti lijisinza.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adatinginyiyagwa sagala, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agimaga ha bhung’hana ilali, bho pye amakanza. Uweyi alemile ugusegeja nulu ugusegejiwa ahabhung’hana bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo alinshikanu ijinaguwikalana ubhung’hana bhunubho. Hunagwene agalenganijiyagwa na jisinza ijo jilijidimu bho pye amakanza, kunguno nang’hwe, alindimu ugubhuleka ubhung’hana bhunubho, umukikalile kakwe. Uweyi adebhile ugubhalanga na bhiye ugubhumana ubhung’hana bhunubho, nuguwikalana. Hunagwene abhanhu bhaganyombaga giki ‘lyabhumende giti lijisinza.’

Akahayile kenako kalanga bhanhu gubhumana ubhung’hana na gubhiza bhashikanu ijinaguwikalana ubhunghana bhunubho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.

(Mathayo 7:24-27; Mathayo 16:13-20; 1Petro 4:12-19).

KISWAHILI: NI IMARA KAMA CHUMA.

Chanzo cha msemo huu, chaangalia kitu ambacho huitwa chuma. Chuma hicho, hata kikichimbiwa chini, alimaye pale kilipochimbiwa atakikuta kikiwa imara kama kilivyokuwa mwanzoni. Chenyewe, hata kikipata kutu, huendelea kuwa kigumu tu; hakigeuki kuwa kilaini. Ndiyo maana watu husema kwamba, ‘ni imara kama chuma.’

Msemo huu hulinganishwa kwa mtu yule asiyetetereka ovyo maishani mwake. Mtu huyo husimama imara katika ukweli wakati wote. Yeye hukataa kuyumbishwa wala kuondolewa kwenye ukweli huo.

Mtu huyo alishaimarika katika kuuishi ukweli huo, hadi kufikia hatua ya kuwa mfano wa kuigwa na wenzake. Ndiyo maana yeye hulinganishwa na chuma kilivyo madhubuti muda wote, kwa sababu naye ni mgumu kuuacha ukweli huo maishani mwake.

Yeye anafahamu pia kuwafundisha wenzake kuuelewa ukweli na kuuishi katika maisha yao ya kila siku. Ndiyo maana watu humsema kwamba ‘ni imara kama chuma.’

Msemo huo hufundisha watu kuufahamu na kuuishi ukweli kwa ukamilifu, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao.

(Mathayo 7:24-27; Mathayo 16:13-20; 1Petro 4:12-19).

chuma

ENGLISH: IT IS ‘AS STRONG AS IRON’.

The origin of this saying is something called iron. Even when it is burried, someone will eventually find it as strong as it was in the beginning when one digs it out. Even if it gets rusty, it just remains strong; it does not turn out to be soft. That’s why people say, ‘As strong as iron.’

The saying is used comparatively to refer to a person who is not swayed in life as regards truth. That person always stands firm on the truth. He refuses to be swayed or shaken from that truth.

Such a person is steadfast in living the truth, to the point of being a role model to others. That is why he is compared to a hard metal that remains so at all timse, because he/she too is hard to let go of the truth in his life.

He also knows how to teach others about understanding the truth and living it in their daily lives. That is why people describe such a person, ‘As strong as iron.’

The saying teaches people about understanding and living the truth to the fullest so that they can adequately succeed in their lives.

(Matthew 7: 24-27. Matthew 16: 13-20. 1Peter 4: 12-19).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.