Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola ndimu iyo ilitanwa Ng’ombe. Ingombe yiniyo, ili na magulu ane, ha matambi amadoto, ayabhili momu, ha mapembe gayo ing’ombe yiniyo. Ilitambi ilimo lisaji, ugwene hunkila goyo, kunguno gukilalaga gulifilinjiwa ukunu nu kunu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, ‘nti gone guli na matambi mpungati, ayane madoto, ayabhili, momu, ilimo lisaji:- Ng’ombe.’
Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile ugugalekanya chiza amakanza. Umunhu ng’wunuyo, umulikanza lya jidiku amanile igiki isi igikalaga ndoto, agalimaga kunguno lilikaza lya gulima.
Uweyi agisuyaga umulikanza lya chu, kunguno isi igumaga na malima nago gagimaga. Agatumamaga milimo ya gujilanhana chiza ijiliwa ijo ojipandika aho olimaga.
Ilitambi ilisaji, ligikolaga na bhanhu abho bhagajitumamilaga sagara isabho ijo bhagajipandikaga umubhuchoji bhobho. Abhanhu bhenabho, bhagajing’welaga walwa mpaga bhandya guyomba mihayo ya sagala, guti bhanhu bhasaji.
Abhanhu bhenabho, ulu bhuhaya guja gujung’wa walwa, bhagiwilaga giki, bhaje ukubhusaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, ‘nti gone guli na matambi mpungati, ayane madoto, ayabhili, momu, ilimo lisaji:- Ng’ombe.’
Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gugatumila chiza amakanza gabho aga milimo, na gujitumila chiza isabho ijo bhalijipandika, umumilimo yabho yiniyo, kugiki, bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Mathayo 16:1-4.
Mathayo 24:32-38.
KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA
MTI WANGU UNA MATAWI SABA MANNE MABICHI, MAWILI MAKAVU, MOJA KICHAA:- NG’OMBE.
Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia mnyama aitwaye Ng’ombe. Ng’ombe huyo, ana miguu, minne, ndiyo matawi mabichi, yale mawili ambayo ni makavu, ni pembe zake ng’ombe huyo. Lile moja ambalo ni jehu, ni mkia wake, maana huwa hautulii, kwa sababu huwa unachezeshwa chezeshwa tu. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘mti wangu una matawi saba, manne mabichi, mawili makavu, moja kichaa:- ng’ombe.’
Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye afahamu kutofautisha vizuri majira mbalimbali ya mwaka. Mtu huyo, hufahamu huutumia wakati wa masika kwa kulima, kwa bidii kubwa, kwa sababu wakati huo, ardhi huwa ni mbichi.
Yeye hupumzika wakati wa kiangazi, kwa sababu wakati huo, ardhi huwa ni ngumu na kavu. Huo ni muda wa kuyakusanya mazao yake vizuri, na kuyahifadhi sehemu ambayo yaweza kuyatunza vizuri.
Tawi jehu huonesha wakati wa kiangazi, ambao baadhi ya watu huyatumia mafanikio ya kilimo chao, au mali zao, kwa kunywea pombe. Baadhi yao hulewa mpaka kufikia hatua ya kuanza kuongea maneno yasiyofaa, kama wehu.
Watu hao, hualikana kwenda kunywa pombe wakielezana kwamba, waende kwenye wehu wao. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, ‘mti wangu una matawi saba, manne mabichi, mawili makavu, moja kichaa:- ng’ombe.’
Kitendawili hicho, chafundisha watu juu ya kuutumia muda wao wa kazi vizuri, na kuyatumia mafanikio ya kazi zao hizo vizuri, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.
Mathayo 16:1-4.
Mathayo 24:32-38.
ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.
MY TREE HAS SEVEN BRANCHES; FOUR ARE NOT DRY, TWO ARE DRY, ONE IS CRAZY- COW.
The source of this riddle is a cow and its body parts; four legs that help it keep on walking, two horns that are immobile, and a tail that keeps on moving to swip away insects that can tend to attack the cow. Therefore the riddle that ‘my tree has seven branches; four are not dry, two are dry and one is crazy’ communicates how the cow body parts work.
This riddle can be compared to a person who knows how to properly distinguish the different seasons of the year. They can use the spring season for ploughing with great efforts because this is the time when the soil is wet and easy to cultivate. During dry season, they gather their produce from the farm and keep them safely for future use. During summer, people spend what they produced from their farms. They drink local brew to their satisfaction. It is the time where one expects to have extravagance in terms of expenditure.
This riddle teaches people about how to use their time well and make the most of their work so that they can better their families as well as their lives.
Matthew 16: 1-4.
Matthew 24: 32-38.