Imbuki ya lusumo lunulo yilolile wisagiji bho nyama yibupu. Inyama yiniyo ilindololo noyi, iyo igagulagwa bho hela ngehu duhu.
Kuyiniyo lulu, uyo aliisagilwe inyama yiniyo adudula ugwilya mpaga wiguta, kunguno ya bhudoo bhoyo bhunubho. Umunhu ng’wunuyo agitindikaga ugujichola iginhu ijo jilina solobho nhale, kunguyo ya ‘gwisagilwa nyama yibupu.’
Ulusumo lunulo lugalenganijjiygwa kuli munhu, uyo agisagilagwa ginhu ijo jidina solobho, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agalekaga uguitumama imilimo iyo ilina solobho, kunguno ya gwisagilwa ginhu jinijo ijo jidadulile nulu ugung’wambilija, umuwikaji bhokwe bhunubho.
Hunagwene agalenganijiyagwa na ‘gwisagilwa nyama yibupu,’ kunguno nang’hwe, wisagililwe ginhu ijo jidina solobho, umuwikaji bhokwe.
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwisagilwa ginhu ijo jidulile gubhambilija ijinagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho, kutinda kujimiza makanza gabho bho gulindila ginhu, ijo jidina solobho.
Warumi 8:25.
Zaburi 62:9.
2 Wakorintho 12:11.
KISWAHILI: KUTUMAINI NYAMA YA KONGOSHO.
Chanzo cha methali hiyo, chaangalia hali ya kutumaini nyama ya kongosho. Nyama hiyo ni ndogo sana na nyepezi, ambayo hununuliwa kwa bei ya chini sana.
Kwa hiyo, mtu yule anayeitumaini nyama hiyo hawezi kuila mpaka akatosheka. Mtu huyo, hujichelewesha kutafuta kitu ambacho kinathamani kubwa, kwa sababu ya ‘kutumaini nyama ya kongosho.’
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutumaini kupata au hutegemea kitu kisicho na thamani katika maisha yake.
Mtu huyo, huacha kufanya kazi za maana, ambazo zinathamini, kwa sababu ya kutumaini kitu hicho ambacho, hakiwezi kumsaidia katika maisha yake.
Ndiyo maana, watu humlinganisha na ‘kutumaini nyama ya kongosho,’ kwa sababu naye hutegemea kitu kisicho na faida maishani mwake.
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kutumaini kitu ambacho chaweza kuwasaidia katika kuzijenga vizuri familia zao, maishani mwao, badala ya kupoteza muda wao, kwa kutegemea vitu visivyoweza kuwasaidia katika kuziendeleza familia hizo.
Warumi 8:25.
Zaburi 62:9.
2 Wakorintho 12:11.
ENGLISH: RELYING ON THE PANCREACE MEAT.
The source of this saying is the pancreace meat that is believed to be very small in size and it is tender thus bought at a very cheap price. Therefore one who eats pancreace meat cannot easily get satisfaction. Instead, he/she is adviced to look for something of great value in order to have satisfaction because reliance on pancreace meat only can make one suffer from hunger.
This saying can be compared to a person who depends on worthless things for his/her survival. Such people are being warned against it by telling them not to ‘rely on the pancreace meat’ as a way to make them hard workers.
This proverb teaches people to hope for something that will help them better build their families. They don’t have to waste their times doing worthless things rather work hard and help their families to develop in different aspects.
Romans 8:25.
Psalm 62: 9.
2 Corinthians 12:11.