Imbuki ya lusumo lunulo yilolile gwinga go bhikaji bha hakaya ndebhe. Ungeni ulu ushika ahakaya yiniyo ukija ugubhasanga abhinikili kaya, agubhuja, uko bhajaga, kugiki adule gumana. Hunagwene umunhu ng’wunuyo agabhujaga giki, ‘kaya iyi yajaga hali?’
Ulusumo lunulo lugalenganijjiyagwa kuli munhu uyo adebhile imilimo ya ng’wa munhu unkima ijinaguilang’hana ikaya. Umunhu unkima, agayilang’hanaga ikaya bho gubhazugila jiliwa, abhanhu bhaha kaya yiniyo.
Ulu hakaya ndebhe munhu unsanga alihoyi ungosha, unkima atiho, agabhujaga uko yajaga ikaya, kunguno ikaya imanilwe na nkima. Hunagwene abhanhu bhagabhujaga ulu bhungayiwa unkima ahaka ndebhe, giki ‘kaya iyi hali?’
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guimana chiza imilimo ya bhakima, umugujilang’hana ikaya, kugiki bhadule gubhambilija bho gwikala nabho chiza, umuwikaji bhobho.
Mwanzo 2:18 21-22.
Mathayo 19:6.
Luka 1:41 – 42.
KISWAHILI: MJI HUU UMEENDA WAPI?
Chanzo cha methali hiyo chaangalia uondokaji wa wanafamilia fulani kwenye mji wao. Mgeni akifika kwenye mji au familia hiyo, akamkosa mwenye nyumba ambaye ni mwanamke wa pale, huuliza alikoenda, ili aweze kufahamu. Ndiyo maana watu huuliza kwamba, ‘mji huu umeenda wapi?’
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anafahamu kazi na umuhimu wa mwanamke katika kuutunza mji. Mwanamke huyo huutunza mji wake, kwa kuwapikia chakula watu waishio kwenye mji huo.
Mtu akienda kwenye mji fulani akamkuta mwanaume bila kuwepo mwanamke, huuliza ulikoenda mji, kwa sababu, mji hufahamiwa na mwanamke. Ndiyo maana watu wakimkosa mwanamke, huuliza kwamba, ‘mji huu umeenda wapi?’
Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuyafahamu majukumu na wajibu wa wanawake katika kuitunza familia, ili waweze kuishi nao vizuri, maishani mwao.
Mwanzo 2:18, 21-22.
Mathayo 19:6.
Luka 1:41 – 42.
ENGLISH: WHERE HAS THIS FAMILY GONE?
The source of this saying is the departure of some family members from their living place. When a stranger arrives in at a family and misses the host, especially the host’s wife, he/she ask her husband on the whereabout of his wife, who is traditionally regarded as the care taker of the whole family. The question ‘where has this family gone?’ is asked to mean the absence of the key person in the family who ensures that food is always available for the family.
The saying can be compared to a man who knows the role and importance of a woman in taking care of the family. The woman takes care of her family by providing it with food and accommodation. So, when one visits another person, one of the expectations is to have good food and accommodation. All these services are traditionally associated with women roles in the family. Thus the absence of a woman in the family there is a possibility of not having a homely environment and one can dare to ask, ‘where has the family gone?’ to mean mother of the house.
The saying teaches people about understanding the roles and responsibilities of women in caring the family. They do so in order to have a good mannered family that knows and respects the roles and responsibilities of members in the family.
Genesis 2:18, 21-22.
Matthew 19: 6.
Luke 1:41 – 42.