Imbuki ya kahayile kenako ilolile lufu lo myaji. Ulufu lunulo lolechije giki nu ng’wana o myaji ng’wunuyo, nang’hwe alacha. Hunagwene abhanhu b’agang’wilaga ung’wana ng’wunuyo giki, ‘bhujiku b’onnia noko nub’eb’e b’ulagulya.’
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adadililaga mayange ga lufu ga bhaduguye. Umunhu ng’wunuyo adajaga ukumayage ga bhiye bhenabho. Ulu bhamilinga giki agambilije ugubhajike abhiye, uweyi agajaga kumilimo yakwe duhu. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘bhujiku b’onnia noko nub’eb’e b’ulagulya.’
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gub’iza na b’umo bho gwiyambilija umumayange, kunguno, b’uli ng’wene alacha.
Mwanzo. 3:19.
Ruth 1:17.
1Wafalme 2:37.
KISWAHILI: USIKU ULIMLA MAMA YAKO NA WEWE UTAKULA.
Chanzo cha msemo huo chaangalia kifo cha mzazi. Kifo hicho chaonesha kwamba, kila mmoja akiwemo mtoto wa mzazi huyo, atakufa. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘usiku ulimla mama yako na wewe utakula.’
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hajali misiba ya ndugu zake. Mtu huyo huwa hahudhulii kwenye misiba hiyo ya ndugu zake hao. Wakimwalika kwenda kuwazika, yeye huenda kwenye kazi zake tu. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘usiku ulimla mama yako na wewe utakula.’
Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umoja wa kuwawezesha kusaidiana katika misiba mbalimbali, kwa sababu kila mmoja atakufa.
Mwanzo. 3:19.
Ruth 1:17.
1Wafalme 2:37.
ENGLISH: THE NIGHT ATE YOUR MOTHER WILL ALSO EAT YOU.
The source of the above saying looks at the death of a parent. The death of the parent indicates that everyone, including the child, will die. That is why people can tell someone that ‘the night ate your mother will also eat you.’
The saying can be compared to a person who doesn’t care about the tragedies of his/her relatives. Such a person does not attend his/her relatives’ problems. If invited, he/she ends up giving a lot of excuses while in actual fact, he/she is busy with his/her own doings. Such people are being warned by telling them that ‘the night ate your mother will also eat you.’
The saying teaches people about being united enough to help one another in different problems. Everyone has to know that death is a final destination for every living creature.
Home. 3:19.
Ruth 1:17.
1Kings 2:37.