Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhung’wi bho ginhu ijo jilijilulu. Iginhu jinijo jigab’ipyaga ululimi lo ng’wa munhu uyo ojing’waga iginhu jinijo. Hunagwene umunhu ng’wunuyo agacholaga ginhu ijo jilijinonu, ja gwipolelegeja bho guyomba giki, ‘nipoleleje.’
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kulimunhu uyo witilagwa mihayo ya gumpinihaja umung’holo yakwe. Umunhu ng’wunuyo, agagayigagwa ulubhango umukikalile kakwe. Hunagwene agacholaga gwigwa mihayo ya wiza, iyo idulile gununguja bho guyomba giki, ‘nipoleleje.’
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kub’alunguja abhichab’o, ab’o bhali na makoye, kugiki bhadule guyega kihamo nabho, umuwikaji bhobho.
Ufunuo 10:10-11.
KISWAHILI: NITULIZE UCHUNGU.
Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye unywaji wa kitu kilicho kichungu. Kitu hicho huharibu ulimi wa yule aliyekinywa. Ndiyo maana mtu huyo hutafuta kitu kilicho kitamu cha kutulizia uchungu huo, kwa kusema kwamba, ‘nitulize uchungu.’
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye amefanyiwa kitendo cha kumhudhunisha moyoni mwake. Mtu huyo hukosa raha maishani mwake. Ndiyo maana hutafuta kusikia neno zuri liwezalo kumfariji, kwa kusema kwamba, ‘nitulize uchungu.’
Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwafariji wenzao walioko kwenye matatizo, ili nao waweze kufurahi pamoja nao, maishani mwao.
Ufunuo 10:10-11.
ENGLISH: LET ME COOL THE BITTERNESS.
The source of the above saying comes from drinking something which has a bitter taste. Such a drink can be very disturbing thus demanding for something sweet that can cool down the bitterness. This is why one can hear people looking for sweet things in order to suppress bitterness that they experience during that particular time.
The saying can be compared to someone who is hurtled by someone else. Such a hurt person will feel uncomfortable most of his/her time. Therefore he/she needs someone else who can come with sweet words to calm him/her down. Such a hurt person, in receiving something to suppress the bitterness, can say, ‘let me cool the bitterness.’
The saying teaches people about comforting others who are in trouble so that they can also enjoy in their lives.
Revelation 10: 10-11.