Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhuchoji bho jiliwa. Ijiliwa jinijo jigategagwa, guti ndimu nulo ndilo. Uluojigobya unchoji ojo ng’wunuyo agayegaga, uweyi kihamo na bhiye. Hunagwene abhiye bhagang’wilaga giki, ‘wagobya nilo (b’ulilo).’
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo opandikaga milimo ya gung’wenhela jiliwa. Umunhu ng’wunuyo agayegaga noyi ulu oyipandika imilimo yiniyo, kunguno ya b’upandiki bhokwe, bho aho ng’wagulila ijiliwa. Abhazenganwa bhakwe nabho bhagayegaga ugumona ng’wichabho opandikaga aho ng’ wagulila ijiliwa. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagang’wilaga giki, ‘wagobya nilo (b’ulilo).
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guchola milimo ya gubhenhela jiliwa, na guyega kihamo ulu bhayipandika imilimo yiniyo.
1Wakorintho 9:13-14.
KISWAHILI: UMEKAMATA PA KULIA
Chanzo cha msemo huo chatokea kwenye utafutaji wa chakula. Chakula hicho hupatikana kwa njia mbalimbali zikiwemo zile za kutafuta kazi, kuvua samaki, kuwinda wanyama na kuwatega kwa mtego. Akipata chakula hicho mtu huyo hufurahi sana, yeye pamoja na wenzake. Ndiyo maana wenzake humwambia kwamba, ‘umekamata pa kulia.’
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule aliyepata kazi ya kumletea chakula. Mtu huyo hufurahi sana apatapo kazi hiyo, kwa sababu kazi hiyo humletea chakula. Majirani zake nao pia hufurahi kumuona mwenzao amepata pa kulia. Ndiyo maana watu hao, humwambia hivi, ‘umekamata pa kulia.’
Msemo huo hufundisha watu juu ya kutafuta kazi za kuwaletea chakula, na kufurahi kwa pamoja wazipatapo kazi hizo.
1Wakorintho 9:13-14.
ENGLISH: YOU TRAPPED SOMETHING TO EAT
The source of this saying is a search for food. Such food is available by trapping animals or fishing. When someone finds such food he/she becomes very happy with his/her companions. That is why his/her companions can tell him/her, “you have trapped something to eat.”
The saying is compared to a person who got a new job that will bring him or her food. Such a person becomes very happy when he/she gets such a job. The neighbours of that person also become happy for him/her. That is why those people can say, ‘you have trapped something to eat.’’
The proverb teaches people about finding jobs that can bring them food and make them happy.
1 Corinthians 9: 13-14.