276. NTIMBA NGONGO DALYA JA NG’WAKA

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile b’ulub’iji b’o matwajo mapya ga ng’waka. Abhanhu ulubhulima jiliwa, bhagikalaga na ng’humbu nhale ya gubisha, na gujilya ijiliwa jinijo. Ulu bhandya ugulub’ila bhagitimbaga ngongo na guyomba giki, ‘ntimba nyongo dalya ja ng’waka.’

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagatumamaga milimo yabho kubhukamu bhutale.  Hangi bhagalumbaga noyi ulu bhajipandika isabho ja matwajo ga milimo yabho yiniyo.

Abhanhu bhenabho bhagayegaga noyi ulu bhagapandika amatwajo genayo, kunguno bhagizukaga umo bhakoyelega ugujilima bho bhukamu bhatale, ijikolo jinijo. Hunagwene ulu bhajilya bhagayombaga giki, ‘ntimba ngongo dalya ja ng’waka.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gutumama milimo bho bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho. Amatwayo genayo, gagubhambilija ijinagujibheja chiza ikaya jabho.

Zaburi 65:9 – 13.

KISWAHILI: PIGA MGONGO KWA MGUMI TUMEKULA VYA MWAKA

Chanzo cha methali hiyo chaangalia ulaji wa mara ya kwanza wa mavuno mapya ya mwaka. Watu wakilima chakula huwa na hamu kubwa ya kupata mavuno mengi na kuyatumia kwa kuyala mavuno hayo. Wakianza kula kwa mara ya kwanza, hujipiga mgongo kwa ngumi wakisema, ‘piga mgongo kwa mgumi tumekula vya mwaka.’

Methali hiyo hulinganishwa kwa watu wale wafanyao kazi zao kwa bidii kubwa. Pia wao hushukuru sana wakipata mali za mavuno ya kilimo chao. Watu hao hufurahi sana wakipata mavuno hayo, kwa sababu ya kukumbuka walivyohangaika katika kulima kwa bidii kubwa namna hiyo. Ndiyo maana wakianza kuyaonja mavuno hayo mpya husema, ‘piga mgongo kwa ngumi tumekula vya mwaka.’

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kufanya kazi kwa bidii kubwa, kusudi waweze kupata mavuno mengi maishani mwao. Mavuno hayo yatawasaidia katika kuzijenga vizuri familia zao.

Zaburi 65:9 – 13.

maize food

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.