271. MONGO GUGALYAGA NG’WELIMI (NG’HEGI).

Imbuki ya lusumo lunulo ilolile ng’welemi, nulu ng’hegi omuminzi. Umunhu ng’wunuyo akikalaga agudahahijije umongo uyo aligubhona, nulu gugab’iza gutale gete uyo gukomile gunchala, nulu gumulaga. Kuyiniyo lulu, agahadikijaga gugub’ita umongo gunuyo, nose gugang’heb’aga na gunchala, kunguno ya wihayi bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, ‘mongo gugalyaga ng’welemi,’ kunguno umunhu uyo adamanile uguhega agabhizaga aling’wob’a ugugukila umongo, nulu gugab’iza guli ndoni.

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo aling’wihai giki adulile bhuliginhu, nijo adajidulile. Umunhu ng’wunuyo adazunyaga igiki adumile ginhu jilebhe. Uwei bhuli jene agigimbaga giki ajidulile. Ing’halikilo ya wihayi bho ng’wa munhu ng’wunuyo ili gulabhuka uwei, nulu guzumalika. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga umunhu ng’wunuyo giki, ‘mongo gugalyaga ng’welemi.’

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu kuleka wihayi, nulu wigimbi bho gwituula bhamani, nulu bhaduji, bha bhuli ginhu.  Gashinaga lulu, yigelelilwe gub’iza na widohya bho kudebha igiki ilihoyi mingi iyo bhadayidulile, kugiki bhadule gulang’hana bhupanga bhobho, na gulangwa na bhichabho iyo bhadayimanile.

(Luka 18:10 – 14; Bagalatia 6:2 – 5)

KISWAHILI: MTO HULA MWOGELEAJI.

Chanzo cha methali hiyo huangalia mwogeleji wa majini. Mtu huyo huwa akijitapa kuwa aweza kuuvuka mto, hata kama mto huo utakuwa mkubwa kiasi cha kuweza hata kumsomba au kumuua. Kwa hiyo basi, yeye hulazimisha kuuvuka mto huo, na matokeo yake huwa kusombwa na mto, kwa mtu huyo kwa sababu ya kujidai kwake huko. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, ‘mto hula mwogeleaji,’ kwa sababu yule ambaye hafahamu kuogelea huogopa kuvuka, hata kama mto huo ni mdogo.

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujidai kwamba aweza kila kitu hata kile ambacho hakiwezi. Mtu huyo hakubali kwamba hawezi kitu fulani. Yeye hujigamba kuwa aweza kila kitu. Matokeo yake ni kuumia au kufariki dunia kwa mtu huyo, kutokana na kujidai kwake. Ndiyo maana watu humkumbusha mtu huyo kwamba ‘mto hula mwogeleaji.’

Methali hiyo hufundisha watu kuacha kujitapa kwamba wao waweza kila kitu, hata kile ambacho hawakiwezi. Kumbe, yafaa kuwa na unyenyekevu wa kuelewa na kukubali kwamba, kuna mengi wasiyoyaweza, wala kuyafahamu, ili waweze kusalimisha maisha yao, na kujifunza mengi wasiyoyaelewa, kutoka kwa wale wanaoyaelewa hayo.

(Luka 18:10 – 14; Wagalatia 6:2 – 5).

 

 

 

swimmer-

ENGLISH: A RIVER DROWNS A SWIMMER.

The origin of this proverb is a swimmer who forces to cross a river, bragging to have the ability to do so even if the river is powerful enough to drown someone. Because of pomposity, the person forces to cross the river, the result of which is usually drowning. That is why people tell him/her, ‘A river drowns a swimmer,’ because he who does not know how to swim is always afraid of crossing a river, regardless of how small it may be.

The proverb is used comparatively to warn people who braggartly claim to be capable of doing everything, while they surely know that they cannot. Such people do not admit incapability. They boast of being able to do everything. The result their braggart is injury or death. That’s why people warn such individuals saying, ‘A river drowns a swimmer.’

The proverb teaches people to refrain from swearing that they can do everything, even when they really know that they cannot. As such, they must have the humility to understand and accept that there is so much that they do not understand or cannot do. In so doing, they can save their lives, and learn so much from those who understand things.

(Luke 18:10-14; Galatians 6: 2 – 5).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.