239. ULU NHIGAMANAGWA NINADIZILE

Imbuki ya kahaile kenako ilolile munhu uyo ajaga hanhu alinawisagiji bho gupandika matwazo masoga. Aliyo lulu, ahooshika koyi ugapandika makoye badala ya mafumilo miza. Gashinaga lulu, akahayile kenako agayombaga munhu uyo oigaiyagwa iyo olikobhaga.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhadibhegelejaga chiza haho bhatali uguitumama imilimo yabho, guti gwita bhukengeji bho gudula gudebha chiza amafumilo ga milimo yabho yiniyo. Ugukija gwita b’ukengeji guti bhunubho haho bhatali uguitumama imilimo yabho, gugabhenghelejaga gugayigwa iyo bhaliicholaga, na guyomba giki, ‘ulu nhigamanagwa ninadizile.’

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwita bhukengeji bhutale bho milimo yabho, haho bhatali uguitumama imilimo yiniyo. Ubhukengeji bhunubho b’ugubhambilija uguimana na guitumama imilimo iyo idulile gubhenhela matwajo mingi umuwikaji b’ob’o.

Yohane 11:21.

NINGEJUA NISINGEKUJA

Chanzo cha msemo huo chaangalia mtu aliyeenda sehemu fulani akiwa na matumaini ya kupata maendeleo mazuri. Lakini basi, alipofika huko alipata matatizo badala ya mafanikio. Kumbe basi, msemo huo husemwa na mtu aliyekosa kile alichokuwa akikitafuta.

Msemo huo hulinganishwa kwa watu wasiojiandaa vizuri kabla ya kufanya kazi zao, kama vile, kufanya utafiti wa kutosha kuzifahamu kazi ziwezazo kuwaletea maendeleo maishani mwao. Kutokufanya utafiti kama huo, kabla ya kuzifanya kazi zao, hupelekea kwao kukosa kile walichokuwa wakikitafuta, na kusema, ‘ningejua nisingekuja.’

Msemo huo hufundisha watu juu ya kufanya utafiti wa kina kabla ya kuzifanya kazi zao. Utafiti huo utawawezesha watu hao kuzifahamu na kuzitekeleza vizuri kazi zile ziwezazo kuwaletea maendeleo maishani mwao.

Yohane 11:21.

IMG_20190704_091951_3

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.